JIHAAD

Simba na Chui 1

Al Wahan.. 3

Neno Jihadi 5

Sheria ya Jihadi 5

Kuwaajib.. 8ika

Fardhi Ayni 8

kiongozi 9

inapokuwa Fardhi 10

Wanaowajibika

Ruhusa ya Wazee. 14

Ruhusa kwa mwenye deni 14

Msaada wa makafiri 15

Msaada wa watu dhaifu.. 15

Fadhila za Jihadi 16

Ibada bora.. 16

Watu bora.. 17

Mujaahidiyn.. 17

Daraja mia Peponi 18

Thamani ya Jihadi 18

Kufa Shahiyd.. 19

Mashahidi aina saba.. 21

Kulinyanyua neno

Nia 22

Fadhila za kulinda mipaka.. 24

 

Fadhila za Kurusha

Wajibu wa viongozi

Usia kwa viongozi 27

Usia wa Umar

Dua

Kupigana Jihadi 29

Kuwa thabiti 37

Kukimbia vitani 38

Hadaa vitani 39

Rehma Vitani 39

Simba na Chui   

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Mtakapouziana kwa riba, mkajishughulisha na biashara, mkaridhika na kilimo, na mkaiacha jihadi (wakati wenzenu wanauliwa), Mwenyezi Mungu atakuteremshieni udhalilifu mtakaoshindwa kuuondoa mpaka (pale) mtakaporudi katika dini yenu.

Abu Daud na Imam Ahmed

   

Na imetolewa na Muslim na Abu Daud na An Nasaai na Al Haakim na Al Bayhaqiy kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) pia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Atakayekufa bila kupigana (jihadi) na wala (hata) kumpitikia moyoni mwake (nia ya kupigana) jihadi, (akifa) anakufa akiwa na sehemu ya unafiki.

   

Waislamu ni umma uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuuongoza ulimwengu na walimwengu na kulinyanyua juu neno la Mwenyezi Mungu, lakini Waislamu leo wamekuwa watu dhalili kupita umma zote zinazotembea juu ya ardhi. Kila anayetaka kuzifanyia silaha zake majaribio au kujipima nguvu, anazielekeza silaha hizo na nguvu hizo kwa Waislamu. Tumeyaona hayo yakitokea sehemu mbali mbali ulimwenguni, zikiwemo Bosnia, India, Afghanistan, Palastina na sasa Iraq, na hivi sasa Ghaza.

    Kote huko na katika sehemu mbali mbali ulimwenguni Waislamu wanadhalilishwa, wanauliwa, watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume, na majumba yao yanabomolewa mbele ya kamera za television na mbele ya macho ya kila mtu, bila watu kujali wala hata nyoyo kusituka. Kisha Waislamu hao hao eti wanakimbilia kupeleka mashitaka yao Umoja wa Mataifa wakitegemea kupata msaada, wakati wote hao (Marekani, Mayahudi na Umoja wa Mataifa) ni kitu kimoja.

Na hii inanikumbusha kile kisa cha chui na kima:

Inasemekana kuwa chui alikuwa akipenda kumuonea kima na kumpiga bila sababu yoyote, na kila anapomuona alikuwa akitafuta kisingizio chochote cha kumpiga makofi ya uso kima yule.

Alikuwa mara nyingine akimwambia; Kofia yako iko wapi! Mbona leo hujavaa kofia, si nilikwambia lazima uivae? Kesho lazima nikuone nayo, humwambia hivyo huku akimtandika makofi na mateke.

Siku ya pili kima anapokuja akiwa amevaa kofia, chui yule yule humvamia na humpiga makofi huku akimwambia:

Kwa nini umevaa kofia! Si nilikwambia usiivae?  akiivaa anapigwa na asipoivaa anapigwa.

Hali ikaendelea hivyo mpaka siku ile kima alipochoka kuonewa, akaamua kumshitaki chui kwa mfalme simba bila kujuwa masikini kuwa simba na chui wote ni kitu kimoja.

Mfalme simba akamwita chui pembeni na kumwambia kwa kumnong'oneza:

Wewe vipi ndugu yangu! unampiga mwenzio bila kumtafutia kisingizio kinachokubalika? Tizama mimi kwa mfano; ninapotaka kumpiga punda nafanya nini? Humtuma aniletee matufaha, na yeye bila kuniuliza hukimbia na kuniletea matufaha mekundu, mimi hapo humtandika makofi na kumwambia:

Nani aliyekuaambia uniletee matufaha mekundu?

Hapo yeye hukimbia na kurudi haraka akiwa ameniletea matufaha ya kijani, na hapo namtandika tena makofi na kumwambia:

Nani aliyekwambia uniletee matufaha ya kijani? na kwa njia hii namtandika makofi kwa raha zangu.

Chui akaona kuwa hii ni fikra nzuri, akaondoka na kwenda moja kwa moja mpaka kwa kima akamwambia:

Nenda kaniletee matufaha sasa hivi, tena mbiyo!

Lakini kima anakhitalifiana na punda, kima alimuuliza chui:

Unata nikuletee matufaha rangi gani? Mekundu au kijani au manjano?

Chui kuona ameshindwa hila akarudia pale pale:

Mbona leo hujavaa kofia eh?, Ngumi! Teke!

   Na hii ndiyo hali yetu Waislamu baada ya kuyaacha mafundisho ya dini yetu, na kuiacha jihadi na kuyakimbilia maisha ya dunia, Mwenyezi Mungu ametusalitishia udhalili ikawa kila safihi anapotaka kujipima nguvu zake anakuja kututandika sisi ngumi na makofi yake, na sisi tunakimbilia kwa mfalme Simba (Mmarekani) au kwa chui (Umoja wa Mataifa) na kumbe wote hao ni kitu kimoja waliokwishaamua kumpiga vita kila anayetaka kuisimamisha bendera ya Laa ilaaha illa Llah.

    Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusimamishie kiongozi wa kheri, awe katika utawala wake kiongozi huyo anaheshimiwa kila mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu, na anadhalilishwa kila mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu. Awaunganishe umma chini ya bendera ya Laa ilaaha illa Llah na kuihuisha Jihadi ambayo kwayo pekee umma huu utarudisha heshima yake - Amin.

 

Al Wahan

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

"Hivi karibuni mtakuja zungukwa na mataifa, mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao (wanavyokaa kuizunga sinia ya chakula)." Tukasema: "Kwa sababu ya uchache wetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu siku hiyo?" Akasema: "Hapana, nyinyi siku hiyo mtakuwa wengi, lakini mtakuwa (mumegawanyika) muko mbali mbali mfano wa takataka zinazokumbwa na maji ya mvua. Mwenyezi Mungu ataondoa haiba yenu kutoka katika vifua vya adui yenu, na ataingiza ndani ya nyoyo zenu Al Wahan (udhaifu)." Mmoja akauliza: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kitu gani hiki Al Wahan?" Akasema: "Kuipenda kwenu dunia na kuyachukia mauti."

Imam Ahmed katika Musnad yake

 

Hadithi hii ni muujiza katika miujiza ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) juu ya hali yetu hivi sasa. Kama kwamba alipokuwa amekaa pale msikitini kwake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akihadithia hadithi hii, alikuwa akiiona hali yetu hivi sasa kama tulivyo.

Maadui wa Waislamu wanatutuhumu kuwa tunaongezeka kwa wingi, na wanazihadaa serikali zetu zikubali kutupa dawa za kuzuwia uzazi. Hii ina maana kuwa idadi yetu inaongezeka, lakini juu ya wingi wetu, hatuna maana yoyote. Hatuna faida yoyote. Maadui wa Mwenyezi Mungu wanatuuwa, wanatudhalilisha, wanatutenganisha, wanatugawa, wanatugombanisha, na sisi hatuna la kufanya, bali hatuwezi kufanya kitu. Wanatusukuma wanapotaka, na wanatuendesha wanavyotaka. Tumekuwa mfano wa takataka zinazokumbwa na kusukumwa na maji ya mvua huku na kule.

 

Na muujiza mwingine uliomo ndani ya hadithi hii ni kule kuungana dhidi yetu kwa mataifa yote. Wamarekani, wazungu wa Ulaya, Mayahudi, Wajapani na maadui wa Mwenyezi Mungu walioko Magharibi na Mashariki ya ulimwengu, wote wamejikusanya na kutuzunguka, mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao. Wote wamekula kiapo kuupiga vita Uislamu. Wakati huo huo sisi tumo katika starehe zetu, kama kwamba hapana kinachotokea. Kila mmoja anakiogopea kiti chake, anaiogopea mali yake, anauogopea mustakbali wake, anaiogopea nafsi yake. Tunaipenda dunia na tunayachukia mauti.

 

Tunafaidika na hadithi hii pia ile balagha, ule ubingwa wa kutumia lugha uliotumika katika kuwaelezea maadui wa Mwenyezi Mungu, pale (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema: "mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao." Na hii inatuonyesha njaa waliyonayo maadui hawa, na tamaa yao kubwa juu ya mali za Waislamu na utajiri wao. Wanakuja kwa nguvu zao zote na kwa ujabaruti na ujeuri mkubwa na kibri huku wakiwasaidia Mayahudi kwa nguvu zao zote ili waweze kuzinyakua mali hizo na uchumi huo na ardhi.

Na muujiza mwingine ni kule kufanya kwao wanavyotaka bila kujali masikitiko yetu wala huzuni zetu wala lawama zetu wala hata vilio vyetu. Wanafanya wanavyotaka. Wanapiga wanavyotaka, wanabomoa wanavyotaka, kama kwamba ardhi yote na Waislamu wote ni milki yao. "Mfano wa walaji wanavyokizunguka chakula chao."

 

Hata Masahaba (Radhiya Llahu anhum) walishangazwa waliposkia, wakauliza:

"Kwa sababu ya uchache wetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu siku hiyo?" Walishanga. Vipi tutakuwa katika hali hii, vipi maadui wataweza kutupiga wakati idadi yetu ni kubwa kupita yao. Bila shaka tutakuwa wachache wakati huo. Lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akawaambia: "Hapana, (bali) nyinyi siku hiyo mtakuwa wengi, lakini mtakuwa mumefarakana mfano wa takataka zinazokumbwa na maji ya mvua."

 

Izingatie vizuri kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema "nyinyi siku hiyo mtakuwa wengi", na hii maana yake ni kuwa mwili wa Waislamu ni mwili mmoja. Tokea wakati ule mpaka wakati huu, sisi sote ni kitu kimoja.

" "

Mfano wa Waislamu katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao ni mfano wa mwili mmoja, kinapoumia kiungo kimoja basi viungo vyote vilivyobaki vinashirikiana (nacho kiungo hicho) kwa homa na kukesha.

Bukhari na Muslim

 

Hivi ndivyo alivyotufundisha Mtume wetu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)

 

Na katika hadithi hii ya kuzungukwa na maaduwi tunaweza kuujuwa ugonjwa wetu na pia kuijuwa dawa yetu.

Maradhi yetu ni kuwa mbali na Mwenyezi Mungu, mfarakano wetu, na kuipenda kwetu dunia.

Na dawa yetu ni kurudi kwa Mola wetu Subhanahu wa Taala. Turudi katika dini yetu. Tuirudishe imani yetu na kumtegemea Mwenyezi Mungu peke Yake. Tumuogope Yeye tu, na tuache kuuogopa uluwa na mali na ufalme na vitu kama hivi visivyo na thamani yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Tuache kuuthamini ulimwengu na kuyaogopa mauti.

Tuwalee watoto wetu malezi ya Kiislamu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na ya Mtume Wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Tuwafundishe taariykh yetu.

Kurudi kwa Mwenyezi Mungu na kurudi katika mafundisho ya dini Yake ndiyo jambo la pekee linaloweza kuturudishia heshima yetu na utukufu wetu.

Maana ya neno Jihadi

    Neno Jihadi, asili yake linatokana na juhudi, tabu, mashaka. Kwa mfano tunasema; Amejitahidi, amefanya juhudi, yaani amezitumia nguvu zake na uwezo wake wote katika kutimiza jambo fulani, na haya yote yanapatikana katika mapambano ya kivita.

 

Sheria ya Jihadi

    Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kwa watu wote, akamuamrisha kuwalingania katika uongofu na katika dini ya haki, na wakati wote alipokuwa Makka alikuwa akiwalingania watu kwa hekima na kwa mawaidha mema, na kwa ajili hiyo ilibidi apambane na kila aina ya uadui, udhia na mateso kutoka kwa watu wa kabila lake baada ya kuuona utukufu na uluwa wao umo hatarini.

    Wakati wote huo Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala alimtaka awe akipambana na uadui huo kwa subira, uvumilivu na kwa kusamehe msamaha mzuri.

Mwenyezi Mungu anasema:

Basi msamehe msamaha mzuri (kila anayekufanyia ubaya).

Al Hijr 85

 

Na akasema:

Na ungoje hukumu ya Mola wako, na hakika wewe uko mbele ya macho Yetu.

At Tur 48

 

Na akasema:

Basi wasamehe wewe na uwambie (maneno ya) salama.

Az Zukhruf 89

 

Na akasema:

Waambie wale walioamini wawasamehe wale wasioziogopa siku za Mwenyezi Mungu (za kuwatia adabu wabaya).

Al Jathiyah - 14

 

    Mwenyezi Mungu hakumtaka Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aukabili ubaya wao kwa ubaya, wala udhia kwa udhia na wala hakumuamrisha kuwapiga vita wanaoipiga vita daawa hiyo, au kuwapiga vita wale wanaowatesa Waislamu, bali alikuwa akimwambia Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam):

 

Ondosha mabaya (unayofanyiwa) kwa (kulipa) mema; Sisi tunajua wanayoyasema.

Al Muminun 96

 

Muda wote huo Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala alimuamrisha Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) apigane jihadi kwa Qurani na kwa hoja zilizo wazi.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Na ushindane nao kwa (Qurani) hii mashindano makubwa.

Al Furqan 52

 

    Lakini baada ya kupita miaka kumi na tatu huku mateso yakiongezeka, na makafiri kuzidisha uonevu na kuwadhalilisha Waislamu, na hatimaye kufanya njama za kumuuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hata akalazimika kuhamia Madina na kuwaamrisha Masahaba wake (Radhiya Llahu anhu) pia kuhamia huko, hapo ndipo Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Alipoteremsha kauli Yake isemayo:

 

Na (kumbuka ewe Muhammad) walipokufanyia hila wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe, na wakafanya hila (zao barabara) Na Mwenyezi Mungu akazipindua hila hizo. Na Mwenyezi Mungu ni mbora wa kupindua hila (za watu wabaya).

Al Anfal 30

 

Kisha Akasema:

 

Kama hamtomnusuru (Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), basi Mwenyezi Mungu alimnusuru.

At Tawba 40

 

    Baada ya kuhamia Madina, makao makuu ya dola mpya ya Kiislamu, na baada ya makafiri kuwaendea huko huko na kuwafanyia mbinu na hila mbali mbali, ndipo Mwenyezi Mungu aliipotoa amri ya kupigana Aliposema:

39 40 41

Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa. Na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.

Ambao wametolewa majumbani (mijini) mwao pasipo haki ila kwa sababu wanasema Mola wetu ni Mwenyezi Mungu.

Na kama Mwenyezi Mungu asingaliwakinga watu, baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangalivunjwa mahekalu na makanisa na nyumba nyengine za ibada na misikiti ambamo jina la Mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi. Na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayesaidia dini yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda.

Wale ambao tukiwamakinisha (tukiwaweka uzuri) katika ardhi husimamisha Sala na wakatoa Zaka na wakaamrisha yaliyo mema na wakakataza yaliyo mabaya. Na marejeo ya mambo ni kwa Mwenyezi Mungu.

Al Hajj 39 41

 

Katika aya hizi zimetajwa sababu tatu ambazo kwa ajili yake Mwenyezi Mungu ametoa ruhusa ya kupigana vita:-

 

    Ya kwanza - Kwa sababu ya kudhulumiwa kwa kushambuliwa na kutolewa majumbani mwao pasipo haki kwa sababu wanasema Mola wetu ni Mwenyezi Mungu.

    Ya pili Lau kama Mwenyezi Mungu asingaliwakinga kwa kuwaamrisha kupigana jihadi, bila shaka yangalivunjwa mahekalu na makanisa na nyumba nyengine za ibada na misikiti ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu hutajwa kwa wingi.

    Ya tatu Sababu ya Waislamu kupewa nusura ya Mwenyezi Mungu na kumakinishwa (kuwekwa uzuri) katika ardhi ni kwa ajili ya Kusimamisha Swala na Kutoa Zaka na Kuamrisha mema na Kukataza mabaya.

Jihadi ni Waajib

    Jihadi imefaridhishwa katika mwaka wa pili wa Hijra aliposema Mwenyezi Mungu:

Mumelazimishwa kupigana vita (kwa ajili ya dini). Nalo ni jambo zito kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua, (lakini) nyinyi hamjui.

Al Baqarah 216

Kupigana Jihadi ni Fardhi Kifaya na wakati mwingine inakuwa Fardhi Aiyn.

Fardhi Ayni

    Fardhi aiyn ni yale ambayo kila Muislamu analazimika kuwa nayo au kuyatenda, na hasameheki asiyetenda hata kama kundi la watu wengine watalisimamia jambo hilo na kulikamilisha, kwa mfano; Imani, SWala, Tohara, Kutoa Zaka, Kufunga, Kuhiji nk. Haya yanaitwa Fardhi aiyn na kila Muislamu analazimika kuwa nayo au kuyatenda na si halali kwa mtu yeyote kutoyapa umuhimu.

 

Maana ya Fardhi Kifaya

    Ama Fardhi kifaya ni yale matendo ambayo Waislamu wanalazimika kuyatenda ingawaje si lazima litendwe na Waisalmu wote, kwani linapotendwa na kundi miongoni mwao, basi waliobaki wanasameheka, kwa mfano;

KATIKA DINI;

Kujifunza elimu ya dini kwa ajili ya kuwasomesha wengine, Kumswalia maiti, Kuadhini nk.

KATIKA MAISHA;

Kulima, Utabibu, Ufundi na yaliyo na mfano wake, mambo ambayo yakikosekana, maisha ya wanadamu yanakuwa hatarini.

 

 

Yanayomhusu kiongozi

    Kama vile kuamrisha mema, kukataza mabaya, Kuitisha Jihadi, na Kuyapiga vita maovu na yale yaliyoharamishwa nk.

 

    Jihadi inaingia katika Fardhi kifaya ambayo haimwajibikii kila mtu iwapo litatokea kundi la watu miongoni mwao litakaloweza kuwapiga vita maadui na kuiondoa shari yao bila kuhitajia msaada wa waliobaki.

 

    Katika kutafuta elimu, Mwenyezi Mungu Anasema:

Wala haiwapasi Waislamu kutoka wote (katika miji yao wakaja Madina wakaiwacha miji yao mitupi). Lakini kwa nini halitoki kundi (tu) katika kila taifa miongoni mwao (lende Madina kwa Mtume) kujitalimisha vyema dini na (kisha wakaja) kuwaonya weziwao (waliosalia makwao) watakapowarudia, ili wapate kujihadharisha (na wao na mabaya).

At Tawba 122

 

Ama kuhusu Jihadi, Mwenyezi Mungu Anasema:

Enyi Mlioamini! Shikeni hadhari yenu (juu ya maadui zenu msikhadaike). Tokeni (kwenda vitani) makundi moja moja au tokeni nyote pamoja (kama atakavyokuambieni Mtume).

An Nisaa 71

 

Na Akasema:

Hawawi sawa Waislamu wanaokaa wasende vitani, isipokuwa wenye dharura. (Hawawi sawa) na wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na kwa nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewafadhilisha katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na kwa nafsi zao kuliko wakaao (wasende kupigana). Ingawa Mwenyezi Mungu ameahidi wote (kupata) wema. Lakini Mwenyezi Mungu amewafadhilisha wale wapiganao kuliko wakaao kwa ujira mkuu.

An Nisaa 95

 

    Na katika Sahihi Muslim kutoka kwa Abu Said Al Khudary (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa; Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alituma ujumbe kwenda kwa watu wa kabila la Hudhayl kuwaambia; Atoke (kwenda vitani) katika kila wawili mtu mmoja na ujira watapata wote wawili.

Sahih Muslim Kitab al Imara mlango wa Fadhail ianat al ghazi fiy sabili Llah hadithi nambari 38

 

Na hii ni kwa sababu ikimwajibikia kila mtu, basi mambo mengi ya kidunia yenye maslahi kwa wanadamu yataharibika, ndiyo maana ikawajibika kwa baadhi yao tu.

 

Jihadi inapokuwa Fardhi

    Jihadi inakuwa Fardhi aiyn katika sehemu tatu;

Ya kwanza ni pale mwenye kuwajibika kupigana anapokuwa vitani keshasimama katika msitari pamoja na wenzake, hapo analazimika kupigana.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Enyi mlioamini! Mkutanapo na jeshi (la makafiri) kazaneni barabara (wala msikimbie).

Al Anfal 45

 

Na Anasema:

Enyi Mlioamini! Mkikutana na waliokufuru vitani msiwageuzie mgongo.

Al Anfal - 15

 

Ya pili Adui anapoingia katika nchi ya Kiislamu, wanalazimika watu wote wa nchi hiyo kwa pamoja kutoka na kupambana naye, na si halali kwa mtu yeyote kurudi nyuma asitimize wajibu wake huo wa kupigana na adui, na hii ikiwa haiwezekani kumtoa adui huyo bila kushirikiana wote kwa pamoja.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Enyi mlioamini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu (kwanza kwani ndio wenye madhara na nyinyi zaidi), na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mungu.

Al Tawba 123

 

Ya tatu Mwenye kuhukumu anapotangaza Jihadi analazimika kila mwenye kuwajibika kupigana kuuitikia mwito huo, na haya yanatokana na hadithi iliyosimuliwa na Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) aliposema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Hapana kuhajir tena (kutoka Makka kwenda Madina) baada ya Waislamu kuuteka (mji wa Makka) isipokuwa (kilichokuwepo ni) jihadi na nia (ya kupigana jihadi), na mnapoitwa muitikie (mwito).

Sahih Bukhari juzu ya 2 mlango wa Fadhila za jihadi. Hadithi nambari 2631

Na maana yake ni kuwa mnapotakiwa kwenda kupigana Jihadi, basi lazima muitikie mwito huo.

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:

Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa Nendeni (kupigana) kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je, mumekuwa radhi na maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kwa (mkabala wa maisha ya) Akhera ni kidogo tu.

At Tawba 38

 

Wanaowajibika kupigana

    Anawajibika kupigana jihadi kila Muislamu mwanamume, mwenye akili timamu, aliyekwishabaleghe, mwenye afya njema mwenye uwezo wa kuwaachia watu wake kiasi cha mali inayowatosha mpaka pale atakaporudi.

Kwa hivyo haimwajibikii asiyekuwa Muislamu, mwanamke, mtoto mdogo, mwenda wazimu na mgonjwa, na kwa ajili hiyo hana lawama yeyote katika hawa asipoutikia mwito wa jihadi kutokana na udhaifu wao au umasikini wao au umri wao au kutokuwa na akili zao ambao huenda kuwepo kwao katika uwanja wa mapambano kukasababisha madhara zaidi kuliko manufaa.

Mwenyezi Mungu Subahanahu wa Taala Anasema:

Hapana lawama kwa wanyonge, wagonjwa, na wasio pata cha kutumia, maadamu wanamsafia nia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapana njia ya kuwalaumu wanao fanya wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

At Tawba - 91

 

Na Anasema:

Kipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama.

Al Fat-h 17

Na kutoka kwa Abdullah bin Omar (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

Nilipelekwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) siku ya Uhud (aniruhusu nikapigane) na wakati huo nilikuwa na umri wa miaka kumi na nne lakini hakuniruhusu.

Fathul Bari sharhi ya Sahih Bukhari Juz. 5 kitabu cha Ushahidi, mlango wa kubaleghe kwa watoto na ushahidi wao.

Sahih Muslim kitabu cha Imara mlango unaobainisha kubaleghe hadithi nambari 1868

Na hii ni kwa sababu jihadi ni ibada na haimwajibikii isipokuwa aliyebaleghe.

 

Imeelezwa na Maimam Ahmed na Bukhari kutoka kwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha) kuwa amesema:

Nilisema (Nilimuuliza) - ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu; wanawake wanawajibika kupigana jihadi? akanijibu: Jihadi (yao ni ile) isiyokuwa na kuuana ndani yake - Hija na Umra.

Musnad ya Imam Ahmed juz. 6 Hadithi za Bibi Aisha (Radhiya Llahu anhu)

Fathul Bari Sharhi ya Sahih Bukhari Juz. 4 mlango wa Hija ya wanawake.

Na katika riwaya nyingine kuwa alisema:

Lakini jihadi iliyo bora ni Hija iliyokubaliwa.

 

Imesimuliwa na Al Waahidi na Al Sayutiy katika Al Dur al Manthur kuwa Mujahid amesema; Ummu Salamah (Radhiya Llahu anha) alisema; Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), (kwa nini) wanaume (tu) wanateka miji (wanapigana jihadi) na sisi hatuteki na sisi tunapata nusu ya urithi (tu)?

Mwenyezi Mungu akateremsha kauli Yake:

Wala msitamani alicho wafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

An Nisaa 32

Imepokelewa pia kutoka kwa Ikrimah (Radhiya Llahu anhu) kuwa alisema:

"Wanawake waliuliza juu ya jihadi wakasema: Tunatamani lau Mwenyezi Mungu angejaalia na sisi pia tuwe tunapigana jihadi ili tupate cho chote katika ujira (mwema) kama wanavyopata wanaume. Ndipo Mwenyezi Mungu alipoiteremsha aya hiyo.

Hata hivyo hapana ubaya ikiwa wanawake watatoka kwa ajili ya kuwatibia walioumia au kwa ajili ya shughuli za mfano wake.

 

Kutoka kwa Anas (Radhiya Llahu anhu) amesema; Siku ya (vita vya) Uhud Waislamu walishindwa wakiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), nilimuona (siku hiyo Bibi) Aisha binti Abubakar na Ummu Suleyum wakiwa wamekunja mikono ya kanzu zao nikiviona visigino vya miguu yao (huku wakiwa wanakwenda mbio) huku (na kule) wakibeba viriba vya maji migongoni mwao na kuwanywesha watu, kisha wanarudi na kuvijaza tena kisha wanarudi kuwanywesha watu (tena).

Bukhari juz. 2 Kitabu cha Jihadi, mlango wa Kupigana jihadi wanawake pamoja na wanaume. Hadithi nambari 2724

Muslim juz. 3 Mlango wa Kupigana jihadi wanawake pamoja na wanaume. Hadithi nambari 1811

 

Kutoka kwa Anas pia anasema;

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akipigana vita akiwa pamoja na Ummu Suleyum na wanawake wengine katika watu wa Madina, waliokuwa wakiwanywesha watu maji na kuwatibia majeruhi.

Muslim juz.3 Mlango wa Kupigana jihadi wanawake pamoja na wanaume. Hadithi nambari 1810

Abu Daud juz. 3 mlango wa Wanawake wanapigana vita. Hadithi nambari 2529

Attirmidhiy juz. 3 mlango wa Wanawake kwenda vitani hadithi nambari 1623

 

Ruhusa ya Wazee

Jihadi iliyowajibika haihitajii ruhusa ya wazee, ama jihadi ya kujitolea lazima ipatikane ruhusa ya wazee wawili au ya mmoja wao.

Amesema Ibni Masaud (Radhiya Llahu anhu):

Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam); Amali (ibada) ipi inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu?

Akasema:

Swala katika wakati wake.

Nikamuuliza (tena):

Kisha ipi?

Akaniambia:

Kuwatii wazee wawili.

Nikamuuliza (tena):

Kisha ipi?

Akaniambia:

Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Sahih Bukhari juz.1 Kitabu cha Nyakati za Sala, mlango wa Fadhila za kusali katika wakati wake, hadithi nambari 504

Sahih Muslim juz. 1 Kitabu cha Imani, mlango wa Imani juu ya Mwenyezi Mungu ndiyo amali bora kupita zote, hadithi nambari 85

 

Na Ibni Omar (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Alikuja mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kumuomba amruhusu kwenda kupigana jihadi, akamuuliza; Wazee wako wahai? Akasema; Ndiyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia: Basi jihadi yako iwe katika (kuwahudumia) wao.

Abu Daud na Annasai na Attirmidhy aliyeisahihisha.

 

Na katika kitabu kiitwacho Shar-atul Islam, (imeandikwa):

Na haijuzu kwenda kupigana jihadi isipokuwa yule tu asiyekuwa na matatizo ya kuwahudumia wanawe na wazee wake, kwa sababu hayo ni bora kuliko kupigana jihadi, bali ndiyo jihadi iliyo bora.

(Bila shaka hii ni katika jihadi isiyowajibika, ama katika jihad ya fardh aiyn yaani jihadi iliyowajibika, basi hapana haja ya kuomba ruhusa kwa mtu yeyote kama ilivyotangulia kuelezwa).

 

Kumuomba ruhusa mwenye deni

Haruhusiwi kwa anayedaiwa kwenda katika jihadi isiyowajibika isipokuwa baada ya kumuomba ruhusa mwenye kumdai au aweke rahani mali inayotosheleza kulipa deni hilo au aweke mdhamini, kwa sababu katika hadithi ya Abu Qatadah (Radhiya Llahu anhu) iliyomo ndani ya kitabu cha Imam Ahmed na pia katika Sahih Muslim (aliulizwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)): Unaonaje nikiuliwa katika (jihadi) katika njia ya Mwenyezi Mungu, nitasamehewa madhambi yangu yote?

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

Ndiyo (utasamehewa) ikiwa utauliwa ukiwa katika subira huku ukitegemea ujira mwema (kutoka kwa Mwenyezi Mungu), isipokuwa (kama una) deni, hakika Jibril ameniambia hayo (hivi punde).

Ahmed na Muslim

 

Kutoka kwa Abdullah bin Omar (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Mwenyezi Mungu anamghufiria aliyekufa shahiyd madhambi yake yote isipokuwa deni.

Pamoja na deni zinaingia pia dhulma alizowadhulumu watu, kama vile kuuwa na kula mali za watu pasipo haki na mfano wake.

 

Msaada wa makafiri

Inajuzu kutaka msaada wa wanafiki na wavunjao amri katika vita dhidi ya makafiri, na hii ni kwa sababu Abdullahi bin Ubay na wanafiki wenzake walikuwa wakienda vitani pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na pia kisa cha Abu Muhjan al Thaqafi aliyekuwa mlevi, aliyepigana katika vita dhidi ya dola ya Kifursi ni mashuhuri sana.

Ama kutaka kupigana vita pamoja na makafiri, jambo hili lina khitilafu ndani yake miongoni mwa maulamaa wa Kiislamu.

Ma Imam Malik na Ahmed wanasema:

Haijuzu kutaka msaada wao, wala kusaidia katika jambo lolote.

Imam Maalik akaongeza:

Isipokuwa kama watakuwa wakiwahudumia Waislamu tu, hapo inajuzu.

Imam Abu Haniyfa yeye anasem:

Inawezekana kutaka msaada wao na wanaweza kutoa msaada wowote ule sharti uwe Uislamu ndio wenye nguvu, ama ikiwa ushirikina ndio wenye nguvu, basi inachukiza.

Imam Shafi yeye anasema:

Inajuzu kwa masharti mawili;

Kwanza Waislamu wawe wengi na washirikina wawe wachache.

Pili Wawe wanajulikana washirikina hao kuwa wana fikra nzuri na muelekeo mzuri juu ya Uislamu. Na watakapotakiwa msaada wao, wasipewe katika sehemu ya ngawira, bali wapewe malipo maalum bila kushirikishwa katika ngawira.

 

Msaada wa watu dhaifu

Kutoka kwa Mus'aab bin Saad bin Abi Waqaas amesema:

Baba yangu alidhani kuwa ana fadhila zaidi kuliko waliokuwa chini yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

Kwani mungepata ushindi na kupata riziki bila ya (dua za) madhaifu miongoni mwenu?

Bukhari na Annasai

 

Katika Annasai imeandikwa kwa lafdhi ifuatayo:

Hakika Mwenyezi Mungu huwanusuru umma huu kwa madhaifu wao, kwa Dua zao na Swala zao na ikhalsi yao.

 

Na kutoka kwa Abu al Darda-a (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:

Niitieni masikini wenu, kwa hakika mnapata rizki na mnapata ushindi kwa (dua) za madhaifu wenu.

Maimamu wote wa Ahlus Sunnah

 

Kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Huenda mwenye nywele zilizotimka (kwa umasikini), anayefukuzwa milangoni (kwa kudharauliwa) anapomuomba Mwenyezi Mungu atamkubalia (dua yake).

Ahmed na Muslim

 

Fadhila za Jihadi

Ibada bora

Fadhila zinazopatikana katika Kupigana Jihadi isiyokuwa ya waajib kwa ajili ya kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuimakinisha hidaya Yake juu ya ardhi, na kwa ajili ya kuimakinisha dini ya haki ni nyingi kupita fadhila zinazopatikana katika kuhiji Hija ya nyongeza baada ya mtu kuhiji Hija yake ya lazima, au Umra ya nyongeza, au Swala za Sunnah au Saumu ya Sunnah.

Juu ya yote hayo, jihadi imekusanya kila aina ya ibada za kiroho na kiwiliwili, kuikinai dunia, kuihama nchi na kuyahama matamanio na hii ndiyo maana ikapewa jina la Ucha Mungu, kwani imekuja katika hadithi kuwa; Ucha Mungu wa umma wangu ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Na ndani yake mna kuitakasa nafsi, kuitakasa mali, na kumuuzia Mwenyezi Mungu nafsi, na haya yote ni matunda ya mapenzi na imani na yakini na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

Mwenyezi Mungu anasema:

 

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

At Tawba - 111

 

Dini ya Kiislamu imeitukuza ibada hii ya Jihadi, na ikatunabahisha juu umuhimu wake katika sura nyingi zilizoteremshwa Madina na ikawalaumu wanaoiacha na wanaoipinga na kuwapa sifa za unafiki na wenye maradhi moyoni.

 

Watu bora

Kutoka kwa Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Nikujulisheni juu ya aliye bora kupita wote? Mtu aliyeshika hatamu za farasi wake (akimuelekeza) katika njia ya Mwenyezi Mungu (kupigana jihadi). Nikujulisheni juu ya anayefuatiya? Mtu aliyejitenga akiwa na mbuzi wake akitoa haki ya Mwenyezi Mungu katika mbuzi hao. Nikujulisheni juu ya mtu muovu kupita wote? Mtu anayeombwa kwa jina la Mwenyezi Mungu kisha hatowi (juu ya kuwa anao uwezo).

Alipoulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam): Mtu yupi aliye bora?

Akajibu: Muislamu anayepigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi yake na mali yake.

Wakamuuliza: Kisha yupi?

Akasema: Muislamu katika bonde mojawapo akimcha Mwenyezi Mungu na anawaepusha watu na shari yake.

 

Pepo kwa ajili ya Mujaahidiyn

Amehadithia Attirmidhiy kuwa mtu mmoja alitamani ajitenge (awe mbali na watu huku akifanya shughuli za ibada peke yake), akamuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) juu ya jambo hilo, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

Usifanye hivyo, kwa sababu mmoja wenu anaposimama (tu) katika njia ya Mwenyezi Mungu (wakati wowote anapokuwa katika jihadi), ni bora kuliko akiswali nyumbani kwake muda wa miaka sabini. Hampendi nyinyi Mwenyezi Mungu akughufirieni kisha akuingizeni Peponi? Piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu. Atakayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu (muda wa) kiasi cha kumkamua ngamia maziwa tu, imemwajibikia Pepo.

Attirmidhy

 

Daraja mia Peponi

Kutoka kwa Abu Saiyd al Khodary (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Ewe Abu Saiyd! Atakayeridhika kuwa Mola wake ni Allah, na Islamu dini yake, na Muhammad Mtume wake, amewajibika kuingia Peponi.

Abu Saiyd akastaajabu kwa maneno hayo akasema:

Yarudie tena (maneno hayo) kwa ajili yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Kisha (Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)) akasema:

Na mengine anamnyanyua kwayo mja wake daraja mia, na baina ya kila daraja mbili (umbali wake) sawa na umbali wa mbingu na ardhi.

Akauliza:

Nini hicho ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?

Akasema:

Ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

 

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema pia:

Hakika huko Peponi zipo daraja mia, Mwenyezi Mungu amewatayarishia wapiganao Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na baina ya kila daraja mbili umbali wake sawa na umbali wa mbingu na ardhi. Na mnapomuomba Mwenyezi Mungu, muombeni (Pepo ya) Al Firdaus, kwani hiyo ipo kati kati ya Pepo, sehemu ya juu ya Pepo, na juu yake ipo Arshi ya Al Rahman, na kutoka hapo inapasuka (inaanzia) mito ya Peponi.

 

Thamani ya Jihadi

Kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):

Kipi chenye thamani kupita jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

Hamukiwezi.

Akaulizwa suali hilo mara mbili au tatu na kila anapoulizwa alikuwa akijibu:

Hamukiwezi.

Mara ya tatu akasema:

Mfano wa anayepigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni mfano wa aliyefunga (aliyebaki akiwa amefunga), (na) akaswali nyakati za usiku huku akiomba na kusoma aya za Mwenyezi Mungu bila kuchoka katika Swala yake wala kuacha kufunga mpaka atakaporudi yule aliyekwenda kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Maimamu watano

 

Kufa Shahiyd

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Hajeruhiwi mtu (anapopigana jihadi) katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu anamuelewa kila anayejeruhiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa atakuja siku ya kiyama huku jeraha lake likiwa linamwaga damu, na rangi ni rangi ya damu lakini harufu ni harufu ya miski.

 

Amesema Muhammad bin Ibrahim katika hadithi ndeefu yenye shairi refu ndani yake kuwa:

Kisha nikakutana na al Fudhail bin Iyadh akaniambia:

Wewe ni katika wanaoandika hadithi?

Nikamwambia; Ndiyo.

Akaniambia; Basi iandike hadithi hii (kama) ujira wako kwa kutuletea kitabu cha Abi Abdul Rahman. Kisha Al Fudhail bin Iyadh akaanza kunihadithia yafuatayo:

Amenihadithia Mansur bin Al Muatamir, kutoka kwa Abi Saleh, kutoka kwa Abi Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa mtu mmoja alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam); Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nifundishe jambo nitakalopata ndani yake thawabu ya mpigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Akasema:

Unaweza uwe unaswali (moja kwa moja) bila kuchoka, na ufunge (moja kwa moja) bila kula chakula?

Akasema:

Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi ni dhaifu nisiyeweza kufanya yote hayo.

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia:

Basi naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, lau kama utafanya yote hayo basi (bado) hutouifikia (daraja) ya mpigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Hujaelewa bado kuwa Mpigana jihadi anapokuwa juu ya farasi (akiwa amekaa tu juu yake) huku amezishika hatamu anaandikiwa thawabu?.

 

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kuwaambia Masahaba wake:

Walipofariki ndugu zenu katika vita vya Uhud, Mwenyezi Mungu alizijaalia roho zao ndani ya mwili (mfano) wa ndege wa kijani, wanaiendea mito ya Peponi na wanakula katika matunda yake na wanakaa katika tundu za dhahabu zilizotundikwa katika kivuli cha Arshi. Walipoona ladha nzuri ya vyakula vyao na vinywaji vyao na makazi yao wakasema:

Nani atakayewajulisha ndugu zetu (waliopo duniani) juu yetu kuwa tuko hai Peponi tunaruzukiwa, ili wasije kufanya ulegevu katika jihadi?

Mwenyezi Mungu Akasema:

Mimi nitawajulisha juu yenu.

Ndipo Alipoteremsha kauli Yake:

. 0

Wala kabisa usiwadhanie waliouliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.

Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.

Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.

Aal Imran 169 171

 

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Roho za mashahidi zimo ndani ya miili (mfano wa miili) ya ndege (yenye rangi ya) kijani, wanatembezwa (wanaingia na kutoka) Peponi wanavyotaka.

Na akasema:

Shahidi hahisi maumivu ya kuuliwa isipokuwa mfano wa mmoja wenu anavyohisi maumivu ya kufinywa.

Na akasema:

Jihadi iliyo bora, ajeruhiwe farasi wako na imwagike damu yako.

 

Mashahidi aina saba

Kutoka kwa Jabir bin Atiq kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Mashahidi ni (aina) saba gheri ya aliyeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu:

Aliyekufa kwa maradhi ya tauni ni shahidi, aliyezama (aliyekufa kwa kuzama) shahidi, mwenye maradhi yanayosibu sehemu za mbavu ni shahidi (aliyekufa kwa maradhi hayo), aliyekufa kwa maradhi ya tumbo ni shahidi, aliyekufa kwa kuungua - shahidi, aliyekufa kwa kuangukiwa na nyumba - shahidi, na mwanamke aliyekufa katika uzazi - shahidi.

Ahmed Abu Daud Annasai kwa isnadi iliyo sahihi

 

Na kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Wepi mnaowahesabu kuwa ni mashahidi miongoni mwenu?

Wakasema:

Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliyeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi.

Akasema:

Basi mashahidi katika umati wangu watakuwa wachache.

Wakasema:

Wepi hao basi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?

Akasema:

Atakayeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi, na atakayekufa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi (yaani akiwa katika kumtii Mwenyezi Mungu), na atakayekufa kwa maradhi ya tauni ni shahidi, na atakayekufa kwa maradhi ya tumbo ni shahidi na aliyezama ni shahidi.

Muslim

 

Na kutoka kwa Said bin Zeid kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Atakayeuliwa kwa ajili ya (kuihami) mali yake ni shahidi, na atakayeuliwa kwa ajili ya (kuipigania) dini yake ni shahidi, na atakayeuliwa kwa ajili ya (kuwahami) watu wake ni shahidi.

Ahmed na Attirmidhiy na akaisahihisha.

 

Wanasema wanavyouni kuwa watu wote hawa wanahesabiwa kuwa ni mashahidi juu ya kuwa hawakufa katika vita vya jihadi ya kuipigania dini ya Mwenyezi Mungu na kuwa siku ya Akhera watapata thawabu sawa na waliokufa katika Jihadi, isipokuwa hapa duniani wataoshwa na kusaliwa (kama maiti wa kawaida).

 

Kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu

Anayepigana jihadi ya kweli ni yule ambaye nia yake ni kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuinyanyua bendera ya Haki na kuiondoa batili na kujitolea mhanga nafsi yake kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.

Ama ikiwa nia ya kupigana Jihadi ni nyingine katika mambo ya kidunia tofauti na hayo yaliyotajwa, basi hiyo haiwezi kupewa jina la Jihadi.

Kwa hivyo atakayepigana kwa ajili ya kupata cheo, au kwa ajili ya ngawira, au apate kuonekana ushujaa wake, au kwa ajili ya kujulikana, basi huyo hana chake katika ujira wowote utokao kwa Mwenyezi Mungu na wala hatopata thawabu.

Kutoka kwa Abu Musa (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Alikuja mtu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema (akauliza):

Mtu anapigana kwa ajili ya kujipatia ngawira (mali inayotekwa katika vita), na mwengine apate kusifiwa, na mwengine apate kuonesha ushujaa wake, yupi kati yao (anahesabiwa kuwa) yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu?

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

Atakayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, huyo yupo katika njia ya Mwenyezi Mungu.

 

Imesimuiwa na Abu Daud na Annasai kuwa mtu mmoja alisema:

Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje mtu anayepigana kwa ajili ya kutaka ujira na umaarufu, anapata nini?

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam):

Hapati chochote.

Akauliza suali hilo mara ya tatu ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipomwambia:

Hapati chochote. Hakika Mwenyezi Mungu haikubali amali (matendo) yoyote ikiwa haikuwa halisi kwa ajili ya kutaka radhi Zake.

 

Nia

Nia ni uhai wa amali yoyote ile, na chochote kinachotendwa bila ya nia basi amali hiyo inakuwa amali isiyo na uhai wala uzito wowote mbele ya Mwenyezi Mungu.

Amesimuliwa Bukhari kutoka kwa Abullahi bin Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Hakika amali zote (huhesabiwa kutokana) na nia, na hakika ana kila mja (malipo) ya aliyoyanuwia.

 

Nia ndiyo yenye kunyanyua daraja ya matendo, kwani mtu anaweza kuifikia daraja ya waliokufa shahiydi hata kama hakufa vitani.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Atakayemuomba Mwenyezi Mungu kwa nia ya kweli afe shahidi, Mwenyezi Mungu atamfikisha katika daraja za waliokufa shahidi hata kama atakufa kitandani pake.

 

Na akasema:

Hakika katika mji wa Madina kuna makundi ya watu ambao hamkwenda mwendo (vitani), na hamkuyakata mabonde isipokuwa walikuwa mabondeni (sawa kama nyinyi), yamewazuwia maradhi.

 

Ikiwa nia ya kupigana jihadi si kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, bali kwa ajili ya kutafuta manufaa ya kidunia, basi si kama mtu huyo atakosa thawabu tu, bali atakuwa amejitafutia adhabu siku ya Kiama.

Kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:

Wa mwanzo kuhesabiwa siku ya Kiama ni mtu aliyekufa shahidi katika vita, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa na baada ya kuzijuwa ataulizwa:

Umezifanyia kazi gani neema hizi?

Atasema:

Nimepigana jihadi kwa ajili yako mpaka nikafa shahidi.

Ataambiwa:

Umesema uongo, bali ulipigana ili pasemwe kuwa wewe ni mjasiri na pashasemwa.

Kisha pataamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa motoni.

Na mtu (mwengine) aliyejifundisha elimu akaijuwa (vizuri), akasoma na qurani, (mtu huyo) ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa;

Umezifanyia kazi gani neema hizi?

Atasema:

Nimejifunza elimu nikafundisha na kwa ajili yako nikasoma qurani.

Ataambiwa:

Umesema uongo, bali ulijifunza elimu ili pasemwe kuwa wewe ni aalim. Ukasoma qurani ili pasemwe kuwa wewe ni msomaji mzuri, na pashasemwa.

Kisha pataamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa motoni.

Na mtu (mwengine) Mwenyezi Mungu amempa wasaa, akampa kila aina ya mali, ataletwa na kujulishwa juu ya neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa:

Umezifanyia kazi gani neema hizi?

Atasema:

Sijaacha njia unayopenda mtu atowe katika mali yake ila mimi nimetowa kwa ajili yako.

Ataambiwa:

Umesema uongo, bali umetoa ili pasemwe kuwa wewe ni mkarimu na pashasemwa. Kisha pataamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa motoni.

Fadhila za kulinda mipaka

Katika mipaka baina ya ardhi ya Waislamu na ya makafiri kwa kawaida panakuwa na upenyo, upenyo ambao adui anaweza kuutumia kwa ajili ya kujipenyeza na kuingia ndani ya ardhi ya Waislamu. Kwa hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuzilinda vizuri sehemu hizo ili adui asiwezi kuzitumia na kuwashambulia kwa urahisi.

Uislamu umetilia mkazo sana kuzilinda sehemu hizo na pia umetilia mkazo kuwatayarisha Waislamu ili wawe wapiganaji hodari, na kwa ajili hiyo kazi hii ya kulinda kwa ajili ya kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ikapewa jina la (Al Ribaat), na uchache wake ni muda wa saa moja na ukamilifu wake ni siku arubaini, na fadhila nyingi sana zinapatikana katika kuzilinda sehemu zenye hatari zaidi.

Maulamaa wamekubaliana kuwa fadhila zake ni nyingi kupita fadhila za kuswali msikiti wa Makka.

 

Hadithi zifuatazo zinatujulisha juu ya fadhila za jukumu hili:-

 

Kutoka kwa Salman (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa; alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:

Ribaat ya siku moja na usiku wake ni bora kuliko kufunga mwezi mzima na kuswali usiku wake, na mtu akifa (akiwa katika jukumu hilo), amali zake zitaendelea kuandikwa na riziki yake ataendela kupata na atasalimika na fitna (za kaburi).

Muslim

 

Na akasema:

Kila maiti amali zake zinakatika isipokuwa aliyekufa akiwa analinda mipaka ili adui asiweze kuingia katika nchi ya Kiislamu (Muraabitan), kwa hakika huyu amali zake zinaendelea kuandikwa mpaka siku ya Kiama, na anaepushwa na mitihani ya kaburi.

 

Fadhila za Kurusha 'Al Ram-yi'

Uislamu umetilia mkazo kujifunza kurusha (mkuki, mshale, kupiga risasi, mabomu nk.), na pia kujifunza fani mbali mbali za kupigana kwa nia ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukapendekeza pia kufanya mazoezi ya viungo na ya kutumia silaha kwa nia hiyo hiyo.

Kutoka kwa Uqbah bin Amer (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akiwa juu ya membari akisema:

Basi waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mnazoweza (silaha).[1][1]

Hakika nguvu ya kweli ni kurusha, hakika nguvu ya kweli ni kurusha, hakika nguvu ya kweli ni kurusha.

Muslim

 

Na kutoka kwa Uqba (Radhiya Llahu anhu) pia alisema:

Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:

Mtawezeshwa kuziteka nchi nyingi, mmoja wenu asishindwe kuutumuia mshale wake (asijifunze kuutumia kwa ajili ya mchezo tu bali kwa ajili ya kupigana jihadi). Hakika Mwenyezi Mungu huwaingiza Peponi watu watatu kwa mshale mmoja - aliyeutengeneza (kwa nia ya jihadi), anayempa (anayekaa nyuma yake au pamoja naye na kumpa pale mishale inapomalizika), na mrushaji katika njia ya Mwenyezi Mungu.

 

Uislamu umeshadidia sana katika kuchukizwa na mtu anayejifunza kutumia upinde au silaha yoyote kisha akasahau namna ya kuitumia silaha hiyo bila udhuru unaokubalika kisheria.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Atakayejifunza kutupa, kisha akasahau hayupo pamoja nasi.

Na akasema:

Mchezo wowote anaocheza mtu ni batil (yaani hapati thawabu ndani yake), isipokuwa (mchezo wa) upinde (na mshale), na kumzowesha farasi wake (pamoja na kumfundisha), na kucheza na watu wa nyumba yake (kwa kuzungumza na mkewe na kutaniana naye), hayo ni katika mambo ya haki (anayopata thawabu ndani yake).

 

Anasema Al Qurtubiy:

Maana ya hadithi hii na Mwenyezi Mungu ndiye ajuwae zaidi, ni kuwa; Kila mchezo unaopoteza wakati wa mtu usio na faida, hauna thawabu yoyote ndani yake, na kuachana nao ni bora zaidi, isipokuwa mambo matatu haya, juu ya kuwa ni mchezo, lakini yanampatia mtu thawabu kwa sababu ya faida inayopatikana ndani yake. Kwa sababu katika kutumia upinde na mshale na kumfundisha farasi mbinu mbali mbali za kivita, na mtu kuzungumza na kutaniana na mkewe kunaweza kumfanya awe mcha Mungu wa kweli. Na kwa ajili hii mambo matatu haya yakawa yanaweza kumpatia mtu thawabu.

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alisema:

Enyi wana wa Ismail! rusheni (mishale) kwani baba yenu alikuwa mrushaji.

Na kujifunza kupanda farasi na kutumia silaha ni katika fardhi kifaya inayoweza kuwa fardhi aiyn.

 

Wajibu wa viongozi wajeshi

Yafuatayo ni mambo anayowajibika kuwa nayo kiongozi wa jeshi.

1-     Kushauriana na wenzake na kutaka rai zao, na asiwe akijiamulia bila kuwashauri, na hii inatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema;

Na shauriana nao katika mambo.

Al Imran 159

Na kutoka kwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Sijapata kumuona mtu anayependa kutaka ushauri wa Masahaba wake kupita Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Imam Ahmed na Imam Shafi (Radhiya Llahu anhu).

 

2-     Upole na kuwarahisishia mambo. Anasema Bibi Aisha (Radhiya Llahu anha):

Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akisema:

Yeyote atakayepewa uongozi wa umma wangu basi awe mpole juu yao, awe mpole juu yao.

 

Na imepokelewa kutoka kwa Muaqal bin Yasar kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Hapana amiri yeyote aliyepewa uongozi juu ya Waislamu, kisha asijitahidi juu yao (katika kuwa mpole kwao na katika kuwatafutia manufaa) wala asiwanasihi, (kwa kuwaamrisha mema na kuwakataza mabaya) isipokuwa hatoingia Peponi.

 

Na amesimulia Abu Daud kutoka kwa Jabir (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akirudi nyuma katika misafara kwa ajili ya kuwasaidia walio dhaifu (kwa kuwashika mikono au kushika hatamu za wanyama wao na kuwatanguliza mbele ili wawe pamoja na wenzao), na kuwapakia juu ya ngamia (wake na wa wengine wendao kwa miguu).

 

3-     Kuamrisha mema na kukataza maovu ili watu waepukane na kumuasi Mwenyezi Mungu.

 

4-     Kulikagua jeshi mara kwa mara apate kuwajuwa vizuri askari wake, na kuwajuwa wale wanaowavunja moyo wenzao wasitake kwenda vitani, na wale wanaosababisha choko choko katika jeshi, kwa kusema kwa mfano; hatuna silaha za kutosha wala nguvu za kutosha. Na pia apate kuwajuwa wale wanaotoa siri za jeshi.

5-     Kupashana habari na viongozi.

6-     Kuchaguwa sehemu zinazofaa kwa ajili ya kupiga kambi.

7-     Kutuma wapelelezi kwa ajili ya kujuwa hali za adui.

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa anapotaka kushambulia mahali akiwababaisha adui kwa kuwajulisha kama kwamba anataka kushambulia mahali pengine.

Alikuwa pia akiwatuma wapelelezi wamletee habari za adui, na alikuwa akilipanga vizuri jeshi lake.

 

Amesema Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu):

Bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ilikuwa nyeusi na ya jeshi ilikuwa nyeupe.

Abu Daud

 

Usia kwa viongozi

Kutoka kwa Abu Musa (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alikuwa anapompa uongozi yeyote katika Masahaba wake katika baadhi ya mambo alikuwa akimwambia:

Wapeni watu bishara njema (juu ya rehma ya Mwenyezi Mungu na kusamehe kwake) wala miswape habari za kuwachukiza (kwa kuwatisha na kuwaogopesha), na mambo muyafanye (yawe) mepesi, msiyafanye (yakawa) magumu.

 

Na pia kutoka kwa Abu Musa (Radhiya Llahu anhu) amesema:

Alinituma Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) mimi na Muadh kwenda Yemen akasema:

Wepesisheni mambo wala msifanye yakawa magumu, wapeni watu bishara njema wala miswape habari za kuwachukiza, wahiyarisheni, na msikhitilafiane.

Bukhari na Muslim

 

Kutoka kwa Anas (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Nendeni kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa kufuata mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala msimuuwe mzee mkongwe, wala mtoto mdogo, wala mwanamke (ila kama ni mwanajeshi), wala msiendeane kinyume katika ngawira, na mchange pamoja ngawira zenu, na mtengeneze na mfanye mema kwa sababu Mwenyezi Mungu anawapenda watendao mema.

Abu Daud

 

Usia wa Umar (Radhiya Llahu anhu)

Omar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) alimwandikia Saad bin Abi Waqaas (Radhiya Llahu anhu) na askari wake wengine akiwausia yafuatayo;:

Amma baad - Mimi nakuamrisha wewe pamoja na askari ulio nao kumcha Mwenyezi Mungu katika kila jambo, kwa sababu kumcha Mungu ni silaha bora kupita zote mbele ya adui, na ni mbinu yenye nguvu kupita zote kati vita. Na nakuamrisha wewe pamoja na ulio nao mchunge msije kufanya maasi kuliko mnavyomchunga adui yenu, kwa sababu madhambi ya wanajeshi yana hatari zaidi juu yao kupita adui wao. Kwa hakika Mwenyezi Mungu huwapa ushindi Waislamu kwa sababu maadui ni watu wenye kumuasi Mwenyezi Mungu, ama sivyo sisi hatuna nguvu za kuwashinda, kwa sababu idadi yao ni kubwa kuliko idadi yetu, na silaha zao ni kali kupita silaha zetu. Kwa hivyo tukiwa sawa nao katika kufanya maasi, basi wao watatushinda kwa nguvu zao, kwa sababu tunapewa ushindi kutokana na fadhila zetu na si kwa nguvu zetu.

Na mjuwe kuwa katika msafara wenu mna (Malaika) wenye kuhifadhi wanaojuwa kila mnalotenda, kwa hivyo muwaonee haya, na msiwe wenye kumuasi Mwenyezi Mungu mkiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wala msiseme kuwa; Kwa vile adui wetu wana shari kupita sisi kwa hivyo hawataweza kupewa ushindi juu yetu, kwani huenda watu wakasalatishiwa (wakapelekewa) na kushindwa na adui aliye mbaya kupita wao kama pale Bani Israil walipomuasi Mwenyezi Mungu akawapelekea Majusi (wanaoabudi moto) wakaingia mijini mwao kila upande, ikawa ahadi iliyoyotimizwa.

Muombeni Mwenyezi Mungu akusaidieni katika nafsi zenu kama mnavyomuomba akupeni ushindi juu ya adui yenu, namuomba Mwenyezi Mungu anipe mimi na nyinyi yote hayo.

Na kuweni wapole kwa Waislamu katika mwenendo wao wala msiwakalifishe mambo mazito yatakayowataabisha.

 

Dua wakati wa mapambano

Mpigana jihadi anatakiwa amuombe Mwenyezi Mungu ampe ushindi kwa sababu ushindi umo mikononi mwake Subhanahu wa Taala, na huu ndio uliokuwa mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na mwenendo wa Masahaba baada yake (Radhiya llahu Anhum).

Kutoka kwa Abu Daud kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Mawili hayarudi patupu; Dua baada ya muadhini, na (dua) katika vita pale wapiganaji wanapovamiana.

 

Mwenyezi Mungu Amesema:

(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni.

Al Anfal 9

 

Imepokelewa kutoka kwa (Maimamu) watatu (wa elimu ya hadithi) kutoka kwa Abdullah bin Abi Aufiy kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) katika siku mojawapo alipokuwa akiwasubiri maadui, alisubiri mpaka wakati wa zawal (kidogo baada ya adhuhuri), kisha akasimama kuwahutubia watu akasema:

Enyi watu! Msitamani kukutana na adui, na muombeni Mwenyezi Mungu usalama, na mtakapokutana naye (adui) basi muwe wenye subira (wavumilivu) na jueni kuwa Pepo ipo chini ya vivuli vya panga.

 

Kisha akasema:

Mola wangu uliyekiteremsha kitabu, mwenye kuyasukuma mawingu, uliyewashinda makundi (katika vita vya Ahzabu), washinde na utupe ushindi juu yao.

 

Na katika dua zake wakati wa vita (alikuwa akisema):

Mola wangu wewe ndiye msaidizi wangu na unipaye ushindi, kwako naelekea na nategemea na kwa ajili yako napigana vita.

Imepokelewa na maimamu wa Ahli Ssunnah

 

Kupigana Jihadi

Dini ya kiisalmu inawaita watu katika uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu ili wafaidike na uongofu huo na ili wapate maisha mema ya hapa duniani na ya kesho akhera.

Kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu ameupa umma wa kiislamu jukumu la kuinyanyua dini yake, na kuwafikishia watu wahyi wake kwa ajili ya kuuongoza na kuukomboa ulimwengu.

Na kwa ajili hii ndiyo umma huu ukawa umma bora kupita umma zote zilizodhihirishiwa watu, na ukawa mbele ya watu wengine ukiongoza mfano wa mwalimu na wanafunzi wake, na kwa ajili hiyo lazima uwe na uwezo wa kujihifadhi na wa kujidumisha, na pia uwezo wa kupambana kwa ajili ya kujipatia haki yake na ili uweze kuchukuwa nafasi yake iliyowekewa na Mwenyezi Mungu.

Na kila mwenye kupunguza asitimize wajibu wake katika kujipatia haki yake hiyo, basi anahesabiwa kuwa amefanya makosa makubwa ambayo Mwenyezi Mungu humdhalilisha kwayo au kumfutilia mbali.

Uislamu umekataza ulegevu na kutaka amani (kwa makafiri) ikiwa lengo halijafikiwa, kwa sababu kutaka amani katika wakati kama huu haitokuwa na maana yoyote wala tafsiri nyingine isipokuwa ni uoga na kuridhika kuishi kama watu duni.

Katika haya Mwenyezi Mungu Anasema:

Basi msiregee na kutaka suluhu (piganeni nao maadui zenu) maana nyinyi ndio mtakaoshinda; na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi; wala hatakunyimeni (thawabu za) vitendo vyenu.

Muhammad 35

 

Na maana ya neno mtakaoshinda maana yake ni kuwashinda na kuwa juu yao katika itikadi, ibada, mwenendo na tabia njema, elimu, na matendo.

Amani ya kweli haipatikani bila ya nguvu na uwezo wa kupigana vita, na hii ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akaweka sharti kuwa lazima adui aache kuwapiga vita waislamu na kuwafanyia uadui ili dhulma ipate kutoweka juu ya ardhi na ili mtu asiteswe kwa ajili ya dini yake.

Likiwepo mojawapo katika sababu hizo, basi Mwenyezi Mungu ametoa idhini ya kupigana vita. (yaani ikiwa waislamu wanapigwa vita au wanadhulimiwa au wanafanyiwa uadui au wanateswa kwa ajili ya itikadi yao basi wanaruhusiwa kupigana vita).

Hapana dini yoyote iliyowapa idhini watu wake kuingia katika mapambano na kupigana vita kwa ajili ya kuisimamisha haki na kwa ajili ya kuwasaidia wanaodhulumiwa na kwa ajli ya kuishi maisha ya kuheshimika isipokuwa dini ya kiislamu.

Kwa atakayefuatilia aya mbali mbali za Qurani tukufu pamoja na maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na ya makhalifa wake (Radhiya Llahu anhu) atayaona yote hayo kwa uwazi kabisa, kwani Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala anautaka umma huu kutumia nguvu zake zote katika kuyatimiza hayo.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Na ipiganieni dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki (kupiganiwa).

Al Hajj 78

Kisha Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Akabainisha kuwa jihadi ni Imani ya matendo, ambayo bila ya hiyo dini haikamiliki, Akasema:

.

Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?

Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.

Al Ankabut 2 3

 

Kisha Akabainisha kuwa hii ndiyo njia aliyowaekea waumini, na kwamba hapana njia nyingine itakayowaletea ushindi na kuwaingiza Peponi, Akasema:

Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.

Al Baqarah 214

 

Akawataka Waislamu kujitayarisha vizuri na akawataka pia wawe wenye kutisha mbele ya makafiri, Akasema:

Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.

Al Anfal 60

 

Na namna ya kujitayarisha inategemea wakati na hali ya mambo, na neno nguvu, maana yake ni kutumia kila njia inayowezekana kutumika kwa ajili ya kumuondoa adui.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Hakika nguvu ya kweli ni kurusha, hakika nguvu ya kweli ni kurusha, hakika nguvu ya kweli ni kurusha.

Muslim

 

Na katika kujitayarisha ni kuchukua hadhari na kumuandaa kila mwenye uwezo.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu! Na mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!

An Nisaa 71

 

Na kuchukuwa hadhari hakukamiliki ila kwa kujitayarisha na majeshi yanayoweza kupigana ardhini na baharini na angani.

Mwenyezi Mungu akatuamrisha kupambana na adui tukiwa katika hali yoyote ile, iwe ya dhiki au katika neema, nzuri au mbaya, Akasema:

Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.

At Tawba 41

 

Uislamu unategemea zaidi nguvu ya imani kuliko nguvu ya silaha na kwa ajili hiyo unatilia nguvu zaidi mambo ya kiroho na kuiamsha hima na azma ya mpiganaji.

Mwenyezi Mungu Anasema:

.

Basi nawapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanaouza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako?

An Nisaa 75-76

 

Na Muislamu anatakiwa awe na subira, kwani kama yeye avyoumia basi adui naye pia anaumia, tena yeye anaumia zaidi kupita wao, na hii ni kwa sababu ya hitilafu kubwa ya malengo yao.

Mwenyezi Mungu nasema:

Wala msifanye uvivu kuwafuatia watu (walio maadui). Kama mmepata maumivu basi wao pia wanapata maumivu kama mnavyoumia. Na nyinyi mnatumai kwa Mwenyezi Mungu wasiyoyatumai.

An Nisaa 105

 

Na Akasema:

Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapigana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu.

An Nisaa - 76

 

Na maana yake ni kuwa; lengo la Waislamu ni tukufu, na ujumbe wao wanaotaka kuufikisha kwa watu ambao kwa ajili yake wanapigana jihadi, ambayo ni risala ya haki na ya kheri, nayo ni kulinyanyua juu neno la Mwenyezi Mungu ni tukufu pia.

 

Na Muislamu anatakiwa awe mwenye nyoyo thabiti kwenye mapambano.

Mwenyezi Mungu Aanasema:

15

Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo.

Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.

Al Anfal 15 16

 

Kisha Akawajulisha juu ya mahali ilipo nguvu zao za imani Aliposema:

.

Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa.

Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri

Al Anfal 45-46

 

Kisha Akatujulisha juu ya nafsi ya Muislamu, na kwamba lazima waipigane kwa juhudi zao zote, kwa sababu hawana isipokuwa hiari mbili tu, ama wauwe au wauliwe, Akasema:

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

At Tawba 111

 

Akiuwa atapata ushindi, na akiuliwa atakuwa amekufa shahidi na ataingia Peponi.

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

Sema; Nyini hamtutazamii sisi ila (kupata) moja katika mema mawili (ima kushinda au kuuawa mkapata Pepo).

At Tawba - 52

 

Anayeuliwa katika jihadi kwa ajili ya kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu hafi akatoweka kama wanavyokufa watu wa kawaida, bali wao wananyanyuliwa na kupelekwa mahali pema zaidi na bora zaidi. Kwa hivyo kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu maana yake hasa ni kubaki.

Mwenyezi Mungu Anasema:

. .

Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi.

Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.

Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini."

Al Imran 169 171

 

Mwenyezi Mungu siku zote huwa pamoja na wanaopigana jihadi na wala hawaachi mkono.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole.

Al Anfal - 12

 

Kisha Mwenyezi Mungu anawatayarishia malipo mema hapa duniani na pia malipo mema huko akhera.

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

. . .

Enyi mlio amini! Nikuonyesheni biashara itakayo kuokoeni na adhabu iliyo chungu?

Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.

Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa.

Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!

Asssaf 10 13

 

Kwa njia hii dini ya kiislamu iliwalea waliotangulia na ikaweza kuingiza ndani ya nafsi zao imani iliyowawezesha kupambanua baina ya haki na batili na kuwawezesha kupata ushindi na kuziteka nchi na iliwawezesha kuwamakinisha vizuri juu ya ardhi.

Mwenyezi Mungu Anasema:

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.

Muhammad 7

 

Na Anasema:

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.

Nur 55

 

 

Wajibu wa kuwa thabiti

Muislamu analazimika kuwa thabiti mbele ya adui na ni haramu kwake kurudi nyumba katika mapambano.

Mwenyezi Mungu anasema:

.

Enyi Mlioamini! Mkutanapo vitani na wale waliokufuru basi msiwageuzie migongo (mkakimbia).

Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.

Al Anfal 15-16

 

Aya hizi zinawajibisha kuwa thabiti katika mapambano na zinaharamisha kurudi nyuma isipokuwa katika hali mbili zifuatazo;

Ya kwanza Kwa ajili ya mbinu za kivita kama vile kuondoka mahali penye hatari zaidi na kukimbilia mahali bora, au kuondoka mahali anapoweza kudhurika kwa urahisi na kukimbilia mahali anapoweza kusitirika, au mahali pa chini na kukimbilia penye muinuko atakapoweza kupambana na adui kwa urahisi zaidi.

Ya pili Kurudi kwa nia ya kuungana na wenzake kwa ajili ya kupambana kwa pamoja dhidi ya adui, au kwa ajili ya kuwasaidia wenzake hao, yote sawa ikiwa wenzake hao wako karibu au wako mbali.

Kinyume na hivyo, kurudi nyuma kwa ajili ya kukimbia tu ni mojawapo ya madhambi makubwa sana yatakayompelekea mtu kupata adhabu iumizayo.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Jiepusheni na mambo saba yaangamizayo.

Wakamuuliza:

Ni yepi hayo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?

Akasema:

Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, Uchawi, kuiuwa nafsi iliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia mnapokutana na adui, na kuwasingizia uongo wanawake waliotakasika wasiojua (maovu)."

 

 

Kukimbia vitani

Hata hivyo inaruhusiwa kukimbia vitani ikiwa idadi ya adui inazidi idadi ya Waislamu mara mbili. Ama ikiwa idadi yao ni mara mbili tu (si zaidi) au chini ya hapo, basi ni haramu kukimbia.

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:

Sasa Mwenyezi Mungu amekukhafifishieni, maana anajua ya kwamba kuna udhaifu (sasa) kwenu (kwa kuwa vita vimeendelea kwa muda mrefu). Kwa hivyo wakiwa watu mia moja kwenu wenye subira nawawashinde watu mia mbili kwao; na kama wakiwa elfu moja miongoni mwenu nawawashinde elfu mbili; kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri (yaani sasa wanaambiwa kila Mwislamu mmoja akabiliane na makafiri wawili)."

Al Anfal 66

 

Imeandikwa katika kitabu cha Al Muhadhab kuwa:

Ikizidi idadi ya makafiri juu ya Waislamu kwa mara mbili basi inajuzu kwao kurudi nyuma na kukimbia, lakini wakiona kuwa hawatoangamizwa, basi ni bora kwao kukazana barabara mbele ya makafiri na wasikimbie. Ama wakihisi kuwa watakuja angamizwa, basi hapo watakuwa na hiari mbili.

1- Inajuzu kukimbia - kwa sababu Mwenyezi Mungu Amesema:

Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.

Al Baqarah 195

2- Haijuzu kukimbia kwa sababu baadhi ya maulamaa wanaona kuwa udhaifu uliokusudiwa katika aya ni udhaifu wa nguvu na si wa idadi.

Uungo na Hadaa vitani

Inajuzu kufanya hadaa na kusema uongo vitani kwa ajili ya kumbabaisha adui, sharti visitumike (uongo na hadaa) katika kuvunja mikataba na ahadi.

Mfano wa hadaa ni pale kiongozi anapomhadaa adui akamfanya adhani kuwa ana jeshi kubwa sana na nguvu nyingi.

Katika hadithi iliyotolewa na Bukhari kutoka kwa Jabir (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Vita ni hadaa.

Na imetolewa na Muslim katika hadithi ya Ummu Kulthum binti Uqbah (Radhiya Llahu anhu) kuwa amesema:

Sijapata kumsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akitoa ruhusa ya kusema uongo juu ya jambo lolote lile katika mazungumzo ya watu isipokuwa katika vita au katika kuleta sulhu baina ya watu na (pia) mtu anapozungumza na mkewe na mwanamke anapozungumza na mumewe.

Rehma Vitani

Uislamu umeruhusu vita kama ni jambo la dharura na ukaweka vipimo maalumu juu yake, kwa mfano;

Asiuliwe isipokuwa anayeshiriki katika vita, ama aliyejitenga asipigane vita, huyo haijuzu kuuliwa au hata kudhuriwa kwa jambo lolote.

Imeharamishwa pia kuua wanawake, watoto, wagonjwa, wazee, maulamaa wa dini, wacha Mungu na waloingia katika sulhu.

Imeharamishwa pia kuuharibu mwili wa aliyeuliwa kwa kukatwakatwa, kuuwa wanyama, kufisidi mazao, maji, kuvichafua visima na kubomoa nyumba.

Ni haramu pia kuua majeruhi, na kuendeleza chuki, na hii ni kwa sababu vita ni mfano wa opreshen operation, ambapo anachotakiwa tabibu ni kuyaondoa maradhi tu, na asivuke zaidi ya hapo.

Imehadithiwa na Sulayman bin Buraidah kutoka kwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anapomchagua kiongozi wa jeshi au wa kikosi, alikuwa akimwita pembeni na kumuusia kumcha Mwenyezi Mungu yeye pamoja na maaskari wake, kisha akimwambia:

Piganeni vita kwa jina la Mwenyezi Mungu katika njia ya Mwenyezi Mungu, piganeni na wanaomkufuru Mwenyezi Mungu, piganeni lakini msichupe mipaka, wala msifanye khiyana, wala msiwaharibu maiti kwa kuwakatakata, wala msiuwe watoto.

 

Amehadithia Nafia kutoka kwa Abdullah bin Omar (Radhiya Llahu anhu) kuwa katika baadhi ya vita, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimkuta mwanamke ameuliwa, akakataza kuuliwa kwa wanawake na watoto.

Muslim

 

Amehadithia pia Rawah bin Rabia (Radhiya Llahu anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimuona mwanamke ameuliwa katika mojawapo ya vita alivyoshiriki na huenda akawa ni huyo aliyetajwa katika hadithi iliyotangulia, akasimama mbele ya maiti hiyo kisha akasema:

Hapakuwa na haja ya kumuua mwanamke huyu. Kisha akawa anaziangilia nyuso za Masahaba wake kisha akamwambia mmoja wao:

Kamwahi Khalid bin Walid (umwambie); asiuwe watoto wala mateka wala mwanamke.

 

Na katika usia wa Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alompa Usama (Radhiya Llahu anhu) alipompeleka katika nchi ya Sham alimwambia:

"Msifanye khiyana wala msishambulie bila taarifa (ghadran), wala msikate kate maiti za adui, wala msiuwe mtoto wala mzee wala mwanamke, wala msiunguze mtende wala msikate mti unaotoa mazao wala msichinje mbuzi au n'gome au ngamia ila kwa ajili ya kula. Na mtakutana na watu waliojitenga ndani ya mahekalu yao kwa ajili ya ibada, basi waacheni hivyo hivyo walivyo."

Kisha akasema: "Nendeni kwa jina la Mwenyezi Mungu."

Na usia namna huu alikuwa akitoa Omar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) na wengine miongoni mwa Makhalifa wa Kiislamu.


 [1][1] At Tawba - 60