Sheikh Ahmad Yaasin (1938- 2004)
Allah (s.w.t.) anasema katika Qur’ani Yake Tukufu:
“Enyi Mlioamini! Jisaidieni (katika mambo yenu) kwa
subira na Salah; bila ya shaka Allah yu pamoja na
wanaosubiri. Wala msiwaite wale waliouawa katika 
njia
ya Allah wafu, bali wahai, lakini nyinyi hamtambui. Na
tutakutieni katika msukosuko wa baadhi ya mambo haya;
hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa
matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri. Ambao
uwapatapo msiba husema: ‘Hakika sisi ni wa Allah 
na
kwake Yeye tutarejea (atatupa jaza yake)’. Hao juu yao
zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema; na
ndio wenye kuongoka”. (2: 153 – 157)
Sheikh Ahmad Yaasin ni mujahid wa Ummah huu na hasa
katika maeneo ya Palestina. Aliishi maisha yake 
yote
kwa kujitolea mhanga na kuwa ndani ya Jihadi mpaka
Allah (s.w.t.) alipomruzuku Shahada.
Sheikh Ahmad Isma‘il Yaasin alizaliwa katika kijiji
cha al-Joura ambacho kipo katika wilaya ya Majdal
karibu na bandari ya Asqalan (Ashkelon), kaskazini mwa
Ukanda wa Gaza mwaka wa 1938. Japokuwa ipo riwaya ya
kwamba alizaliwa mwaka wa 1936. Alifariki babake na
umri wake haufiki miaka mitano (5) na katika mwaka wa
1948 ilibidi ahame kutoka katika kijiji chake baada ya
kushindwa vibaya jeshi la Kiarabu na Wazeyuni. Vijiji
karibu 531 viliharibiwa kabisa kwa njia moja au
nyengine zikiwemo vijiji 122 ambazo watu wake
walitolewa kwa nguvu na jeshi la Kiyahudi, 270 kwa
mashambulizi ya kiaskari ya Mayahudi ya moja kwa moja,
38 ni watu wa vijiji kuingiwa hofu ya kuwa askari
wanaweza kuwashambulia, vijiji 48 ni kwa ile taathira
ya kwamba mji mkuu umetekwa, vijiji sita walitoka watu
wake kwa 
hiyari na vijiji 46 kwa njia nyenginezo.
Kijiji kilichoathirika ni kile alichokuwa akikaa
Sheikh na familia yake. Hivyo ilibidi ahame yeye na
familia yake Gaza katika kijiji kilichokuwa kinaitwa
Journal ash-Shams na kuishi hapo maisha ya kawaida
kabisa.
Katika mwaka 1952 alipata ajali alipokuwa akicheza na
marafiki zake na hivyo kupooza mwili mzima ila sehemu
ya kichwa na kumfanya yeye awe ni mwenye kutumia
kigari. Athari hiyo ilimfanya awe haoni vyema. Lakini
upungufu wote huu haukumfanya asiweze kutekeleza
wajibu wake wa kimasomo na Da‘wah, bali alikuwa
msitari wa mbele katika haya yote. Aliendelea na
masomo 
yake na mwaka wa 1958 alitunukiwa shahada baada
ya kumaliza masomo ya Thanawiyah (masomo ya
sekondari). Baadae alielekea al-Azhar ambapo alimaliza
masomo yake na kupata shahada ya awali (degree ya
kwanza) katika masomo ya Kiislamu. Alipokuwa Misri
alijiunga na Harakati ya Ikhwanul Muslimiina. 
Hapo
alikuja kuelewa na kufahamu kuwa Palestina si ya
Wapalestina wala Waarabu peke yao bali ni ya Waislamu
wa ulimwengu mzima. Hivyo haifai kwa kiongozi, sheikh,
mufti au mtu yeyote kumpatia mwengine ardhi hiyo wala
kufanya mikataba ili kuitoa katika milki ya 
Waislamu.
Alirudi Gaza na hapo akaanza kazi ya ualimu ambapo
alikuwa alifundisha Lugha ya Kiarabu na Tarbiyah ya
Kiislamu. Kisha alianza kutoa darsa na khutbah na kuwa
mhubiri mkubwa katika Misikiti ya Ukanda wa Gaza.
Alipata umashuhuri kwa sababu ya maneno yake 
ya
ushupavu, matendo yake mema na nguvu katika kuleta
hoja mzito na kufikia katika uimara na msimamo na
kuwapatia changamoto Wazeyuni walioiteka Gaza kimabavu
baada ya Vita vya Siku sita za 1967.
Katika miaka ya 1970, alichaguliwa kuwa mwenyekiti 
wa
Taasisi ya Kiislamu Gaza na Chama cha Kiislamu cha
Sadaka. Aliendelea kuzitumikia taasisi hizi mpaka
alipotiwa mbaroni mwaka 1983 na kufungwa na serikali
haramu ya Kizeyuni. Na katika mwaka wa 1979,
alianzisha Harakati ya Kiislamu iliyokuwa ikiitwa 
Majd
al-Mujahideen (Utukufu wa Mujahidina). Alikamatwa
mwaka wa 1983 na kutuhumiwa kuwa alipatikana na
silaha, kuanzisha harakati ya kivita na kuhamasisha
Waislamu kuwatoa Waisraili katika ardhi ya Palestina
na kuing’oa  Dola haramu ya Kizeyuni. 
Sheikh
alipelekwa kotini mwaka 1984 na kuhukumiwa kifungo cha
miaka 13 lakini aliachiliwa tarehe 20 Mei 1985. Hayo
yalikuwa baada ya muafaka baina ya Popular Front for
the Liberation of Palestine (Harakati Maarufu katika
Kuikomboa Palestina – PFLP) na wakuu wa Kizeyuni 
kwa
kubadilishana mateka wa pande hizo mbili. Alikaa
gerezani kwa muda wa miezi kumi na moja.
Tarehe 8 Desemba 1987 yalitokea mabadiliko ambayo
yaliwapatia fursa ndugu zetu kuweza kunyanyua vichwa
vyao na kuona kuwa Wazeyuni mbali na silaha zao si
lolote si chochote. Siku hiyo Mzeyuni mmoja akiendesha
lori aliivurumiza katika halaiki ya vibaruwa wa
Kipalestina na kuwaua 4 na kuwajeruhi 9. Tarehe 9
Desemba 1987, watu elfu tatu walio na hasira walikuwa
walishiriki katika mazishi ya mashahidi. Jeshi la
Israili lilikuja na kuuzunguka umati huo na kujaribu
kuwaondosha. Mawe yalirushwa kwa maaskari hao ambao
walianza kupiga 
risasi na kuwaua 2 na kuwajeruhi
wengine 30. Habari hizi za mapambano haya zilienea
kote katika Ukanda wa Gaza (Gaza Strip) na Ukingo wa
Magharibi wa Mto Jordan (West Bank) na hapo Intifadha
ikaanza.
Tarehe 14 Desemba 1987, pazia ilifunguka na 
Harakatul
Muqaawamatul Islamiyyah (Harakati ya Upinzani ya
Kiislamu) ilianzishwa. Kwa ufupi inaitwa Hamas (au
Hamasa). Harakati hii ilianzishwa na Sheikh mwenyewe
pamoja na wanaharakati wenziwe katika Ukanda wa Gaza.
Sheikh alikuwa na kilema lakini alikuwa ana uoni 
na
kipawa cha kuiongoza harakati hiyo bila ya matatizo.
Alisaidiwa katika uongozi na Dkt. Abdul-‘Aziz Ranteesi
(alitaka kuuliwa mwaka jana 2003), Mahmoud az-Zahhaar,
Isma‘il Haneyya, Shaheed Isma‘il Abu Shnab (ambaye
aliuliwa na Wazeyuni mwaka jana – 2003) 
na
‘Abdul-Fattah Dukhan. Baada ya kuuliwa Sh. Isma‘il Abu
Shnab Sh. Muhammad Nizzal alichaguliwa kushika mahali
pake. Na katika West Bank, viongozi walikuwa ni
Shaheed Jamal Salim (ambaye aliuliwa tarehe 30 Julai
2001), Hasan Yusuf na Jamal an-Natasha (ambaye 
yuko
gerezani). Na baada ya kuuliwa kwa Sh. Jamal Salim,
Dkt. Muhammad al-Ghazaal alichukua mahali pake.
Viongozi wa Hamas ambao wapo nje ya Palestina ni
Khalid Mish‘al (aliyetaka kuuliwa Jordan 1997 na
Mossad kwa kupigwa sindano ya sumu), Dkt. Musa 
Abu
Marzouq na Ibrahim Ghoushah.
Baada ya Intifadha Sheikh ndiye aliyekuwa alama ya
istiqama na kielelezo katika zama zake kwa kuwa na
subira ya hali ya juu na jihadi. Polisi wa Kizeyuni
waliingia nyumbani kwake mwishoni mwa Agosti 1988 na
kuipekuwa pamoja na kupora vitu na wakamtishia kuwa
watamsukuma na kigari chake kwenye mipaka ya Lebanon.
Naye raisi wa sehemu za kusini Jemadari Ishaqu
Mordekhai alikwenda kumuona Sheikh tarehe 11 Januari
1989 na kumuonya kwamba asitumie Misikiti katika
kuhamasisha watu dhidi ya ukoloni wa Kizeyuni. Hiyo
ilikuwa fursa mzuri kwa Sheikh kwani yeye alimuambia
awaachilie huru wafungwa wote na asitishe kuchukua
kodi na ushuru kutoka kwa watu wa Palestina (West Bank
na Gaza).
Baada ya kuuliwa kwa wasaliti wa Kipalestina ambao
walikuwa wanashirikiana na Wazeyuni katika kuwamaliza
wana-harakati, serikali haramu ya Kizeyuni 
ilimshika
Sheikh usiku wa tarehe 18 Mei 1989 katika kampeni ya
kinyama ambao iliwanasa pia mamia ya wanaharakati wa
Hamas. Aliteswa sana gerezani, hivyo afya yake
kuzorota sana. Dawa zilikatazwa kumfikia na
aliadhibishwa bila ya huruma mpaka akawa 
anazirai
katika siku zake za awali. Kwa unyama wao askari wa
Israili walikuwa wanamtia vyuma katika sehemu zake za
siri na kuzima sigara kwenye uso wa Sheikh.
Mahakama ya Kizeyuni ilipitisha hukumu isiyo ya
uadilifu kwa Sheikh mnamo tarehe 16 Novemba 
1991.
Hukumu iliyotolewa dhidi yake ni kifungo cha maisha na
miaka 15 ziada ya hiyo. Kwa wenye akili ya kutafakari
na kuzingatia sijui mutaitafsiri vipi hukumu hiyo!
Hukumu hii ilikuja baada ya miaka miwili ya msimamo wa
hali ya juu na kuakhirishwa kwa kesi. Sheikh 
huyo
Mujahid alimkatalia wakili wake kupatana na serikali
jambo ambalo lingeweza kumhafifishia hukumu na
akasema: “Sema: ‘Halitatusibu ila alilotuandikia
Allah. Yeye ni Mola wetu’. Basi Waumini nawamtegemee
Allah tu”. (9: 51) Sheikh Ahmad Yaasin alipokea 
hukumu
hii ya kibeberu kwa moyo wa Muumini mwenye subira na
bashasha yenye uyakini kuwa yeye anapigania jambo la
haki na kuwa ushindi utakuja karibu au baadae. Kesi
yenyewe ilifanywa katika hali na mazingira ya ulinzi
mkali ambao haujawahi 
kuonekana.
Sheikh Mujahid Ahmad Yaasin alituhumiwa kwa makosa 15.
Miongoni mwayo ni:
1.        Kuanzisha harakati ya Hamas na msingi wa kitengo
chake cha usalama (MAJD) na taasisi ya kivita
(Mujahidina).
2.        Kutoa amri kuwaua na kuwamaliza watu sita kwa
sababu ya kushirikiana na viongozi wa Kizeyuni.
3.        Kutoa amri ya kumalizwa mtu yeyote mwenye kufanya
uhalifu au kuwa na maadili mabaya.
4.        Amri yake aliyoitoa kwa Mujahidina wa Kipalestina
kurusha mabomu kwa magari ya kivita ya Kizeyuni.
5.        Amri yake kwa Mujahidina wa Kipalestina kuchoma
mashamba ya Wazeyuni.
6.        Kushambuliwa kwa Myahudi aliyekuwa akichimba 
kisima
kusini mwa Gaza na mashambulizi kwa gari la Muisraili
ambaye alikuwa anapita katika maeneo hayo.
7.        Kushikwa kwa aina 18 za silaha kutoka kwa
wanaharakati wa chama cha Mujahidina wa Kipalestina
zikiwemo 
bunduki, bunduki ambazo ni automatic mfano wa
M-16, Carl Gostav na Klashinkov.
8.        Kuwa alihusika katika kutekwa nyara na kuuliwa kwa
askari wawili wa Kiisraili –Afi Sportas na Elan Saadon
mnamo Mei 1989. Mwili wa Saadon ulipatikana Ukanda wa
Gaza na ule mwengine haujulikani ulipo.
9.        Kubadilisha kwa njia ya haramu dola laki sita
(600,000) kwa ajili ya wana-harakati wa Hamas.
10.      Kuhusika katika jaribio la kuwatorosha wafungwa
katika majela ya Kizeyuni.
Mbali na kuwa Sheikh Ahmad alikuwa amepooza mwili
mzima pia alikuwa na matatizo na maradhi tofauti na
mengi. Miongoni mwayo ni upofu katika jicho lake la
kuume kwa sababu ya ngumi alizokuwa akipigwa na
maaskari wa Kizeyuni wakati wa kuhojiwa na udhaifu wa
jicho la kushoto. Pia alikwa na uvimbe na uwekundu wa
muda mrefu katika masikio yake, magonjwa ya mapafu na
maumivu ya tumbo. Kutiwa kwake korokoroni kulichangia
kuzorotesha siha yake ambayo ililazimu kupelekwa
hospitalini mara kadhaa.
Sheikh Ahmad aliachiliwa tarehe 1 
Oktoba 1997 (baada
ya miaka 8) baada ya mapatano baina ya Jordan na dola
ya Israili. Hiyo ni kwa kuwa wapelelezi wawili wa
Kizeyuni walishikwa Jordan baada ya kutofanikisha
shughuli yao ya kumuua Khalid Mish‘al, raisi mkuu wa
maktaba (ofisi) ya siasa ya Hamas. Hapo 
Sheikh
aliachiliwa na kurudi katika kilele cha harakati zake.
Baada ya kuachiliwa alijikuta katika dhiki kubwa kwa
kuanzishiwa kifungo cha nyumbani na uongozi wa
Palestina chini ya Yaasir Arafat.
Sheikh Ahmad Yaasin alinusurika kwa kupata majeraha
madogo kwenye mkono wake wa kuume na jaribio la
Wazeyuni kutaka kumuua mnamo tarehe 6 Septemba 2003
pale ndege yao ya kivita iliporusha makombora kwenye
nyumba aliyokuwa amekwenda Sheikh pamoja na Sh.
Isma‘il Haneyya kumtembelea mwanaharakati mwenziwao.
Alitoka hapo na azimio kubwa zaidi katika kupinga
ubeberu wa Kizeyuni na kujiimarisha katika jihadi.
Jaribio la pili la 
kulenga maisha yake lilifaulu mnamo
tarehe 22 Machi 2004 baada ya Salah ya Alfajiri kwa
kurushiwa swawaarikh tatu (missiles/ makombora) kutoka
kwenye helikopta ya kivita ya Kizeyuni. Makombora na
helikopta zilizotumia zimetengenezwa Marekani. Pamoja
na Sheikh walikufa wengine wanane, watatu 
miongoni
mwao wakiwa ni walinzi (bodyguards) wake pamoja na
watoto wake wawili (‘Abdul-Ghani na ‘Abdul-Hameed)
ambao wamepatikana na majeraha na wapo hospitalini.
Tunawaombea kwa Allah awapatie nafuu katika hali yao
hiyo. Shambulizi hilo lilifuatiliwa kwa makini na 
kwa
ukaribu na Waziri Mkuu wa Israili, Ariel Sharon. Tukio
hili lilikuja baada ya kuwa helikpta hiyo ilikuwa
ikizunguka katika maeneo hayo kwa muda wa masaa
matatu. Mtoto wa Sheikh alimwambia babake kuhusu hilo
lakini akasema sisi ndio tutakalo kufa mashahidi. 
Hii
ilikuwa ni kama ile hali aliyokuwa nayo Sayyidna ‘Umar
(r.a.) alipomuomba Mola wake: “Ewe Mola wangu! Hakika
nimekuwa mzee na nguvu zangu zimedhoofika, hivyo
niruzuku shahada katika njia Yako na unijaalie nife
katika mji wa Mtume Wako”. ‘Umar alipata 
kama
alivyotamani. Na huyu hapa Sheikh Ahmad Yaasin
ameruzukiwa shahada katika uzee na udhaifu wa mwili na
nguvu na akiwa katika ardhi tukufu iliyobarikiwa na
Allah.

 

Alikutana na Allah akiwa katika ulinzi Wake. Amesema
Mtume (s.a.w.): “Yeyote atakae Sali Salah ya 
asubuhi
basi yupo katika ulinzi na uangalizi wa Allah”.
(Imepokewa na Muslim kutoka kwa Jundub bin Sufyaan
[r.a.]). Na katika riwaya nyengine: “Atakae Sali Salah
ya Alfajiri kwa jamaa yupo katika ulinzi wa Allah”. Na
anaingia katika Hadithi ya Mtume (s.a.w.) 
kuwa:
“Yeyote anayemuomba Allah, Aliyetukuka shahada kwa
ukweli, Allah Atamweka katika cheo (daraja) ya
Shuhadaa japokuwa atakufa kitandani mwake”. (Imepokewa
na Muslim, Abu Dawud, at-Tirmidhi na an-Nasai kutoka
kwa Sahl bin Hunayf [r.a.]). Na katika fadhila 
ya
mauti yake ni kupata shahada siku ya Jumatatu, kwani
Mtume (s.a.w.) amesema: “Amali hupelekwa (kwa Allah)
siku ya Jumatatu na Alhamisi”. (Imepokewa na
at-Tirmidhi lakini katika sanadi yake yupo Muhammad
bin Rafa‘ah bin Tha‘labah ambaye hakuaminiwa ila 
na
Ibn Hibbaan hivyo kuifanya Hadithi kuwa dhaifu. Hata
hivyo kuna Hadithi nyingi zenye maana sawa katika Abu
Dawud na An-Nasai ambazo zimeipatia nguvu).
Sheikh aliishi maisha yake yote katika jihadi, naye
akapata shahada kama alivyokuwa akitamani 
kwani
alikuwa akisema: “Jihadi ndiyo njia yetu na mauti
katika njia ya Allah ndiyo matamanio yetu makuu”. Hawa
ndio wale watu waliofuata mfano wa Anas bin an-Nadhr
(r.a.) alipomuahidi Allah na Mtume Wake baada ya Vita
vya Badr kuwa vikitokea vita vingine basi 
atafanya
yale atakayo yafanya. Katika Vita vya Uhud alipata
shahada na mwili wake mzima ulikuwa na majeraha hata
hakuweza kujulikana isipokuwa na dadake aliyemtambua
kwa sababu ya alama aliyokuwa nayo katika kidole.
Allah (s.w.t.) aliteremsha aya inayomhusu yeye 
na
mfano wake: “Wapo watu miongoni mwa Walioamini
waliotimiza ahadi waliyoahidiana na Allah. Baadhi yao
wamekwisha maliza umri wao (wamekwisha kufa) na baadhi
yao wanangoja (siku yao kufika), wala hawakubadilisha
ahadi yao hata kidogo”. (33: 
23)
Walikuwa Mayahudi wakimuogopa Sheikh Ahmad Yaasin
kuliko wanavyohofia viongozi na watemi Waislamu na wa
Kiarabu wote kwa ujumla. Japokuwa alikuwa katika
kigari chake na sauti yake hafifu lakini anatingisha
majemadari wa Kizeyuni na wanasiasa wao. 
Allah
(s.w.t.) anasema: “Hakika nyinyi Waislamu mnaogopwa
zaidi katika nyoyo zao kuliko wanavyomuogopa Mwenyezi
Mungu, maana wao ni watu wasiofahamu lolote”. (59: 13)
MAZINGATIO/ MAFUNDISHO:
1.        Sheikh Ahmad Yaasin 
alitengeneza pamoja na kupooza
kwake harakati, na unyonge wa watu matumaini na
udhaifu wake wa mwili nguvu na utukufu. Hivyo
matumaini ya kiroho yakashinda ule udhaifu wa mwili
wake uliotulia na hawakuweza Mayahudi walio waoga
kuyavunja matumaini hayo, hapo ndipo walipo 
ukatakata
mwili wake dhaifu.
2.        Tuyajaalie mauti ya Sheikh uhai kwa ummah huu wa
Kiislamu wote ili upate kuelekea kwa yale malengo
aliyo pata nayo shahada kwayo. Malengo hayo matukufu
yalikuwa ni kuikomboa Baytil Maqdis na Msikiti 
wa Aqsa
kutokana na uchafu wa Mayahudi na Wazeyuni.
3.        Sheikh aliyaweka wazi malengo yake, nayo ni
kuipinga na kuupiga vita ukoloni kwa kila njia na
nguvu inayowezekana na kutotekeleza matendo hayo nje
ya Palestina. Pia 
alikataza kabisa utumiaji wa silaha
kuwadhuru Wapalestina, na hivyo akasema: “Damu ya
Wapalestina ni haramu, haramu, haramu”. Hayo pia ndiyo
yaliyokuwa maagizo ya Shaheed Sheikh ‘Izz-ud-Deen
‘Abdul-Qaadir Mustafa al-Qassaam alipowausia
mujahidina wake mnamo tarehe 20 Novemba 
1935:
“Musiwaue watoto wetu kwani wao ni masikini hawajui
wanafanya nini. Elekezeni silaha zenu kwa Waengereza
tu”. Waengereza walikuwa wamewaeka Waarabu msitari wa
mbele katika vita hivyo.
Bwana huyu aliyepooza alikuwa akiitetemesha dola ya
Israili na kuwatia hofu majemadari wa kijeshi na
wanasiasa wao naye amekaa kwenye kiti chake hawezi
kukiacha isipokuwa kwa msaidizi. Uume wa mtu haupimwi
kwa nguvu za mwili wake bali kwa nguvu ya Imani yake
na fadhila zake. Allah (s.w.t.) anasema yafuatayo
kuhusu wanafiki: “Na unapowaona, miili yao
inakupendeza”. (63: 4) Na Waarabu wamesema katika
methali zao: “Utamuona kijana 
kama mtende, na ni nini
kitakachokujulisha kilichomo ndani?” Kwa hakika kufa
shahidi kwa Sh. Ahmad Yaasin ni darsa ya Tarbiyyah
yenye nguvu inayobainisha kuwa nguvu za kihakika ni
katika maazimio, matarajio na mipango. Na kwamba
kilema aliyepooza aliifanya dola ya Kizeyuni 
isimame
katika mapambano na kuingia naye katika vita kwa
matukio ya kujitweza ambayo yanakwenda sambamba na
najisi ya Wazeyuni. Huyu mgonjwa ambaye hawezi
kujisaidia njiani ameweza kuwazundua watu wake wote
kwa ujumla na kutoa lengo la kweli katika mapambano 
na
kuwajaalia watoto wa Palestina kuingia katika jihadi
katika njia yake iliyo sahihi.
Ulimwengu mzima ulishuhudia jinsi gain dola mzima
ilivyoshuka na silaha zake za kiaskari kumuua Sh.
Ahmad Yaasin katika hali yake ya uzee, maradhi na
kupooza. Na wahalifu hawa wakaweza kutekeleza uhalifu
wao katika mtaa unaokaa raia na katika sehemu tukufu
ya Msikiti. Hii pia ni kutuonyesha ya kwamba Mayahudi
hawana kabisa kielelezo chema katika maadili na
kuamiliana na watu.
Lau kama Sheikh alikuwa anaimba usalama na amani na
analinda maisha yake angeweza kujiepusha na Salah
katika Msikiti na 
hasa Salah ya Alfajiri na
akabadilisha nyumba moja kwa nyengine. Lakini yeye
alijipinda na kujiekea ulazima wa kusali kwa jamaa,
hivyo kifo chake kilikuja baada ya kutekeleza faradhi
na kumridhisha Mola wake na kukutana Naye akiwa na
udhu, amesali, amerukuu na kusujudu, ameridhika 
na
kuridhiwa. Amesema Allah (s.w.t.): “Na wale waliouawa
katika njia ya Allah, hatazipuuza vitendo vyao.
Atawaongoa na kustawisha hali yao. Na atawaingiza
katika Pepo aliyowajulisha”.  (47: 4 – 6) Nasi
tunatamani na kumuomba Mola wetu atukhitimishe 
kama
alivyomhitimishia Sheikh Ahmad Yaasin.
4.        Mufahamu kuwa mauti ya Sheikh Ahmad Yaasin
hayatodhoofisha upinzani na Intifadha na wala cheche
zake hazitozimika kama anavyoota Sharon na kikundi
chake katika Dola 
haramu ya Israili. Bali wataona kwa
macho yao kuwa moto utazidi kuwaka na sheikh ameacha
nyuma yake watu na kuwa kila pote litaathirika na
Sheikh Ahmad Yaasin. Kila kikundi kitajiweka tayari
katika kuelekeza nguvu na silaha zao kwa Israili kwa
mfano Brigedi wa Qassaam, Brigedi wa Mashahidi 
wa
Aqsa, Kikundi cha Shaheed Abu ‘Ala Mustafa na watu
wote wa Palestina. Hakika damu ya Sheikh Ahmad Yaasin
haitapotea bure bali itakuwa moto na laana kwa Israili
na wendani wake. Allah (s.w.t.) anasema: “Na karibuni
(hivi) wafanyao dhuluma watajua ni mgeuko wa 
namna
gani watakaogeuka (watakaopinduka)”. (26: 227)
Israili imejaribu kuwaua viongozi na wanaharakati
ndani na nje ya Palestina mifano ni Shaheed Sahar
Tammam (16 Aprili 1993), watu 30 waliouliwa ndani ya
Msikiti Ibrahimiyyah wakiwa ndani ya Salah ya 
Alfajiri
(25 Februari 1994), Shaheed Yahya Zakarneh (6 Aprili
1994), Shaheed Ayman Radhi (25 Novemba 1994), Shaheed
Anwar Muhammad na Shaheed Salah ‘Abdul-Hamid (22
Januari 1995), Shaheed Dkt. Fathi Shiqaqi, katibu wa
Jihadi Islami, Malta (26 Oktoba 1995), Shaheed 
Yahya
‘Ayyash (5 Januari 1996), Mashaheed Ibrahim Abu Arab
na Majdi Abu Wardeh (25 Februari 1996), jaribio la
kumuua Khalid Mish‘al huko Jordan (25 Septemba 1997),
Shaheed Sheikh Salah Shehada na familia yake ya watu
15 (22 Julai 2002), Shaheed Sheikh Jamal Salim 
(30
Julai 2001), Shaheed Sheikh Isma‘il Abu Shnab (2003),
Sh. Dkt. Taariq Abu Hassin (Oktoba 2003) na Shaheed
Sheikh Ahmad Yaasin na wengine 8 (22 Machi 2004).
Wengine ni ‘Imad ‘Aql, Ahmad ‘Ateeq, Maahir, Dhiyaa
Muhammad, Mahmoud Abu Hamoudah, Muhammad 
Farhat,
Shadii at-Toubaasi, ‘Abdul-Baasit ‘Awdah na wengineo.
Kuanzia Intifadhah ya Msikiti wa aqsa tarehe 29
Septemba 2000 mpaka sasa takriban ndugu zetu elfu nne
(4,000) wamekufa mashahidi mdogo kabisa akiwa wa miezi
miwili lakini upinzani haujasangaa wala kupungua 
na
wala upepo wa jihadi haujatulia bali mapambano
yamezidi kwa makali na kupamba moto.
Na vipi haitakuwa hivyo baada ya Qur’ani kutufahamisha
kuwa hapigani mtu kwa ajili ya mtu hata mtu mwenyewe
akiwa ni Mtume (s.a.w.), bali anapigana kwa ajili ya
misingi na risala (ujumbe). Kwa hakika ndugu zetu
Palestina ni watu wenye kuzaana kwa wingi, hivyo
anapoondoka shujaa, huzaliwa mwengine. Na sio mmoja
pekee bali kadhaa ambao wanaendelea kubeba bendera
nayo Insha’allah haianguki milele. Na amesema kweli
mshairi wa Kiarabu:
Anapokufa mtukufu miongoni mwetu, anasimama mwengine,
 
Hii ni ishara mzuri kama walivyosema watukufu, hivyo
fanyeni.
 
 
5.        Hii ni kutuyakinishia kuwa Israili haitaki amani
katika eneo la Mashariki ya Kati bali wanataka vita
pekee. Lakini haya yasitustaajabishe kwani Qur’ani
imetuelezea sifa 
zao kubwa – mauaji. Ikiwa walifanya
vitimbi na kuunda njama ya kuwaua na kutaka kuwaua
Mitume (a.s.) na watu wema waliopita na katika zama
zetu hizi, seuze sisi wa kawaida? Waliwaua Manabii
Zakariyya na mwanawe Yahya (a.s.) na wakataka kumuua
‘Isa (a.s.) na Mtume Muhammad (s.a.w.), hivyo sisi 
na
watu wengine watakuwa takataka mbele yao. Allah
(s.w.t.) anatuelezea hayo pale aliposema: “Na haya ni
kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Allah, na
wakiwaua Manabii pasipo haki. Basi haya ni kwa sababu
ya kuasi kwao na kupindukia mipaka ya Allah”. (2: 
61)
Na tena: “Sema: ‘Walikufikieni Mitume kabla yangu kwa
hoja zilizo wazi na kwa haya mnayosema. Basi mbona
mliwaua, kama mlikuwa wakweli?” (3: 183) Na Allah
(s.w.t.) anasema tena: “Hakika utawakuta walio maadui
zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislamu ni 
Mayahudi
na wale mushirikina”. (5: 82) Tuelewe kuwa viongozi
kadhaa wa kizeyuni wamesema wazi kwamba: “The only
good Arab is the one who is dead – Muarabu wa pekee
aliye mzuri ni yule aliyekufa”.
Lakini wakati huu Israili imetupa mipaka na kuwa na
kiburi katika ardhi pasi na haki. Wanafanya uhalifu
mkubwa kama kwamba wanakunywa maji usiku na mchana na
wanaeneza ufisadi katika ardhi. Allah ametuelezea
ufisadi huu pale aliposema: “Na tukawafunulia Bani
Israili katika (hicho) Kitabu kuwa: ‘Bila shaka nyinyi
mtafanya uharibifu katika nchi mara mbili, na kwa
yakini mtatakabari kutakabari kukubwa”. (17: 4)
Wao 
wanaangamiza mimea na roho, wanamwaga damu, na
kuua wasio na hatia na watukufu na viongozi katika
jamii, watoto na wanawake na wazee, wanaharibu
majumba, wanakata miti na kuwang’oa wanati kwa moto na
mkono wa chuma. Allah (s.w.t.) anasema: “Na
wanapoondoka, wanakwenda huku na huku katika 
ardhi
kufanya uharibifu humo na kuangamiza mimea na roho. Na
Allah hapendi uharibifu”. (2: 205) Na yote haya
wanafanya mchana kweupe na ulimwengu mzima unaona.
Uhalifu wao umefika kilele kwa kumuua mtu aliyepooza,
aliye jitahirisha na kusali kwa mpango wa kutoka 
kwa
Sharon na kwa usimamizi wake. Na huo ni ugaidi wa dola
ulio dhahiri na wazi kabisa. Na hili ni onyo ya kuanza
kwa kumalizika kwa Taaghut (shetani wa kibinadamu au
mtu anaye abudiwa asiyekuwa Allah), kwani wakati wao
umefika. Ushetani unapoengezeka kwa kasi na 
udhalimu
ukazidi: Watu wake huwa wanajipeleka katika maangamivu
nao hawajui. Allah (s.w.t.) anasema: “Basi walipopuza
yale waliyokuwa wakikumbushwa Tuliwafungulia milango
ya kila kitu (walichokuwa wakikitaka). Mpaka
walipofurahia yale waliyopewa, hapo Tuliwakamata 
kwa
ghafla; na mara wakawa wenye kukata tamaa. Ikakatwa
mizizi ya watu waliodhulumu (wakaondoka ulimwenguni).
Na sifa zote njema ni za Allah Muumba wa walimwengu
(wote)”. (6: 44 – 45)
 

 

6.        Bila shaka Marekani ni mshiriki katika dauru ya
uhalifu huu na uhalifu 
mwengineo kabla ya huu. Israili
inatekeleza mauaji kwa kutumia silaha na mali ya
Marekani na usaidizi wao. Nao hawakubali Israili itiwe
adabu au kulaumiwa kwani veto (kura ya turufu) ya
Marekani ipo malindizo, tayari kutolewa bila ya
kusita. Anasema Allamah Dkt. Yusuf 
‘Abdallah
al-Qaradhawi: “Lau kama ningekuwa Qadhi (hakimu)
kuhukumu kesi hii ya mauaji ya Shaheed Sh. Ahmad
Yaasin basi angekuwa mtuhumiwa wa kwanza kwangu ni
Raisi Bush. Yeye ni mchochezi wa kwanza kwa uhalifu
huu, naye ndiye aliyempatia mhalifu silaha. 
Pia
anamuona kuwa mhalifu yule anayepigana kutetea haki na
nafsi yake. Yeye ndiye aliyetoa fatwa kwa Sharon na
sahibu zake kuwa upinzani kinzi wa Wapalestina ni
ugaidi na walio msitari wa mbele ni Hamas na Jihadi
Islami. Na maana ya kuwa ni vyama vya ugaidi ni 
kwamba
wanaharakati wake wanastahiki kuuliwa na hivyo hakuna
adhabu kwa mwenye kuwaua magaidi. Na hivyo ndivyo
alivyosema naibu wa Waziri wa Ulinzi na Vita wa
Israili kuwa: ‘Sheikh Ahmad Yaasin anastahiki
kuuliwa”.
Hii ndiyo mantiki ya Marekani na Israili au mantiki ya
Bush na Sharon kuwa Ahmad Yaasin ni gaidi mhalifu
anayestahiki kuuliwa. Sababu ni kuwa anatetea ardhi na
heshima yake, nyumba na nchi yake na shamba lake na
miti ya zaituni pamoja na utukufu wa sehemu zake
katika Palestina.
7.        Hakuna matumaini kwa yale wanayoyaita “Muelekeo wa
Amani” na “Mazungumzo ya Amani” kwani kila mwenye
kuyatizama matukio bila mapendeleo na kwa moyo msafi
anayakinisha kuwa Israili haitaki amani ya kihakika na
amani kamili ya uadilifu. Amani ya uadilifu
haipatikani ila kurudishwa haki kwa watu wake na kila
mmoja asimame katika 
mipaka yake. Lakini Israili
haijui lugha nyengine isipokuwa ya nguvu na haifahamu
ila lugha ya chuma na hawazungumzi isipokuwa kwa ulimi
wa moto. Kwa hakika wao wanawachezea Wapalestina na
viongozi wa Kiarabu kwa ahadi na amani za uwongo na
inakuwa ni kama mangati (mazigazi) ambayo 
kwamba
mwenye kiu huyadhani ni maji, akiyaendea hayaoni
chochote.
Hakika tumejua kwa kufuatilia na majaribio kuwa
chochote kilichochukuliwa kwa nguvu hakirudishwi
isipokuwa kwa nguvu. Hivyo chaguo pekee la Wapalestina
ni kuendelea na upinzani na badili ya upinzani ni
kujisalimisha kwa unyenyenkevu kwa Israili. Na badali
ya upinzani ni mauti.
8.        Ni juu ya Waislamu wote kuamka na hasa Wapalestina,
kwani adui yao anawavamia na kuwapiga wote bila
kubagua. Na haijulikani pigo jengine litaelekezwa
wapi? Inawezekana kuwa mwenye kuchinjwa katika wakati
ujao ni Yaasir Arafat au mwengine katika viongozi.
Hivyo inatakiwa kila mmoja ashike mkono wa mwenziwe
katika ushirikiano. Na hivyo ndivyo inavyotakiwa
katika ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu wanatakiwa
washikamane katika umoja na undugu huo. Inatakiwa
msimamo wao uwe ni 
kauli ya Allah, Aliyetukuka
inayosema: “Kwa yakini Allah anawapenda wale
wanaopigana katika njia ya Yake, safusafu, (mkono
mmoja); kama kwamba wao ni jengo lililokamatana bara
bara”. (61: 4)
Ni juu ya Ummah wa Kiislamu waamke katika usingizi wao
wa muda mrefu na kuwasaidia ndugu zao huko Palestina.
Na katika mshororo huo ni Waarabu walio Waislamu ambao
inaonekana kuwa wamejitoa katika mapambano hayo na
kuwafanya Waislamu wengine wajitoe. Mapambano kwa sasa
yanaonekana kuwa ni baina ya Wapalestina – Waisraili
kama hili si tatizo la Waislamu. Ama Waarabu
wamejificha, Allah anasema: “Naapa kwa umri wako!
Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu);
wanahangaika ovyo”.  (15: 72) Waarabu walipigania huko
Palestina mwaka 1948 ambapo muungano wa nchi za
Kiarabu wakati huo una wanamemba saba na imepita miaka
mitatu kuanzia uanzishwe. Lakini ulipokaribia umri wao
miaka sitini na idadi yao kuongezeka hadi kufika zaidi
ya dola ishirini iliiacha dauru yao. Kwa ajili hiyo
wakaachwa Wapalestina peke yao wakiwa katika upinzani
na kupigana vita na vifua vyao na mikono yao dhidi ya
jeshi ambalo lina silaha kali zaidi katika eneo la
Mashariki ya 
Kati. Na wapinzani wao wakiwa wanasaidiwa
na dola yenye uwezo mkubwa wa kisilaha na hela.
Pia ni wajibu kwa Ummah wa Kiislamu kuiokoa ardhi ya
Israa na Me‘eraj na mji wa al-Quds na Msikiti Mtukufu
wa Aqsa, ambao umebarikiwa pembezoni mwake. Hakika
Aqsa si milki ya Wapalestina peke yao 
hata
wakalifishwe kuitetea na kuipigania peke yao. Msikiti
wa Aqsa ulitekwa hapo kale na watu wa msalaba
(Wakristo kutoka Bara Ulaya) na ukabakia mateka kwa
miaka takriban tisini (90). Wale ambao walifanya
juhudi ya kuukomboa walikuwa ni makabila, koo na 
rangi
tofauti miongoni mwa Waislamu. Harakati iliyo anzishwa
na ‘Imad-ud-Deen Zinki, Mturuki na mtoto wake
Nuur-ud-Deen Mahmoud na mwanafunzi wake Salah-ud-Deen
Hasan al-Ayyubi Mkurdi na Dhaahir Baybras Mamluki na
Sh. ‘Izz-id-Deen al-Qassaam Msuri na wengineo. 
Na
hakika Waislamu wamefaradhishwa kuwadhamini na
kuwasaidia wenziwao ili kuwasaidia katika kuikomboa
ardhi ya Kiislamu na sehemu tukufu za Kiislamu na
kuitetea heshima ya Kiislamu.
Na kwa hakika shaheed Sh. Ahmad Yaasin ni muonyaji
kwetu kwa ujumla na kwao (Wapalestina na Waarabu)
washikamane kama alivyosema Allah (s.w.t.): “Na
shikamaneni kwa kamba (dini) ya Allah nyote, wala
msifarikiane (msiachane)”. (3: 103) Hivyo ni juu ya
Waislamu wote kusimama na ndugu zao katika ardhi ya
Manabii (a.s.) kwa aina ya usaidizi – wa pesa, kususia
bidhaa za adui na kwa dua ili waweze kuendelea na
jihadi na 
upinzani kinzi dhidi ya adui.
9.        Sheikh alisimama na msimamo imara juu ya Qur’ani na
Sunnah, jihadi na subira mpaka akakutana na Mola wake
akiwa shahidi. Je, misimamo yetu ni hali gani? Je,
sisi tumeingia katika kutekeleza ahadi? Mfano mdogo ni
kuwa sisi tunamuahidi Allah (s.w.t.) mara kumi na saba
kila siku: “Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na Wewe tu
ndiye tunayekuomba msaada”. (1: 5) Je, sisi
tunamuabudu Allah kihakika? Au sisi ni wale watu
tunapopata shida na matatizo tunaelekea katika vitu
ambavyo haviwezi kutudhuru wala kutusaidia. Ikiwa 
ni
hivyo basi misimamo yetu haijakuwa sawa kabisa kwani
ushirikina unaharibu amali zote na unamtoa mtu katika
Uislamu. Inatakiwa sisi tusimame na nasaha
aliyotupatia Mtume (s.a.w.). Nayo ni: Imepokewa kwa
Abu ‘Abbas ‘Abdallah bin ‘Abbas (r.a.) kwamba: 
“Siku
moja nilikuwa nyuma ya Mtume (s.a.w.) akaniambia: ‘Ewe
kijana! Mimi nitakufundisha maneno, mjali Allah naye
atakuhifadhi. Mjali Allah utampata Yuko nawe.
Ukimuomba muombe Allah; ukitaka msaada taka msaada kwa
Allah. Na ujuwe kwamba hakika lau watu 
wote
wakusanyike ili wakunufaishe wewe kwa jambo lolote,
hawawezi kukunufaisha ila kwa jambo alilokuandikia
Allah na wakikusanyika ili kukudhuru kwa jambo lolote,
hawawezi kukudhuru ila kwa jambo alilokuandikia Allah.
Kalamu zimeshainuliwa, na kurasa zimeshakauka”. 
(Ahmad
na at-Tirmidhi) Katika Hadithi nyengine iliyopokewa na
Abu ‘Amr Sufyaan bin ‘Abdallah (r.a.) kwamba:
“Nilisema: ‘Ewe Mtume wa Allah, niambie mimi neno
katika Uislamu ambalo sitamuuliza yeyote isipokuwa
wewe’. Akasema: ‘Tamka: Nimemuamini Allah, kisha 
wende
mwendo wa sawa (kuwa imara)”. (Muslim) Sisi leo tupo
wapi na misimamo ya dini katika ardhi hii. Tuchukuwe
fursa ya kujiuliza: Je, tunasali kama inavyotakikana
Salah za Faradhi na Sunnah? Je, tunafunga Ramadhan na
kuongezea funga za Sunnah? Je, sisi ni wakweli 
na
waaminifu kwa Allah na binaadamu? Je, ninashirikiana
na Waislamu wenzangu katika ulinganiaji? Je,
nimeutumikia vipi Uislamu? Na mengi mengineyo.
10.      Sheikh aliruzukiwa shahada baada ya kusali Salah
ya Alfajiri Msikitini. Ilikuwa shauku yake 
kubwa ni
kutekeleza wajibu huo wa kusali Salah kwa jamaa na
hali yeye ni mzee mgonjwa aliyepooza mwili mzima na
mwenye kutafutwa kuuliwa na maadui wakati wa giza
totoro la Alfajiri. Hivyo ndivyo alivyoaga maisha ya
dunia hii baada ya kutekeleza Faradhi hiyo. Hii 
ni
dalili tosha katika nafsi za vijana na maana yenye
kutoa nuru pembezoni mwake. Tukio hili linatuonyesha
na kutufahamisha kwamba wale wenye kujibu mwito wa
jihadi ndio hao hao wanaojibu njooni katika Salah
KAULI ZAKE ZA HEKIMA:
Mwili wa Sheikh wetu mpendwa umeondoka hapa duniani
lakini bado kwetu yu hai kwa kauli zake, misingi na
misimamo yake ambayo ilikuwa ikisimama katika Qur’ani
na Sunnah. Miongoni mwa kauli zake ni:
1.        Hakika roho zipo Mikononi mwa Allah na riziki 
ya
kila mmoja imeandikwa na Allah, hiyo hofu na kukimbiya
ni kwa nini?
2.        Imefika wakati kwa Ummah huu kuleta pamoja nguvu
zake za mali na nyenginezo katika kuinusu Palestina
iliyotekwa. Sababu ni kuwa Palestina ni Qiblah 
cha
kwanza cha waislamu na moyo kwao unaodunda. Ikiwa
Waislamu hawatafanya hivyo basi wangojee hukumu ya
historia ambayo haimrehemu mtu yeyote.
3.        Kumuamini kwako Allah na Uislamu ina maana kuwa ni
lazima utake na 
kuitafuta “shahada” na wala usiogope
kufa.
4.        Intifadha itaendelea na matatizo ya Wapalestina
nayo yataendelea pamoja na fursa ya nguvu katika
upinzani kinzi. Allah pekee ndiye anayejua jihadi hii
na upinzani huu 
utaendelea kwa muda gani.
5.        Palsetina ni ardhi tukufu kwa Waislamu, Manasara na
Mayahudi, na wote wanatakiwa waishi pamoja humo kwa
amani. Na kwa kuwa Waislamu ndio wengi ni haki yao
kuunda serikali ya Kiislamu. Manasara na Mayahudi
wataishi humo kwa kupatiwa ulinzi na kutendewa haki
kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani.
6.        Kuhusu mahusiano baina ya uongozi wa Fatah na
Hamas, alisema: “Hivi ni vyama viwili tofauti lakini
adui ni mmoja. Kwa ajili hiyo wanatufanya tuwe na
umoja unaotakiwa”. Adhabu na matatizo yaliyowakumba
Wapalsetina hayana mfano katika historia ya wakati
huu. Mimi siogopi kifungo gerezani kwa sababu ardhi ya
Palestina na wakfu ya Kiislamu na kizazi chochote
hakina haki kuiuza sehemu yake au ardhi yote. Hii
ndiyo itikadi yetu na 
itikadi haigawanyiki.
7.        Adui anamuona kila mmoja wetu ni gaidi na lau
wataweza watamuua kila mmoja Palestina, kwani wao
wanataka ardhi bila watu. Haituhusu sisi mgawanyo wa
aina yeyote. Katika historia ya Kiislamu, makafiri
walikuwa wakisema kuwa Mtume (s.a.w.) ni muongo na
mchawi. Je, sifa hizi zote zilikuwa za kweli? Lakini
yeye alisubiri na kubeba haya yote na akafanya juhudi
na mwishoni Uislamu ulishinda. Na sisi tunabeba
bendera ya haki, nasi ni watu wakweli kabisa katika
ulimwengu na amani 
kwetu ni muhimu. Sisi hatupigani na
Mayahudi kwa kuwa wao ni Mayahudi au kwa kuwa wao
wanaishi Palestina. Huko Misri wanaishi Mayahudi na
Manasara pamoja na Waislamu na wala hawapigwi, lakini
lau ndugu yangu atachukua nyumba yangu nitapigana naye
kwa ajili ya haki yangu ambayo ameichukua 
kutoka
kwangu.
Ni juu yetu kumuombea kwa Allah amrehemu na aikubali
jihadi, subira na kujitolea kwake mhanga na amweke
pamoja na Manabii, wakweli, mashahidi na watu wema. Na
mwisho ni kuseme:
Ee Mola sisi tumekuja kwako kumuombea Shifaa basi
mpatie shufaa. Ee Mola mghufirie na umrehemu. Na
ukaribishwe kushuka 
kwake na yapanue maingilio yake.
Na muoshe kwa maji, theluji na ubaridi (barafu). Na
yasafishe makosa yake kama inavyosafirishwa nguo
nyeupe kutokana na uchafu. Na mbadilishie nyumba bora
kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake. Na
mke bora kuliko mke wake. Na mwepushe na adhabu 
ya
kaburi na adhabu ya moto. Ee Mola mbadilishie makosa
yawe ni thawabu. Na akiwa ni muovu basi yasamehe maovu
yake. Ee mola usituharamishie ujira wake wala
usitufitini baada yake na utusamehe sisi na yeye na
waislamu wote.
 
Inna lillahi wa inna ilayhi raaji ‘uun. Allahumma
ajirna fii musiibatuna… wakhlujlana khayran 
minha.
 
“Bila shaka tunatoka kwa Allah na kwake tutarudi. Ee
mola tupe ujira katika huu msiba na utupe badali iliyo
bora zaidi”.
 

 Makala haya yameandaliwa na ndugu yangu mpenzi, Muhammad El Maawy