JINA LA
QURAAN: Zanjabil
MAJINA YA KAWAIDA:
Ginger(Eng), Hinna,Hinnan (Arab), Zanjbil,Janzbil, ……….(Heb),Sonth,Adrak
(Hindi), Tangawizi(kiswahili)
JINA LA KITAALAMU:
Zingiber officinate
JAMII: Zingiberaceae
WAPI KATIKA QURAAN
IMETAJWA:
76:17
Mwenyezi Mungu anasema:
"Na humo
watanyweshwa kinywaji kilichochanganywa na Tangawizi."
(76:16)
Kinywaji cha pombe
ambacho huko peponi watakinywa wale ambao hawajapata kunywa hapa duniani.
Inaelezwa katika aya ya (Sura Dahr) kuwa kinywaji hicho kitachanganywa na
Tangawizi.
Tangawizi hapa inaelezwa kwa kuwa huko
Arabuni zamani tangawizi ilikuwa inahusishwa sana na Wa-Arabu, kwa hivyo ndio
mana imetajwa.
Kitarekh Tangawizi inaelezwa
kuwa ni kipando cha nchi za India, lakini Zanzibar nayo kuna wakati ilikuwa
ikipatikana kwa wingi, na hivi sasa Tangawizi yote itumiwao Zanzibar inatoka
nje ya nchi, sijui wataalamu wakilimo wanaweza kutueleza nini?
Mtangawizi unaota chini
ya ardhi na Tangawizi imekuwa inatumiwa kila mwahali duniani. Inavitu kama
"Zingiberine, cineol, na borneol".
Mafuta ya Tangawizi,
Ginger oleoresin na tangawizi kavu ni biashara kubwa duniani kote.
Tangawizi hutumika
kuhifadhia vitu, hutumika katika vinywaji, biskuti, viungo vya mchuzi, mkate,
beer, na hata shira mbali mbali hutengenezwa na mchanganyo wa tangawizi..
Mwenye kukosa utashi wa
kula (loss of appetite) mchanganyiko wa tangawizi, sharbati ya ndimu na
mchanganyo wa chumvi ya mawe huwa kinywaji kitachoweza kurejesha hamu na nguvu
ya kula.
Inaaminika kwa wale
wagonjwa wa kisukari kinywaji cha tangawizi husaidia kwa mgonjwa lakini
kinywaji hicho kiwe bila ya kuchanganya na sukari.
Kusumbuliwa na kumwa na
ufizi na kichwa (neuralgic headaches) mchanganyiko wa tangawizi kavu na maji
huwa msaada mkubwa.
Ibn Sina ameelezea kwa
mapana faida za tangawizi.
Nchi nyingi duniani
husafirisha tangawizi zikiwemo India, Malaysia, Nigeria. Nchi ya India huingiza
mapato ya wastani kwa kusafirisha Tangawizi katika nchi za Iran, Kuwait,
Morocco, saud Arabia, Yemen, U.A.E, Uiengereza na hata Merekani.
Tangawizi itumiwao kwa
kuhifadhi vyakula huzalishwa kwa wingi na nchi ya Hong Kong, Australia na China
na kusafirishwa kwa wingi kwa nchi za Magaribi.
HADITHI
Anaeleza Abu Said Al Khudri
kuwa;
“Mtawala wa Rumi (Rome)
alituma kikapu cha Tangawizi kama ni zawadi kwa Bwana Mtume Muhammad SAW, na
Bwana Mtume alimpa kipande kila mmoja katika Masahaba nami nikapata
changu."
Abu Nu’im