Hijjah Na ‘Umrah

 

Imekusanywa Na Kufasiriwa Na

Muhammad Faraj Salem Al saiy

 

Yaliomo

 

Utangulizi

Ni Katika Amali Bora

Wajumbe Wa Mwenyezi Mungu

Inawajibika Hapo Hapo

Kuhiji Kwa mali Ya Kukopa

Hijjah Ya Mwenye Deni

Kuhiji Kwa Mali Ya Haramu

 

‘Umrah

Miyqaat (Mipaka)

Vizuri Kuswali Kabla Ya Kutia Niyyah

Hukmu Ya Talbiyyah

   Fadhila Zake

   Kunyanyua Sauti Katika Talbiyyah

Twawaafu ya ‘Umrah

Maqaam Ibraahiym

Kunywa Maji Ya Zamzam

Sa’ay Baina Ya Swafaaa Na Marwahh

Kujihalalisha

   Fadhila Za Kunyoa Nywele Zote

 

Hijjah

‘Arafah

   Hukmu yake

   Kusimama ‘Ar

Utangulizi

Ni Katika Amali Bora

Wajumbe Wa Mwenyezi Mungu

Inawajibika Hapo Hapo

Kuhiji Kwa mali Ya Kukopa

Hijjah Ya Mwenye Deni

Kuhiji Kwa Mali Ya Haramu

 

‘Umrah

Miyqaat (Mipaka)

Vizuri Kuswali Kabla Ya Kutia Niyyah

Hukmu Ya Talbiyyah

   Fadhila Zake

   Kunyanyua Sauti Katika Talbiyyah

Twawaafu ya ‘Umrah

Maqaam Ibraahiym

Kunywa Maji Ya Zamzam

Sa’ay Baina Ya Swafaaa Na Marwahh

Kujihalalisha

   Fadhila Za Kunyoa Nywele Zote

 

Hijjah

‘Arafah

   Hukmu yake

   Kusimama ‘Arafah

Muzdalifah

Minaaa

Twawaaful Ifaadhwah

   Hukmu yake

Nyakati za kupiga mawe

Kuomba Du’aa

Siku Ya Kuharakisha

Twawaaful Wida’a

afah

Muzdalifah

Minaaa

Twawaaful Ifaadhwah

   Hukmu yake

Nyakati za kupiga mawe

Kuomba Du’aa

Siku Ya Kuharakisha

Twawaaful Wida’a

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Utangulizi

 

Shukrani zote ni zake Mwenyezi Mungu, tunashuhudia kuwa hapana anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni Mtume wake.

 

Ameufikisha ujumbe na kuifikisha amana, kwa hivyo tunakuomba Mola wetu umsalie na kumsalimu Mtume wako huyu mtukufu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) na Aali yake na Masahaba wake watukufu - Aamin.

 

Amma baad,

 

Mwenyezi Mungu Anasema:

 

{{Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hijjah katika Nyumba hiyo; yule awezaye kufunga safari kwenda huko. Na atakayekanusha (asende na hali anaweza) basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kuwahitajia walimwengu.}} [Aali ‘Imraan–97]

 

Maulamaa wote wamekubaliana kuwa Hijjah ni moja katika nguzo tano za Kiislamu, na ni fardhi ijulikanayo kuwa ni ya lazima. Atakayekanusha kuwajibika kwake huwa ni kafiri aliyertadi na kutoka katika dini ya Kiislamu.

 

Wanavyuoni wengi wanasema kuwa: Hijjah imefaradhishwa katika mwaka wa sita baada ya Hijra, (baada Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuhamia Madiynah).

 

Mwanachuoni maarufu Ibnil Qayyim, katika kitabu chake kiitwacho Zaadul Ma-ad, yeye amesema kuwa Hijjah imefaridhishwa mwaka wa tisa, pale ilipoteremshwa aya isemayo:

 

{{Na timizeni Hijjah na Umra kwa ajili ya MwenyeziMungu.}} [Al Baqarah – 196]

Rudi ju

 

Ni Katika Amali Bora

 

Amesimulia Abu Hurayrah (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliulizwa:

 

"Amali ipi iliyo bora?"

Akajibu:

"Imani juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake"

Akaulizwa: “Kisha ipi?”

Akasema:

"Kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".

"Kisha ipi?"

Akasema:

"Kisha Hijjah iliyokubaliwa".

 

Anasema As-Sayid Saabiq, mwandishi wa kitabu ‘Fiq-hus Sunnah’:

 

"Hijjah iliyokubaliwa ni ile isiyochanganyika na maovu.”

 

Al-Hassan Al-Basry yeye amesema:

 

"Hijjah iliyokubaliwa ni ile iliyomfanya aliyehiji anaporudi akawa anaipenda akhera yake kuliko dunia.”

Rudi ju

 

Wajumbe Wa Mwenyezi Mungu

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((Mahujaji na wenye kufanya ‘Umrah ni wageni wa Mwenyezi Mungu.Wanachomuomba anawapa, na wakiomba maghfira anawaghufiria.))

[Imepokewa na An-Nasai, Ibni Majah, Ibni Khuzaymah na Ibni Hibban]

 

Kwa hivyo kila aliyebahatika atambue kuwa tokea siku ile alipoamua kwenda kuhiji, keshakuwa mgeni wa Mola wake Subhanahu wa Taala, na kwa ajili hiyo anatakiwa awe mtu anayekistahiki cheo hicho. Na anapokuwa katika Ibada hiyo tukufu asigombane wala kuzozana na Mahujaji wenzake.

 

Zimepokelewa Hadiyth nyingi zinazotufahamisha kuwa atakayehiji bila kufanya maovu wala kugombana wala kuzozana, hapana zawadi nyingine anayoistahiki isipokuwa Pepo.

Rudi ju

 

Inawajibika Hapo Hapo

 

Maimamu wakubwa kama vile Abu Hanifa na Maalik na Ahmad bin Hanbal na baadhi ya wanafunzi wa Imam Ash-Shaafi’iy wanasema:

 

"Hijjah inamwajibikia kila mtu toke pale anapokuwa na uwezo. Kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((Anayetaka kuhiji basi aharakishe, kwa sababu huenda akaumwa, mnyama wake akazeeka au akapatwa na shida (akazitumia pesa zake).))

 

Na katika hadithi nyengine amesema:

 

((Fanyeni haraka mkahiji, maana hajui mmoja wenu atapatwa na nini.)) [Imepokewa na Ahmad, Al-Bayhaqiy, At-Twahaawiy na Ibn Maajah]

Rudi ju

 

Kuhiji Kwa mali Ya Kukopa

 

Kutoka kwa Abdullah bin Abu Auf (Radhiya Llaahu ‘anhu) amesema:

((Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) juu ya mtu asiyewahi kuhiji iwapo anaruhusiwa kukopa kwa ajili ya kuhiji?” Akaniambia; “La, (asifanye hivyo)”.)) [Imepokewa na Al-Bayhaqiy]

Rudi ju

 

Hijjah Ya Mwenye Deni

 

Kamati ya kudumu ya Utafiti wa Kielimu na Utoaji Fatwa imetoa fatwa kuhusiana na suala la Hijjah ya mwenye deni kwa kueleza yafuatayo:

Moja ya masharti ya Hijjah ni uwezo, na mtu kuwa na uwezo wa mali wa kuifanya Hijjah. Ikiwa mtu ana deni ambalo anadaiwa na mkopeshaji na mkopeshaji akawa hakubali yule mtu aende Hijjah bila kumlipa pesa zake, basi hatoruhusika kwenda Hijjah hadi alipe deni analodaiwa, kwani mtu huyo atahesabika si mwenye uwezo wa kwenda Hijjah. Lakini endapo mkopeshaji hatomshikilia alipe pesa zake na ima kamruhusu aende Hijjah hali ya kuwa ana deni lake, basi anaweza kwenda na Hijjah yake kwa hali hiyo itakubalika.

[Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah 11/46]

 

Na katika Fatwa nyingine, Kamati ya Kudumu ya Fatwa walipoulizwa swali kuhusu Hijjah ya mwenye deni la nyumba ambalo muulizaji alisema anapaswa kulilipa kwa awamu, ilieleza ifuatavyo:

Uwezo wa kutekeleza Hijjah ni moja ya masharti ya kuwa kwake ni waajib. Ikiwa una uwezo wa kulilipa deni hilo kwa awamu ambayo imekutana na wakati wa Hijjah, basi unaweza kwenda baada ya kulilipa deni katika awamu hiyo. Lakini ikiwa huwezi kulipa deni hilo kwa awamu hiyo, basi ahirisha Hijjah hadi utakapopata uwezo kwani Allaah Anasema:

“Na kwa ajili ya Allaah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia (mwenye uwezo) ya kwendea.” [Aal ‘Imraan 3: 97]

Na at-Tawfiyq ni kutoka kwa Allaah

[Al-Lajnah ad-Daaimah lil Buhuuth al-‘Ilmiyyah wal Iftaa 11/45]

 

Naye Mwanachuoni Shaykh Muhammad bin Swaalih al-‘Uthaymiyn anasema:

Deni linalodaiwa linapaswa kutangulizwa kulipa kuliko Hijjah, kwani wajibu wa kulilipa unawekwa mbele kuliko mtu kwenda kutekeleza Hijjah. Hivyo, anapaswa mtu kulipa kwanza deni kisha ndio kwenda Hijjah. Na ikiwa hatobakiwa na chochote au kitakachobaki hakimtoshelezi gharama za kwenda Hijjah, basi atasubiri hadi Allaah Amjaalie uwezo wa kwend akuitekeleza nguzo hiyo. Lakini likiwa ni deni lenye kuwa na muda mrefu aliopewa mkopeshwa la kulilipa siku za mbele, hivyo, kwa hali hii hata kama mkopeshaji akimruhusu au asimruhusu kwenda Hijjah, hatoruhusika kwenda Hijjah ikiwa hana uhakika au dhamana ya kulilipa kwa ule muda aliopewa/waliokubaliana na mkopeshaji.

Kwa hali hiyo tunasema: Ikiwa mtu anadaiwa deni, na anafahamu kuwa ana uwezo wa kulilipa kwa muda aliopewa (hata ikiwa ni mbeleni baada ya Hijjah), basi Hijjah kwa hali hiyo inakuwa ni wajibu kwake japokuwa ana deni.

[Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn, 21/96]

Rudi ju

 

Kuhiji Kwa Mali Ya Haramu

 

Imepokewa kutoka kwa At-Tabarani kuwa Abu Hurayra (Radhiya Llaahu ‘anhu) amesema: kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((Anapotoka mwenye kuhiji kwa pesa njema akauweka mguu wake juu ya kipandio cha mnyama wake, akasema: "Labbayka Allahumma labbayk", (Nakuitikia ewe Mola wangu nakuitikia) hujibiwa na msemaji kutoka mbinguni, "Labbayka wa Sa’adayka (Mwitikio wako umekubaliwa na utafurahi kwa amali yako njema hii), kwa sababu zawadi yako (chakula na vifaa vyako) ni vya halali, na mnyama wako ni wa halali, na Hijjah yako inakubaliwa na haina madhambi".

Lakini anapotoka anayeihiji kwa pesa za haramu akauweka mguu wake juu ya kipandio cha mnyama wake akasema, "Labbayka Allahumma labbayk" (Nakuitikia ewe Mola wangu nakuitikia), hujibiwa kutoka mbinguni, "Laa labbayaka walaa sa’adayka. (Hakukubaliwi kuitikia kwako wala hutolipwa mema), kwa sababu vifaa vyako ni vya haramu na pesa zako ni za haramu na Hijjah yako ni ya dhambi na wala haikubaliwi".

Rudi ju

 

Kwanza – ‘Umrah

Miyqaat (Mipaka)

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ameweka Miyqaat ‘mipaka’ maalum ambayo yeyote anayekwenda Makka kwa nia ya kuhiji au kufanya ‘Umrah haruhusiwi kuivuka kabla ya kutia nia ya Ihraam mwahala hapo. Amewawekea watu wa Madiynah mji wa Dhul Hulayfah kuwa ni Mpaka wao. Mji huu unajulikana pia kwa jina la Abaar ‘Ali, nao upo Madiynah, kiasi cha Kilomita 450 mbali na Makkah.

 

Akawawekea watu wa Sham mji wa Al-Juhfa kuwa ni Miyqaat yao. Na Miyqaat ya watu wa Najd ni Qarn al Manazil. Amma watu wa Yemen Miyqaat yao ni mji wa Yalamlam. Na watu wa Iraaq Miyqaat yao ni Dhaata ‘Irq.

 

Hii ni mipaka aliyoiweka Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kisha akasema:

 

((Hiyo ni mipaka yao na ya kila apitae njia hizo, kwa wasio wakazi wa miji hiyo, kwa kila atakaye kuhiji au kufanya ‘Umrah.))

 

Mtu anapowasili katika mipaka hiyo anatakiwa aoge, ajisafishe, akate makucha na kujitia manukato akitaka. (Si vizuri kujitia manukato katika vazi la Ihraam, ingawaje si haram kufanya hivyo, isipokuwa sharti iwe kabla ya kutia nia ya kuhiji).

 

Unaweza kukoga na kuvaa Ihraam (vazi la kuhijia) pamoja na kufanya yote hayo ukiwa nyumbani kwako, hotelini au popote ulipofikia kabla ya kuifikia mipaka hiyo, isipokuwa nia lazima uitie ufikapo penye mipaka hiyo.

Rudi ju

 

Vizuri Kuswali Kabla Ya Kutia Niyyah

 

Utakapofika katika mojawapo ya mipaka iliyotajwa ukiwa bado hujaswali Swalah ya fardhi ya wakati huo, basi ni bora kuswali kwanza kisha utie niyyah. Amma ukiwa umekwishaswali, basi ni vizuri (si lazima) kusali raka’ah mbili Sunnah ikiwa wakati huo si katika nyakati zinazokatazwa kuswali, kisha unatia niyyah kwa kusema: “Labbayka ‘Umrah

 

Kisha unaanza kufanya Talbiyyah kwa kusema:

 

“Labbayka Allaahumma Labbayk. Labbayka Laa Shariyka Laka Labbayk, Inna Lhamda Wanni-‘mata Laka Wal Mulk Laa Shariyka Lak.”

 

Unaendelea hivyo njia yote, wanaume wanasema kwa sauti kubwa na wanawake kwa sauti ndogo huku ukimuomba Mwenyezi Mungu maghfira na kumdhukuru kwa wingi.

 

Unatakiwa pia uwe ukimswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam kwa wingi pamoja na kuamrisha mema na kukataza maovu unapokuwa safarini mpaka utakapowasili Makkah.

Rudi ju

 

Hukmu Ya Talbiyyah

 

Talbiyyah ni kutamka "Labbayka Allaahumma Labbayk. Labbayka Laa Shariyka Laka Labbayk, Inna Lhamda Wanni-‘mata Laka Wal Mulk Laa Shariyka Lak.”

 

Maulamaa wote wamekubaliana kuwa Talbiyyah ni kitendo kilichotolewa amri juu yake.

 

Kutoka kwa Ummus-Salama (Radhiya Llaahu ‘anha) amesema:

 

((Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akisema: ‘Enyi watu wa nyumba ya Muhammad, anayehiji kati yenu anyanyuwe sauti yake anapofanya Talbiyyah.)) [Imepokewa na Imam Ahmad na Ibni Hibban]

 

Maulamaa wamekhitilafiana katika hukmu yake, katika wakati wake, na katika kuichelewesha.

 

Imam Ash-Shaafi’iy na Imam Ahmad wanasema kuwa kitendo hicho ni Sunnah na kwamba mtu anatakiwa aanze kufanya Talbiyyah mara baada ya kutia nia ya Ihraam. Na iwapo ametia nia ya Hijjah kisha asifanye Talbiyyah, basi Hijjah yake inasihi na wala haina tatizo lolote.

 

Imam Maalik, yeye anaona kuwa kitendo hicho ni Wajib na mtu asipofanya Talbiyyah baada ya kutia nia ya Ihraam, akaendelea hivyo muda mrefu bila kufanya Talbiyyah, basi inampasa kuchinja mnyama.

Rudi ju

 

Fadhila Zake

 

Imesimuliwa na Jaabir (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((Muislam yeyote atakayefanya Talbiyyah tokea asubuhi mpaka jua linapozama, dhambi zake zitafutwa na atarudi (akiwa hana dhambi) kama alivyokuwa siku aliozaliwa na mama yake.)) [Imepokewa na Ibni Majah]

 

Imesimuliwa pia na Abu Hurayrah kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((Kila mwenye kuinyanyua sauti yake kwa kufanya Talbiyyah, anapewa bishara (njema), na kila mwenye kufanya Takbir (kutamka 'Allaahu Akbar') anapewa bishara (njema)” Akaulizwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bishara ya Pepo?” Akasema: “Ndiyo”)) [Imepokewa na At-Tabaraniy na Sa’iyd bin Mansuur]

Rudi ju

 

Kunyanyua Sauti Katika Talbiyyah

 

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((Alinijia Jibriyl akaniambia: “Waamrishe sahibu zako wanyanyuwe sauti zao katika Talbiyyah, kwani hiyo ni katika alama za Hijjah.”)) [Imepokewa na Ibni Majah. Imam Ahmad, Ibni Khuzaymah na Al Hakim]

 

Na kutoka kwa Abubakar (Radhiya Llaahu ‘anhu) amesema:

 

((Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliulizwa: “Amali gani iliyo bora katika Hijjah?” Akajibu: “Al ajji wa thajji” (Kunyanyua sauti katika kufanya Talbiyyah na kuchinja).)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy na Ibni Majah]

Rudi ju

 

Twawaafu ya ‘Umrah

 

Unapowasili Makkah unaanza kufanya ‘Umrah kwa taratibu ifuatayo:

 

Unatufu’, kwa kuizunguka Al-Ka’abah mizunguko saba ukianzia penye jiwe jeusi (Al Hajar al aswad), ukiwa mbali na jiwe hilo anzia sawa na jiwe jeusi.

 

Kabla ya kuanza kutufu lielekee Jiwe jeusi kisha linyoshee mkono (ukiweza kulifikia na kulibusu au kuligusa bila ya kuumiza watu ni vizuri), la kama utasababisha madhara kwa watu au kwa nafsi yako, inatosha kuliashiria tu kwa mkono wa kulia kwa mbali huku ukisema: “Bismillahi Allaahu Akbar” Kisha unaizunguka Al-Ka’abah ikiwa kushotoni kwako mizunguko saba.

 

Kwa wanaume ni vizuri katika mizunguko mitatu ya mwanzo kukimbia kidogo kidogo mfano wa mtu anayekimbia juu ya mchanga, na mizunguko minne iliyobaki unakwenda mwendo wa kawaida. Wanawake wanakwenda mwendo wa kawaida katika mizunguko yote saba.

 

Wakati wote huo unatakiwa uwe ukisoma du’aa zozote ulizohifadhi. Hapana kisomo maalum au du’aa maalum, bali unaweza kuomba du’aa yoyote na kwa lugha yoyote, na unaweza pia kusoma sura ulizohifadhi katika Qur-aan.

 

Al-Ka’abah ina nguzo nne, na maarufu katika hizo ni nguzo ya jiwe jeusi na nguzo iliyo kabla yake ambayo ni nguzo ya Yaman (Ar-Rukn al-Yamani). Unapoifikia nguzo ya Yaman (Ar-Rukn al-Yamani) ni vizuri kuigusa. Hutakiwi kuibusu wala kuiashiria kama unavyolifanyia jiwe jeusi. Na unapokwenda baina ya nguzo hiyo ya Yamani na Jiwe Jeusi ni vizuri kuomba na kuikariri du’aa ifuatayo.

“Rabbana Aatina Fidduniya Hasanatan Wa Fil Aakhirati Hasanatan Wa Qinaa ‘Adhaaba Nnaar”.

 

Na maana yake ni:

 

(Mola wetu tupe katika dunia yaliyo mema, na katika akhera (tupe) yaliyo mema, na utuepushe na adhabu ya Moto).

 

Unaendelea hivyo mpaka utakapolifikia Jiwe jeusi. Hapo utakuwa umekwishamaliza mzunguko wa mwanzo, na utaanza mzunguko wa pili kwa kunyanyua mkono wa kulia huku ukiliashiria tena jiwe jeusi na kusema: “Allaahu akbar”, kisha utatenda yale yale uliyotenda katika mzunguko wa mwanzo, mpaka umalize mizunguko saba.

 

Kila unapolifikia jiwe jeusi au unapokuwa sawa nalo, unanyanyua mkono wa kulia na kulielekea jiwe huku ukisema: “Allaahu Akbar”

Rudi ju

 

Maqaam Ibraahiym

 

Ukishamaliza kutufu mara saba, unakwenda kuswali raka’a mbili nyuma ya Maqaam Ibraahiym. Katika raka’a ya mwanzo unasoma Alhamdu na Qul ya ayyuha l kaafiruun na katika raka’a ya pili unasoma Alhamdu na QulhuwAllaahu ahad.

 

Usipoweza kuswali penye Maqaam Ibraahiym kwa sababu ya msongamano mkubwa wa watu, unaweza kuswali popote karibu na hapo au popote mbali na hapo sharti iwe ndani ya msikiti.

Rudi ju

 

Kunywa Maji Ya Zamzam

 

Baada ya kumaliza kutufu na kuswali raka’a mbili penye Maqam Ibrahim, ni vizuri kunywa maji ya Zamzam. Unaweza kunywa kutoka katika majagi ya maji yaliyoenezwa msikitini hapo, na unaweza pia kwenda penye mifereji (mabomba) ya maji ya Zamzam yaliyokuwepo penye uwanja wa Swafaaa na Marwah.

 

Imepokewa kutoka kwa Al-Bukhaariy na Muslim kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikunywa maji ya Zamzam kisha akasema: ((Maji haya yamebarikiwa, yanamshibisha mwenye njaa na yanamponesha mgonjwa.))

Rudi ju

 

Sa’ay Baina Ya Swafaaa Na Marwahh

 

Swafaaa na Marwah ni vilima viwili vilivyoelekezana, vilivyomo ndani ya msikiti upande wa kisima cha Zamzam.

 

Ukimaliza kutufu na kunywa maji ya Zamzam, unakwenda penye jabali Swafaaa kwa ajili ya kuanza kufanya ibada ya Sa'ayi, baina ya majabali Swafaaa na Marwah.

 

Unaanza kwa kupanda Swafaaa huku ukisema:

“Inna Swafaa walMarwahta min shaairi llah". kisha unasema "Abdau maa badaa llahu bihi”, na maana yake ni:

 

(“Hakika Swafaaa na Marwah ni katika alama za kuadhimisha dini ya Mwenyezi Mungu. Ninaanza pale alipoanzia Mwenyezi Mungu. (Ambaye ndani ya Qur-aan tukufu ameanza kulitaja jabali Swafaaa kisha Marwah).

 

Si lazima kutamka maneno hayo, lakini hi ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alisema na kufanya hivyo.

 

Unapowasili juu ya Swafaaa unaelekea Qiblah kisha unasema:

 

ÇáÍãÏ ááå - Çááå ÇßÈÑ - áÇ Åöáåó ÅáÇøó Çááåõ æóÍúÏóåõ áÇ ÔóÑöíßó áóåõ¡ áóåõ Çáãõáúßõ æóáóåõ ÇáÍóãúÏõ æåõæó Úóáì ßõáøö ÔóíÁò ÞóÏíÑñ¡ áÇ Åöáóåó ÅáÇ Çááåõ æóÍúÏóåõ ÃóäúÌóÒó æóÚúÏóåõ¡ æóäóÕóÑó ÚóÈúÏóåõ æóåóÒóãó ÇáÃóÍúÒóÇÈó æóÍúÏóåõ.

 

“Alhamdu Lillahi Allaahu Akbar La Ilaha Illa Llahu Wahdahu Laashariyka Lahu Wahuwa Alaa Kulli Shay-In Qadiir. La Ilaha Illa Llahu Wahdau, Anjaza Waadahu Wanawsara ‘Abdahu Wahazamal Ahzaaba Wahdahu” Unasema hivyo mara tatu.

 

Hivi ndivyo alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Kama hukuweza (kutokana na zahma au kama hujaweza kuhifadhi vizuri) basi unasoma hata mara moja tu, au unaomba du’aa yoyote na kusoma chochote unachoweza kusoma. Kisha teremka na ufanye "Sa’ay ya Umra”.

 

Na Sa’ay ni kwenda baina ya Swafaaa na Marwah mara saba (Kwenda, inahisabiwa mara moja, na kurudi mara moja). Ni vizuri kukimbia kidogo kidogo kila unapozifikia alama za kijani zilizo ukutani baina ya Swafaa na Marwah, lakini wanawake, wao wanakwenda mwendo wa kawaida. Ukifika Marwah, unapanda juu na kusema pamoja na kufanya yale uliyoyafanya ulipokuwa juu ya Swafaaa.

Hakuna katika Twawaafu wala katika Sa’ay, du’aa au kisomo maalum. Soma chochote na omba du’aa yoyote.

Rudi ju

 

Kujihalalisha

 

Ukishamaliza kufanya Sa’ay, unapunguza nywele zako au unazinyoa zote. Kwa wanaume ni vizuri kunyoa, kama alivyofanya na kupendekeza Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Lakini wanawake, wao wanapunguza kidogo tu.

 

Hapo utakuwa umekwisha maliza ibada ya ‘Umrah na unaweza kuvua nguo za Ihraam na kuvaa nguo zako za kawaida. Na kinakuhalalikia kila kitu  ulichoharamishiwa ulipokuwa katika Umrah, hata mkeo. (Kama ni ‘Umrah ya Hijjah unaisubiri tarehe 8 Dhul-Hijjah ili uanze ibada ya Hijjah.)

Rudi ju

 

Fadhila Za Kunyoa Nywele Zote

 

Kutoka kwa Abdillahi bin ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((“Mwenyezi Mungu Awarehemu walionyoa (nywele zote)” Masahaba (Radhiya Llaahu ‘anhum) wakasema: “Na waliopunguza je ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Mwenyezi Mungu awarehemu walionyoa (nywele zote).” Wakasema: “Na waliopunguza je ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Mwenyezi Mungu awarehemu walionyoa (nywele zote).” Wakasema: “Na waliopunguza je ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Na waliopunguza.”))

 

Katika Hadiyth hii Mtume Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amewaombea rehema mara tatu walionyoa nywele zote na akawaombea mara moja tu waliopunguza.

 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuingize katika Rahmah Yake – Aamin

Rudi ju

 

Hijjah

 

Tarehe nane Dhul Hijjah inaitwa "Siku ya Attarwiyah”, nayo ni siku inayoanza Ibada za Hijjah. Likishatoka jua la siku hiyo, oga na uvae nguo zako za Ihraam ukiwa nyumbani, hotelini au popote ulipofikia mjini Makkah au nje yake kisha sema: “Labbayka Hijjah”. Masharti ya Ihraam ni yale yale tuliyoyataja hapo mwanzo katika ibada ya ‘Umrah.

 

Asubuhi ya siku hiyo Mahujaji wanaondoka Makkah kuelekea Minaa na wanaswali mahali hapo Swalah ya Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, Isha ya siku hiyo, pamoja na Swalah ya Alfajiri ya siku ifuatayo. Kila Swalah inaswaliwa katika wakati wake Qasran (kwa kufupisha). Unazifupisha Swalah za raka’a nne unaziswali raka’a mbili, ama Swalah ya Magharibi unaiswali kwa ukamilifu – raka’a tatu.

Rudi ju

 

‘Arafah

Hukmu yake

 

Kusimama y ni nguzo kubwa kupita zote katika nguzo za Hijjah, na hii inatokana na Hadiyth ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) aliposema:

 

((Al Haju ‘Arafah – (Kusimama) Arafa ndiyo Hijjah yenyewe - atakayewahi usiku wa kujikusanya kabla ya kuingia alfajiri (ya siku ya ‘Arafah) basi amewahi”.)) [Imepokewa na Imam Ahmad pamoja na ma Imam wengine wa Hadyith]

Rudi ju

 

Kusimama ‘Arafah

 

Likishatoka jua la tarehe tisa Dhul Hijjah, Mahujaji wanaondoka Minaa na kuelekea ‘Arafah kwa utulivu na tahadhari, huku wakisema: “Allaahu akbar” – au “Laa ilaaha illa Allaah” au huku wakilabiy kwa kusema:

“Labbayka Allahumma Labbayk Labbayka Laa Shariyka Laka Labbayk - Inna Lhamda Wanni’mata Laka Wal Mulk Laa Shariyka Laka.”

Wanakwenda kwa utulivu bila kuwaudhi wenzao, na wanaziswali Swalah za Adhuhuri na Alasiri wakati mmoja hapo ‘Arafah, Qasran, zote wakati wa Adhuhuri, kwa adhana moja na iqama mbili.

 

Ni vizuri kubaki katika sehemu ya Namirah, mahali ulipo msikiti mkubwa wa Namirah na wasiingie ‘Arafah mpaka baada ya wakati wa zawaal (Kiasi cha saa sita za mchana).

 

Hii siyo lazima, hasa kutokana na zahma za hapo ‘Arafah siku hiyo, isipokuwa ni bora kama ikiwezekana. Hakikisha kuwa umo ndani ya mipaka ya ‘Arafah, na unapokuwa mahali hapo patakatifu, zidisha kuomba du’aa na kumtaja Mola wako huku ukiwa umeelekea Qiblah, kwa sababu siku hiyo na mahali hapo ndipo watu wanapoghufiriwa madhambi yao yote na kurudi makwao kama siku waliyozaliwa.

 

Nyakati za jioni tafuta sehemu za juu juu. Panda, kisha elekea Qiblah na unyanyue mikono yako juu huku ukiomba, kama alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).

 

Imesimuliwa na Jaabir (Radhiya Llaahu ‘anhu) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((“Hakuna siku bora kwa Mwenyezi Mungu kuliko siku kumi za (mwanzo) za Dhul Hijjah”. Mtu mmoja akamuuliza: “Siku hizo ni bora, au mtu anapokuwa katika Jihadi kwa muda huo?” Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamuambia: “Siku hizo ni bora kuliko idadi ya siku hizo katika Jihadi fiy sabiili Llah. Na hapana siku iliyo bora kwa Mwenyezi Mungu kuliko siku ya ‘Arafah. Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala huwaambia Malaika wake kwa fahari: “Tazameni waja wangu, wamekuja nywele zao zikiwa zimetimka, wamejaa mavumbi, wametoka kila sehemu za mbali wakitaraji rehema Zangu na wala hawakuwahi kuiona adhabu Yangu”. Hakuna siku ambayo Mwenyezi Mungu anawaepusha watu wengi na moto kuliko siku hiyo”.)) [Imepokewa na Abu Ya’ala – Al-Bazzaar – Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan]

 

Imepokewa pia kuwa Anas bin Maalik (Radhiya Llaahu ‘anhu) amesema:

 

((“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alisimama ‘Arafah wakati jua linakaribia kuzama, akasema: “Ewe Bilaal! Ninyamazishie watu.” Bilaal (Radhiya Llaahu ‘anhu), akainuka na kuwataka watu wanyamaze. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akasema:

“Enyi watu! Alinijia Jibril hivi punde na kunipa salam zitokazo kwa Mola wangu. (Kisha) Akasema: ‘Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala amewaghufiria watu wa ‘Arafah na watu wa Masha'ari l haraam (Muzdalifah).” Akainuka ‘Umar bin Khattab (Radhiya Llaahu ‘anhu) akauliza: “Hizi (salam na haya maghfira) ni kwa ajili yetu peke yetu?” Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Hizi ni zenu na za wote watakaokuja (hapa) baada yenu mpaka siku ya Qiiyaamah.” ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) akasema: “Kheri za Mwenyezi Mungu ni nyingi na nzuri.”))

 

Imesimuliwa na Ibnul Mubarak kutoka kwa Sufyaan Ath-Thawriy kuwa:

 

'Mtu anapokuwa hapo anatakiwa ajishughulishe na kuomba du’aa pamoja na kumtaja Mwenyezi Mungu sana ili arudi akiwa amefaidika na ameghufiriwa, na asiwe katika waliokula hasara siku hiyo kwa kuyakosa maghfira ya Mwenyezi Mungu.'

 

Jua likishazama Mahujaji wanaondoka ‘Arafah na kuelekea Muzdalifah. (Usiswali Magharibi hapo ‘Arafah).

Rudi ju

 

Muzdalifah

 

Unapokuwa Muzdalifah utaswali Swalah ya Magharibi na ‘Ishaa wakati wa ‘Ishaa, raka’a tatu za Magharibi kisha mbili za ‘Ishaa kwa adhana moja na Iqama mbili. Kisha utabaki hapo mpaka baada ya Swalah ya Alfajiri.

 

Ukiwa hapo utaomba du’aaa kwa wingi huku ukinyanyua mikono yako juu na kuelekea Qiblah kama alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam).

 

Ukiwa Muzdalifah utaokota mawe ya kupigia Jamaraat. (Jamaraat ni milingoti mikubwa mitatu ya mawe yanayopigwa hapo Minaa ambayo watu wengine huyaita Mashetani). Unaokota mawe saba tu, (si lazima kuokota mawe yote hapo Muzdalifah), na mawe mengine utaweza kuokota ukiwa Minaa. Unaweza pia kuokota mawe yote ukiwa hapo kama ukitaka.

Rudi ju

 

Minaaa

 

Utaondoka Muzdalifa kwa utulivu na kuelekea Minaa baada ya Swalah ya Alfajiri na kabla ya kutoka jua.

 

Utakapowasili Minaaa unafanya yafuatayo:

 

1.     Unalipiga Jamaratul ‘Aqabah ambalo watu wanaliita Shetani Mkubwa, lililo karibu na Makkah kwa mawe saba, moja baada ya jingine. Kila unaporusha jiwe unasema:

 

Allaahu Akbar".

 

(Haijuzu kuvurumisha mawe yote saba kwa pamoja).

 

Jamaraat’ si mashetani kama wanavyoitakidi baadhi ya watu wenye kuvurumisha mawe kwa ghadhabu na kutukana na wengine huvurumisha mawe makubwa wakidhani kuwa wanampiga na kumkomesha shetani. Hayo yote hayajuzu, kwa sababu ‘Jamaraat’ yamewekwa kwa ajili ya kujikumbusha tu namna gani Nabii Ibraahiym mahali hapo alivyompiga mawe shetani aliyejaribu kumshawishi asimchinje mwanawe kama alivyoamrishwa na Mola wake.

 

Kwa hivyo mtu anatakiwa arushe mawe madogo sana na kuyapiga Jamaraat kwa nia ya kutii amri ya Mwenyezi Mungu tu, bila ya kuingiza fikra nyingine.

 

Kwa wale wasiojiweza wanaweza kumwakilisha mtu awapigie, na mtu mmoja anaweza kuwakilishwa na wengi.

(Kumbuka siku ya mwanzo unalipiga mawe Jamarat moja tu, tofauti na siku zilizobaki unapoyapiga mawe Jamaraat zote tatu).

 

2.     Chinja mnyama wako, na ni vizuri kama utakula katika nyama hiyo na nyengine utawapa masikini.

 

3.     Punguza au nyoa nywele zako. (kunyoa nywele zote ni bora zaidi), na mwanamke anakata nywele zake kidogo tu.

 

Utaratibu huu ni bora zaidi ingawaje unaweza kutanguliza hiki kabla ya kile. Ukimaliza kupiga mawe, kuchinja na kunyoa, unakuwa umekwisha jihalalisha uhalalisho mdogo na unaweza kuvaa nguo zako za kawaida na kufanya yote uliyokatazwa ulipokuwa na Ihraam, isipokuwa tu huwezi kumwingilia mkeo mpaka umalize Twawaaful Ifaadhwah (Twawaafu ya Hijjah).

Rudi ju

 

Twawaaful Ifaadhwah

Hukmu yake

 

Maulamaa wote wamekubaliana kuwa Twawaaful Ifaadhwah (Twawaafu ya Hijjah) ni katika nguzo za Hijjah, na kwamba asiyetufu Twawaafu hiyo Hijjah yake inabatilika.

 

Na hii inatokana na kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema:

 

{{Kisha wajisafishe taka zao, na watimize nadhiri zao, na waizungike Nyumba ya Kale (Nyumba kongwe – Al-Ka’abah).}} [Al Hajj – 29]

 

Ukishamaliza shughuli za hapo Minaa, unakwenda Makkah na unafanya Twawaaful Ifaadhwah, nako ni kuizunguka Al-Ka’abah mara saba na kufanya kama ulivyofanya katika Twawaafu ya ‘Umrah. Kisha unafanya Sa’ay, kutembea baina ya Swafaaa na Marwah na kufanya kama ulivyofanya mara ya mwanzo ulipofanya ‘Umrah.

 

Ukishamaliza, unakuwa umekwisha jihalalishia halalisho kubwa na kwa hivyo, hata mkeo anakuhalalikia. Unaweza kuiahirisha Twawaafu ya Ifaadhwah mpaka baada ya kumaliza shughuli zote za Minaa.

 

Ukishamaliza Twawaafu ya Ifaadhwah unarudi Minaa na unabaki hapo usiku wa tarehe 11, 12 na 13 kwa wasiokuwa na haraka. Hizo zinaitwa siku za Tashriyq. Inatosha kama utabaki hapo usiku wa tarehe 11 na wa 12 tu.  Katika siku 2 au 3 hizo unapiga mawe Jamaraat zote tatu kila siku kwa mpangilio ufuatao:

 

Anza kupiga Jamaraat la mbali na Makkah, (Jamaraat dogo) kisha la kati, kisha Kubwa (Jamarat al Aqaba). Kila moja piga kwa mawe saba huku ukisema: "Allaahu Akbar", kila unaporusha jiwe. Hii ni kwa siku tatu zilizobaki.

Rudi ju

 

Nyakati za kupiga mawe

 

Siku ya An-Nahr – Sikukuu mosi, usipige mawe mpaka jua lichomoze:

 

((Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alipokuwa Muzdalifah aliwatanguliza Minaa watu dhaifu na wazee na wanawake, akawaambia: “Musirushe mawe mpaka jua litoke”)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy]

 

Mwenye udhuru anaweza kuchelewesha mpaka kabla ya Magharibi, lakini ni vizuri kupiga mawe baada ya kutoka jua na kabla haijaingia Magharibi kwa asiyekuwa na udhuru. (Baadhi ya Maulamaa wanajuzisha kupiga mawe baada ya Magharibi kwa udhuru, lakini bora ujaribu kupiga kabla jua kuzama).

 

Wakati wa kurusha mawe kwa siku mbili zilizobaki au siku tatu kwa wale wasiotaka kuharakisha, ni baada ya Zawal (wakati wa adhuhuri pale jua linaposogea kidogo baada ya kuwa katikati).

Rudi ju

 

Kuomba Du’aa

 

Ni vizuri kuelekea Qiblah na kuomba du’aa baada ya kumaliza kupiga kila Jamaraat isipokuwa Jamaraat la mwisho. Hadiyth iliyosimuliwa na Al-Bukhaariy na Imam Ahmad inasema:

 

((Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akeshapiga kila Jamaraat kwa mawe saba akisimama na kuelekea Qiblah na kuomba du’aa, isipokuwa baada ya kulipiga Jamaraat la mwisho hakusimama.)) [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Imam Ahmad]

Rudi ju

 

Siku Ya Kuharakisha

 

Ikiwa unataka kubaki hapo kwa mda wa siku mbili tu, basi siku ya tarehe Kumi na mbili Dhul Hijjah ambayo hujulikana kama ni "Yawmul isti’ijaal" - Siku ya Kuharakisha – unapiga mawe na kuondoka Minaa kabla ya jua kuzama, na ikiwa utakawia kuondoka ukawepo hapo baada ya juwa kuzama itakubidi ubaki hapo siku moja zaidi. Ni vizuri kubaki usiku wa tatu ikiwa huna cha kukushughulisha.

Rudi ju

 

Twawaaful Wida’a

 

Unapotaka kurudi nchini kwako baada ya kumaliza shughuli za Hijjah, unatufu Twawaaful wida’a, (Twawaafu ya kuaga) nayo ni kama ifuatavyo:

 

Unatufu Al-Ka’abah mara saba na kufanya kama ulivyofanya katika Twawaafu za mwanzo, lakini mara hii bila ya kufanya Sa’ay baina ya Swafaa na Marwah.