Kiongozi wa Kabila la Janjaweed – Sudan:

“Nitakubali ikiwa makundi yote yatakubali kuweka silaha zao chini”

Musa Hilal

Khartoum 3/4/2004

Kutoka Islam Online

Akizungumza na Islam Online Bw. Musa Hilal kiongozi wa kabila la Waarabu la Janjaweed huko Sudan alisema kuwa watu wake watakubali kuweka silaha zao chini na kujisalimisha mbele ya serikali ya Sudan iwapo makundi yote yenye silaha huko Darfur yatakubali kufanya hivyo pia.

Akijibu tuhuma za seikali ya Marekani pamoja na azimio la Umoja wa Mataifa la hivi karibuni lionaloitaka serikali ya Sudan kuwalazimisha watu wa kabila la Janjaweed kusalimisha silaha zao serikalini katika muda usiozidi mwezi mmoja Bw.Musa alisema: “Azimio la Umoja wa Mataifa la kuwataka watu wa kabila lake kutupa silaha zao chini lazima lijumuishe makundi yote yanayopambana huko Darfur na si kabila lake peke yake

Miongoni mwa makundi muhimu yanayopambana na serikali ya Sudan huko Darfur ni lile linalojiita Jeshi la Haki na Uadilifu (Equality Movement (Jem)) na Jeshi la Ukombozi wa Sudan (Sudan Liberation Army (SLA))

Akieleza juu ya kukubali kwake azimio la Umoja wa Mataifa linalohusu mkoa wa Darfur Bw. Hilal alieleza kutoridhika kwake juu ya ibara inayowataka watu wa kabila lake la Janjaweed peke yao kutupa silaha zao chini, akasema: “Ikiwa ni watu wa kabila langu peke yao ndio wanotakiwa kuranya hivyo basi sitokubali hata kulisoma azimio hilo.. Kwa mantiki gani wanazungumza hawa kuwa sisi peke yetu tutupe silaha zetu chini kisha tuwe mawindo mepesi ya kuanzgamizwa na wengine

Jina la Bw. Hilal linabeba nambari 1 katika orodha iliyowekwa na Serikali ya Kimarekani yenye majina ya viongozi 7 wa makabila ya Janjaweed ya Kiarabu. Orodha hiyo inawatuhumu watu hao kuwa waliwaua na kuwaunguza watu wa makabila ya Kiafrika katika mkoa wa Darfur huko Sudan, na kwa jili hiyo Ijumaa iliyopita tarehe 30/07/2004 Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio kuipa serikali ya Sudan muda usiozidi mwezi mmoja kuwanyang’anya silaha Janjaweed na iwapo watashindwa kufanya hivyo basi serikali hiyo itawekewa vikwazo vya uchumi.

 

Hilal aitahadharisha serikali ya Kimarekani

Hilal aliitahadharisha serikali ya Kimarekani pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa wasije wakaingia katika shimo la upotofu unaozushwa na makundi ya waasi wa Sudan. Aliendelea kusema: “Ikija kuwa hivyo, basi mambo yatakuwa mabaya kwao kama yalivyo huko Iraq ambapo Idara zenu za upelelezi ziliudanganya ulimwengu na kuwaingiza ndani ya shimo mkashindwa kutoka ndani yake mpaka hivi sasa, na uvamizi huo haukukuzidishieni kheri yoyote isipokuwa umekuzidishieni kuchukiwa na watu wote wa eneo hili na kuhatarisha maslahi yenu”.

 

Haki kwa wote

Bw. Hilal aliongeza kusema: “Ikiwa wanataka kutoa uamuzi wowote dhidi yangu, basi mimi sina kipingamizi, lakini lazima kwanza ufanyike uchunguzi kwa njia ya uadilifu, na ni wajibu wao kuchgua kamati itakayotafuta ukweli bila ya upendeleo, na isiwe kusudi lake kamati hiyo kuzusha tuhuma za uongo, bali kusudi lake liwe ni kuutafuta ukweli na uadilifu katika pande zote

Alisema pia kuwa mahkama itakayohukumu kwa uadilifu itamtakasa na tuhuma za uongo walizomzulia.

Bw. Hilal alipendekeza ufanyike mkutano utakaojumuisha makundi yote kwa ajili ya kupatanisha na kuweka misingi ya amani na kuondoa matatizo yote yaliyorimbikika. Alisema: “Napendekeza litafutwe suluhisho la daima, na pande zote - zile zenye asili ya Kiarabu na zenye asili ya Kiafrika zipate haki zao sawa sawa. Na sisi hatuna chuki dhidi ya kundi lolote lile na wala hatutaki kupewa na yeyote, si serikali wala upinzani. Sisi tupo hapa tokea mamia ya miaka iliyopita na hatutaki jengine isipokuwa kubaki. Na maslahi yetu pia yaendelee kama yalivyo, na uamuzi wowote utakaoyadhuru maslahi yetu hatuyakubali na tunasema kuwa uamuzi huo unaweza kumleta (John) Garang mpya

 

Sisi ndio tuliodhurika zaidi

Bw. Hilal alisema pia kuwa waliodhurika zaidi na matukio ya Darfur ni Waarabu, na kwamba sababu kubwa ya kuundwa kwa majeshi ya waasi ni: “Kwa ajili ya kutufukuza sisi hapa Darfur na pia kutoka sehemu yote ya Magharibi ya Sudan ili lianzishwe taifa jingine lisilokuwemo ndani yake makabila ya Kiarabu

Akasema: “Tokea mwaka 1980 walikuwa wakieneza chuki dhidi yetu, wakitaka Waarabu wafukuzwe nje ya Mkoa wa Magharibi ya Sudan, bali nje ya Sudan yote, maana wao wanatuhesabu kuwa sisi ni wageni katika nchi hii. Na hapo mwanzo walikuwa wakituibia mali zetu na kuwaua watu tena kwa kufanya mipango maalumu, na sisi tuliwahi kutahadharisha juu ya jambo hilo.

Aliendelea kusema: “Lakini serikali zote zilizotangulia ikiwemo hii ya Muhammad Al Bashir zilipuuza tahadhari zetu na kutuacha peke yetu tukipambana na waasi wenye asili ya Kiafrika waliopewa mafunzo ya kisasa ya kupigana vita pamoja na silaha za kisasa na wala hatukuwahi hata siku moja kuusikia Umoja wa Mataifa ukisema lolote kutaka tusishambuliwe kama ilivyo hivi sasa. Walikuwa wapi

Bw. Hilal alikanusha kuwa anapigana vita dhidi ya makabila ya Kiafrika  kwa ajili ya kuisaidia serikali ya Sudan akasema: “Nakanusha kuwa hapana hata Mwarabu mmoja kutoka katika makabila ninayoyaongoza mimi aliyewahi kukishambulia kijiji chochote au kufanya jambo lolote kumdhuru Muafrika yeyote yule. Yale mapambano yanayotokea mara kwa mara baina yetu na baina ya makabila ya Al For na Zaghawa na Samalit yalikuwa ni kwa ajili ya kujihami tu na mashambulizi yao, kwani wao wamepewa mafundisho kamili ya kivita na wanayo makundi ya ‘militia’, na sisi tulichokuwa tukifanya ni kujihami nafsi zetu kutokana na mashambulizi yao na  uadui wao na hatujapata hata siku moja kuanzisha sisi mashambulizi ya aina yoyote

Tulichowahi kufanya sisi ni kujiunga na jeshi la ukombozi pale serikali ilipotangaza kuunda jeshi la kupambana na waasi, na vijana wetu wapatao elfu 3 walijiunga na jeshi hilo ambalo ndani yake hayakuwepo makabila ya Kiarabu peke yake, bali makabila ya Kiafrika yanayotokana na makabila hayo ya Al For na Zaghawa na Samalit pia yalijiunga na jeshi hilo wale waliokuwa wakipinga uasi.

Alipoulizwa; ‘Kwa nini basi hatuoni wakimbizi kutoka makabila ya Kiarabu katika kambi za Darfur’ Bw Hilal alisema: “Walituunguzia vijiji vyetu vingi sana, na wengi kati ya watu wa makabila yetu iliwalibidi kuacha nyumba zao, lakini sisi Waarabu hatukubali kuwapeleka wanawake zetu na na watoto wetu katika kambi za wakimbizi wakaomba chakula na nguo kutoka katika jumuiya za kusaidia watu, bali sisi wenyewe tunawahami na kuwaweka katika majumba yetu na kuwalisha na kuwavisha katika chakula chetu