ADHABU YA KABURINI

ITIKADI ZISIZO SAHIHIMTOTO WA ZINA

BID'AH HADAA ZA IBILISI

EWE BINADAMU

Usimuogope mwenye nguvu madamu nguvu Zangu ni zenye

kubakia. Na nguvu Zangu haziishi abadan.

EWE BINADAMU

Usiogope kwa kuwa wewe ni mwenye rizki ya shida na

ilhali hazina zangu zimejaa. Na hazina zangu haziishi

abadan.

EWE BINADAMU

Usimuombe mwengine na ilhali Mimi ni kwa ajili yako.

Utakaponitaka utanikuta. Na unaponiacha nitakuacha, na

kw hivyo kheri yote itakupita.

 

EWE BINADAMU

Nimekuumba kwa ajili ya ibada basi usicheze. Na

nimekugawia rizki yako basi usijihangaishe. Lau kama

utaridhika kwa kile nilichokugawia basi utaupumzisha moyo

wako na mwili wako, na utakuwa Kwangu ni mwenye

kushukuriwa. Na kama hutaridhika na nilichokugawia

basi Naapa kwa utukufu wangu; Nitakuendeshea mbio duniani

uende mbio kama wanyama mwitu wanapokimbilia wanyama, kisha hutapata ila kile nilichokugawia tu, na

utakuwa kwangu ni mwenye kudharauliwa.

EWE BINADAMU

Nimeumba mbingu saba na ardhi saba wala sikupata

tabu katika kuziumba, basi kitanichosha kipande cha

mkate ninachokusogezea bila ya taabu.

EWE BINADAMU

Hakika sikumsahau mwenye kuniasi, basi vipi

(nimsahau) mwenye kunitii? Na ilhali Mimi ni Mola

Mwingi wa rehema na Mweza wa kila kitu.

EWE BINADAMU

Usiniombe riziki ya kesho kama ilivyo Mimi

sikukukalifisha amali ya kesho.

EWE BINADAMU

Mimi kwako wewe ni mpenda basi kwa haki yangu juu

yako uwe mpenzi kwangu . (Yaani ninakupenda kwa

kuwa nimekuumba na kukupa neema zisizo na hesabu kwa

kutaraji wewe ushukuru neema hii na utekeleze

ninayokuamrisha ili upendeze kwangu na kukupa ridha

yangu).