Hapana
kulazimisha katika Dini
Imetafsiriwa
na Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Ni
wajibu wa kila Muislamu kufahamu kuwa miongoni mwa mafundisho
muhimu na ya msingi yasiyopingika katika dini yaliyomo ndani ya Qurani na ndani
ya mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) ni
kuwa hapana kulazimisha katika dini.
Lazima
afahamu haya kwa sababu kutokana na kuzidi kuenea,
kukubalika na kufuatwa dini hii na watu wengi
Kila
Muislamu anawajibika kuufahamu na kuufikisha ujumbe huu
pamoja na dalili zake kwa kila mtu ili ukweli udhihiri na uongo ujitenge, kisha
baada ya hapo anayetaka kufuata afuate na anayetaka kuendelea kupinga na
aendelee. Hairuhusiwi kwa vyovyote vile kuwatisha watu
wala kuwadhuru ikiwa hawataki kuukubali Uislamu.
Zifuatazo
ni baadhi ya dalili zisizopingika kuhusu maudhui haya:
Mwenyezi
Mungu anasema:
"Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na
upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini
Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua."
Al Baqarah – 256
Na
akasema:
"Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote
waliomo katika ardhi. Je,
wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?."
Yunus – 99
Na
akasema:
"Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio
nifuata. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na
kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu
basi wameongoka. Na wakikengeuka basi juu yako ni
kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja
wake."
Al Imran -20
Na
akasema:
"Haimlazimu Mtume ila kufikisha ujumbe
tu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnacho kidhihirisha na mnacho
kificha."
Al Maidah – 99
Ni muhimu kufahamu pia kuwa aya mbili za mwisho zimeteremshwa Madina, wakati
Waislamu wakiwa na nguvu. Hili lina umuhimu wake ili mtu asiseme kuwa huenda amri hizo ziliteremka Makkah
wakati Waislamu walipokuwa wachache na dhaifu.
Mtu
anaweza kushangazwa akajiuliza: 'Ikiwa dini ya Kiislamu inafundisha mafundisho
haya, nini basi hizi habari tunazozisikia juu ya Jihadi? Tutawafahamisha vipi watu
juu ya vita alivyopigana Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) pamoja na Sahaba zake (Radhiya Llahu anhum)
dhidi ya washirikina?'
Jawabu
ni kuwa; Jihadi 'Vita vitakatifu' vinapiganwa kwa
sababu nyingi, lakini kuwalazimisha watu kuingia katika dini si mojawapo ya
sababu hizo. Sababu asili ya kufaridhishwa Jihadi ni
kuwaruhusu Waislamu kujitetea nafsi zao kutokana na mateso na mauaji na
kufukuzwa majumbani mwao.
Mwenyezi
Mungu anasema:
"Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa
sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.
Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila
kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi
Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za
wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la
Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi
Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu."
Al Hajj
– 39-40
Wengi
miongoni mwa maulamaa waliotangulia wamesema kuwa hizi ni
aya za mwanzo zilizoteremshwa kuhusu Jihadi, kisha zikateremshwa aya zifuatazo:
"Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na
wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu
hawapendi waanzao uadui. Na wauweni popote mwakutapo, na
muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko.
Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.
Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini
iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na
Al Baqarah
– 190-193
Kutokana na aya zilizotangulia tunaona kuwa maana ya Jihadi
ikaongezeka kutoka katika hali ya kujitetea tu na uadui, Waislamu wakaruhusiwa kupambana
na wanaowafanyia uadui na pia wenye kuwanyima uhuru wa kuabudu na kuchagua dini
wanayoitaka wenye na kuwazuwia kuilingania dini
Lakini
katika kuieneza dini, Waislamu wanatakiwa kutumia njia za kielimu usalama na amani pekee kwa kutumia ndimi na kalamu zao. Silaha
hairuhusiwi kutumika isipokuwa dhidi ya wenye kuwazuwia kufanya ibada zao na dhidi ya wenye kuwazuwia Waislamu kuilingania dini
"Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na
Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na
Al
Baqarah –193
Katika
barua aliyomuandikia Heracles mfalme wa Warumi, Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) alimuambia:
"Nakuita katika Uislamu.
Ukiukubali utapata amani. Ukiukubali
Uislamu Mwenyezi Mungu atakulipa mema mara mbili. Na
Sahih
Muslim
Muislamu
akiweza kuufikisha ujumbe kwa watu bila ya pingamizi,
anakuwa keshatimiza jukumu lake. Anayetaka kuamini anakuwa huru kufanya hivyo, na asiyetaka pia yuko huru.
Hata pale
Waislamu wanapolazimika kupigana vita wakafanikiwa kuteka nchi, basi jukumu lao linakuwa kuiweka sheria ya Mwenyezi Mungu katika nchi
hiyo na kuweka haki sawa baina ya watu wote. Waislamu na
wasiokuwa waislamu. Hawana haki ya kuwalazimisha raia kuukubali Uislamu dhidi
ya matakwa
Ingelikuwa
sababu ya kupigana jihadi ni kuwalazimisha watu kufuata
dini ya Kiislamu basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Ssallam)
asingewaamrisha Waislamu kutowashambulia maadui pale wanapoacha kupigana
wakarudi nyuma, na asingekataza kuua wanawake na watoto, na hivi ndivyo
alivyofanya.
Siku moja
katika vita, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu
alayhi wa Ssallam) aliona kundi la watu limejikusanya. Akatuma
mtu kutaka kujuwa kuna nini. Akaambiwa kuwa watu
wameizunguka maiti ya mwanamke aliyeuliwa. Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) akasema:
"Asingeshambuliwa!"
Khalid bin
Al Waliyd (Radhiya Llahu anhu) ndiye aliyekuwa kiongozi wa
majeshi hayo, kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa
Ssallam) alimtuma mtu kwa Khalid akamuambia:
"Muambie Khalid asiue wanawake wala wafanya
kazi."
Sunan
Abi Daud
Hata
katika vita vikali dhidi ya adui, wanaoruhusiwa kushambuliwa na
kuuliwa ni wapiganaji tu.
Ingelikuwa
sababu ya kupigana jihadi ni kuwalazimisha wasioamini
kufuata dini ya Kiislamu basi Makhalifa walioongoka (Radhiya Llahu anhum)
wasingekataza watu kuwaua makasisi na wacha Mungu wasioshiriki katika kuwapiga
vita Waislamu.
Khalifa wa Waislamu Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) akilihutubia
jeshi
"Mtawakuta
watu waliojitenga kwa ajili ya shughuli za ibada tu
(makasisi). Hao waacheni waendelee na wanayofanya na wala msiwadhuru."
Tumekwisha
onyesha hoja mbali mbali kuthibitisha kuwa katika misingi ya mafundisho ya dini
ya Kiislamu ni kuwa hapana kulazimisha katika dini, na
tukaelezea juu ya malengo na sababu za kupigana jihadi, na hivi sasa tutaelezea
juu ya baadhi ya mafundisho yaliyowakanganya baadhi ya watu wakayatafsiri
vibaya.
Moja
katika mafundisho hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu
isemayo:
"Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote
mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni
katika kila njia."
Al
Tawbah -5
Baadhi ya
watu, hasa wale waliojiunga hivi karibuni katika kuandika dhidi ya dini ya Kiislamu
wanadai kuwa eti aya hi inaifuta ile aya isemayo:
"Hapana kulazimisha katika Dini."
Wanadai
kuwa eti aya hii "Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina
popote mwakutapo…", kwa ujumla inataka kila
asiyekuwa muislamu apigwe vita. Wanasema kuwa dalili ni
kuwa aya hii ni katika aya za mwisho kuteremshwa juu ya vita.
Ukweli ni kuwa aya hii haikuletwa kwa ajili ya kufuta msingi wa
mafundisho ya Kiislamu kuwa hapana kulazimishana katika dini. Inaweza kuwa
inaonyesha hivyo katika maneno yake, lakini tafsiri yake inafahamika vizuri kwa kuzisoma aya zilizokamatana na aya hii pamoja na hadithi
zinazoelezea sababu za kuteremshwa kwa aya hii ambazo tutazungumza juu yake
kila tukiendelea mbele na darsa hii.
Waliokusudiwa
katika aya hii ni washirikina wa Kiarabu peke
Aya hii
haizungumzi juu ya washirikina wengine wa Kiarabu
wasiovunja mikataba na wale wasiochukuwa silaha kuwapiga vita Waislamu, na bila
shaka haizungumzi juu ya Mayahudi na Manasara na haizungumzi pia juu ya
washirikina walio nje ya bara ya Arabu.
Tutaweza
kuifahamu vizuri tafsiri ya aya hii tunayoizungumzia ikiwa tutautizama vizuri mfumo
wote wa aya hizi - zile aya zilizo kabla na baada ya
aya hii zilizomo katika Surat al Tawbah.
Aya ya
mwanzo na ya pili katika sura ya Al Tawbah zinasema:
"Huku
ni kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenye jukumu
la maagano na mlio ahidiana nao katika washirikina.
Basi tembeeni katika nchi miezi mine, na jueni kwamba nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na
kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anaye wahizi makafiri."
Al
Tawbah -1-2
Katika aya
hizi tunaona kuwa washirikina walipewa miezi mine ya amani huku wakijulishwa
kuwa baada ya kumalizika miezi mine hiyo mapambano yataanza tena.dhidi
Mwenyezi
Mungu anasema:
"Isipo
kuwa washirikina ambao mliahidiana nao kisha wasikupunguzieni chochote, wala
hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi hao watimizieni ahadi
Al
Tawbah -4
Kwa hivyo katika
aya ya tano Mwenyezi Mungu anaposema:
"Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote
mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni
katika kila njia."
Al
Tawbah -5
Lazima
tuelewe kuwa kuwa aya hii haijumuishi wote wasiokuwa Waslamu na
kwamba aya inazungumza juu ya kundi maalum la washirikina wa Kiarabu waliokuwa
vitani dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) na ni
wale tu waliovunja ahadi.
Haya
yanafahamika vizuri zaidi
"Je,
hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na
hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio walio kuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi
mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini."
Katika
kuifasiri aya hii amesema Ibn Al Arabi:
"Ni
wazi kabisa kuwa maana ya aya hii ni kuwaua
washirikina waliokuwa wakiwapiga vita Waislamu."
Ahkam
al Quran (2/456)
Katka aya
iliyokuja baada ya aya tunayoizungumzia Mwenyezi Mungu anasema:
"Itakuwaje
iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na
mbele ya Mtume wake, ila wale mlio ahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi
maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika
Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu."
Al
Tawbah – 7
Fundisho
lingine waliloshindwa kufahamu maana yake ni hadithi
ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) aliposema:
"Nimeamrishwa
kupambana na watu mpaka wakubali kuwa hapana
anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah, na kwamba mimi ni mjumbe wa Allah. Wakinitii
katika
Bukhari
na Muslim
Hapana
wasiwasi wowote juu ya usahihi wa hadithi hii, kwa
vile imo ndani ya Sahih al Bukhari na Sahih Muslim. Hata hivyo, hadithi hii
haijuzu kufasiriwa kwa ujumla nje ya mfumo wake bila
kujali ushahidi mwingine ulioambatana nayo.
Neno 'Watu' katika hadithi hii haina maana ya watu wote.
Anasema
Ibn Taymiyah:
"Linakusudiwa
tu wale wanaopigana vita dhidi ya Waislamu, wale ambao Mwenyezi Mungu
ameturuhusu kupambana nao. Halikusudiwi wale tulioahidiana nao ambao Mwenyezi
Mungu anatuamrisha kutimiza ahadi zetu.
(Majmû`
al-Fatâwâ (19/20))
Mwenyezi
Mungu anawaamrisha Waislamu wawe waadilifu kwa wenye
itikadi nyingine, yote sawa watu hao wawe Mayahudi au Manasara au washirikina.
Uislamu unatufundisha kuwa wapole nao na kujaribu kufanya
urafiki nao ikiwa hawajachukuwa silaha na kutupiga vita.
Mwenyezi
Mungu anasema:
"Mwenyezi
Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale
ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika
Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.
Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na
wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao
marafiki basi hao ndio madhaalimu."
Al-Mumtahanah: 8-9
Mwenyezi Mungu anawaamrisha Waislamu kuwaheshimu
wazazi wao wasiokuwa Waislamu na kuishi nao kwa kwema.
Qurani inatufundisha kujadiliana nao kwa njia nzuri.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Wala msijadiliane na Watu wa
Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu
miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na
yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni
Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake."
Al-`Ankabût: 46
Tunaamrishwa pia kutimiza ahadi zilizo baina yetu na wasiokuwa Waislamu na kwamba tusiwaendee kinyume wala
kuvuka mipaka dhidi
Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swallah Llahu alayhi wa Ssallam) alitupa onyo kali
"Yeyote atakayemuua katika wale tulio na mikataba ya amani nao hatoionja harufu ya Peponi."
Sahih Muslim
Mtu haukubaliwi uislamu wake ikiwa hajaiamini Mitume
yote walioletwa kabla yake (Swallah Llahu alayhi wa
Ssallam).
Mwenyezi Mungu anasema:
"Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume
wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho
kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na
Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi
huyo amekwisha potelea mbali."
Al Nisaa -136