Hivi ndivyo wanavyosherehekea siku ya Ashura

 

Imeandikwa katika Nahjul Balaghah kuwa Ali bin Abu Talib (RA) alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake katika mji wa Al Kufa alisema;

    Raia kwa kawaida huwa wanaogopa wafalme wao madhalim, lakini mimi leo naogopa wafuasi wangu madhalim. Nimekuiteni katika jihadi mkakataa, nikakusemesheni lakini hamkutaka kunisikia, nikakuiteni kwa siri na kwa dhahiri mkanikatalia, nikakunasihini mkakataa nasaha zangu. Hivo walokuwepo wanaweza kuwa sawa na wasiokuwepo, na watumwa sawa na wanaomiliki? Nikikusomeeni hukmu nyinyi mnanikimbia, nakuwaidhini mawaidha mazuri mnafarikiana nayo, nakuhimizeni katika jihadi dhidi ya wavukao mipaka, siwahi hata kumaliza maneno yangu mnafarikiana makundi mengi, mnarudi katika majlis zenu huku mkiendeana kinyume, leo mumenyoka kesho yake mnakuwa kama majoka, Wavivu wakubwa.

    Enyi ambao miili yenu iko hadhir lakini akili zenu hazipo! Kila mmoja kati yenu anafuata matamanio yake. Enyi ambao mkubwa wenu amepata mtihani mkubwa kupata wafuasi kama nyinyi! Mkubwa wenu anamcha Mungu na nyinyi mnamuasi, YARETI wallahi kama Muawiya atakubali ningebadilishana naye kama Dinari inavyobadilishwa kwa Dirham. Ningempa kumi katika nyinyi na yeye anipe mmoja tu katika watu wake.

Enyi watu wa mji wa Al Kufa nimepewa mtihani mitatu kwa miwili. Nyinyi ni viziwi wenye masikio, mabubu wenye maneno mengi, vipofu wenye macho, hamna ukweli katika mapambano, na wala si ndugu wa kuaminika katika mitihani, mikono yenu imeingia michanga, enyi mfano wa ngamia wasio na wachungaji! Kila ninapokukusanyeni upande mmoja mnafarikiana upande mwingine.

Nahjul Balaghah 187/1-189