Assalaam alaykum

Namuomba Mola Jalali awazidishie imani na subra katika kazi hii njema ya kuwazindua na kuwaongoza ndugu zetu Waislam.  AAMEEN

Nimelisoma shairi la Ndugu yetu All Hajj Udii (Sauti Ya Nasaha) lenye anuwani “NGUO FUPI (SWALI) nikavutiwa sana haswa kuhusu ndugu zetu waliyoathirika na mavazi yasiokua na maana. Nami hivi leo nimewatumia shairi lifuatalo la kumuunga mkono All Hajj Udii ili  kuonya na kubainisha ubaya wa nguo fupi. Nawaomba mukipata nafasi mulitie katika mtandao.

Swaleh Suheil Abeid

         

                            Gonga hapa ulisome shairi  TUKAE KIMYA KWANINI?

 

+++++++++++++++++++++++++++++++++

 

 

 

Subject :      maombi

         

 

 

 

Assalam Aleikum

                         Mimi ni mmoja wa wageni wa safu hii nipo Marekani ila natamani mungeweka ya kusikiliza mawaidha//

 

Mohamed Ali

+++++++++++++++++++++++++++++++++

 

Subject :      Uislamu na ugaidi

 

Asalaam aleikum.

Kwanza sina budi kuwapongeza kwa juhudi zenu kubwa za kuweza kufikiria na kufanikiwa kufungua website hii ambayo ndani yake,waislam na wasiowaislam waweza kujifunza kuhusu uislam na mafundisho ndani ya waislam.Leo hii waislamu tumekuwa katika wakati mgumu ambao inabidi tuwe makili ili kuweza kulitukuza jina la mola wetu na mitume.Watu wengi wasio waislamu wanapenda sana kujua nini hasa uislamu na ndani ya uislamu kuna nini.Wanapenda kujua kuhusu mola, quran,mtume muhammad(saw) na uislamu kwa ujumla.Wengine huanza kutaka kujua kwa kuuliza maswali magumu,sababu wengi wao ni wasomi.Watu hawa wanapokutana na muislamu ambaye haujui vizuri uislamu na hakutaka kusema kweli kuwa haujui vizuri uislamu,hupata majibu mepesi na yenye mapengo kuhusu uislamu.Lakini,wanapokutana na muislamu mwenye kuujua vizuri uislamu basi hupata majibu ambayo mara nyingi huwabadilisha na kuwa zaidi upande wa uislamu.Mfano kamili ni sasa wakati ambao ugaidi umekuwa ni tamko la kila siku katika vyombo vya habari.Hapa mtu humuuliza muislamu,kwa nini uislamu unaamrisha ugaidi?,mtu huyu ukimuuliza kwa nini ameuliza swali hili,atasema"kila kunapotokea ugaidi,magaidi huwa na ni waislamu".Ukimuuliza kwa nini unasema ni magaidi ni waislamu,atakujibu"angalia hapa majina yote ya magaidi ni ya kiislamu''.Ukiangalia ni kweli majina yote ya magaidi ni ya kiislamu,lakini je uislamu unaamrisha ugaidi?.Ndugu waislamu naomba kama kuna yeyote atakayependa kuendeleza mada hii,ili tuweze kuwaelimisha watu wengi ambao si waislamu na baadhi ya waislamu ambao wakibanwa kidogo hukubali kuwa uislamu unaamrisha ugaidi.Inshaallah mada hii itaendelea-----

Asalaam aleikum

Juma

 

+++++++++++++++++++++++++++++++++

Tuesday, July 19, 2005 

Assalamu Alaykum,

Nawapa shukurani kwa jitihada zenu. Ama kwa hakika nimesoma makala kadha na nikaona ni yenye faida sana. Mola Karimu awape moyo huo huo wa kuwaelimisha na kwanasihi na kuwazindua Ndugu zetu Waislamu  walioghurika na anasa za duniya wafuate njia ilo mustaqeem. Inshaallah kazi yenu hii ya kujitolea haitakua ni ya bure bali hamutokosa fadhila na jaza yake Subhana Huu Wataala Duniani na Akhera. Mwenyezi Mungu awape kila la kheri na baraka. AAMEEN.Hivi leo ninawatumia shairi fupi ambalo linatukumbasha mauti. Tafadhalini lichapishine :-

Swaleh Suheil Abeid

Gonga hapa uweze kulisoma shairi

+++++++++++++++++++++++++++++++++