KHALID NA HAYDAR

Utangulizi 1

Kadhia ya Uimamu. 4

Kuwakufurisha Waislamu. 9

Kumlilia Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) 16

Kukingwa 15

Ziara ya kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) 19

Kupiga vifua. 23

Wali na nyama. 25

Kwa nini Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu)?. 27

Hitimisho. 31

 

 

 

Kimeandikwa na Abdullah Abdul Rahman Al Raashid

Kimefasiriwa na Muhammad Faraj Salem Al Saiy

 

Utangulizi

 

Hakika shukrani zote anazistahiki Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, tunamuomba atusaidie katika shida zetu, atusamehe madhambi yetu, atukinge na shari za nafsi zetu na shari za amali zetu ovu.

Swala na salamu zimfikie yule aliyeletwa akiwa ni rehma kwa walimwengu wote, aliyeufikisha ujumbe, akaiwasilisha amana, akawanasihi umma, na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki. Mola wetu mtukufu tunakuomba umswalie na umsalimie Mtume wako huyu pamoja na Aali zake na Sahaba zake wakarimu.

Yule atakaye Mwenyezi Mungu kumuongoza basi hapana wa kumpoteza, na anayeachiwa basi hana wa kumuonoza. Ninakiri kuwa hapana apasaye kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Asiye na mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ni Mtume wake wa mwisho na mjumbe wake wa mwisho.

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:

Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Al Hashr 7

 

Na Akasema:

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema (mfano mwema wa kuufuata) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.

Al Ahzab 21

 

Na Akasema:

Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.

Al Fath 28

 

Na kasema:

Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa?

Yunus - 32

 

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

Hakika ya ukweli unaongoza katika wema, na wema unaongoza Peponi. Na mtu huwa anapenda kusema kweli na anahakikisha kuwa kila asemalo ni la kweli, mpaka anaandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni msemakweli.

Na hakika ya uongo unaongoza katika uovu, na uovu unaongoza Motoni. Na mtu huwa anapenda kusema uongo na anahakikisha kuwa kila asemalo anatia uongo ndani yake, mpaka anaandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni (mtu) muongo.

Bukhari na Muslim

 

Kutokana na aya na hadithi zilizotangulia, tunafahamu kuwa Muislamu wa kweli ni yule ambaye mara anapotambua kuwa itikadi aliyo nayo inakwenda kinyume na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) basi huiacha mara moja bila kubishana na bila kutafuta visingizio, na hakubali kufuata ila yale tu aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliyetumwa na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala kwa uongofu na Dini ya Haki.

Na Muislamu wa kweli anayeitaka Pepo ya Mola wake hakubali kufuata yale aliyoyakuta ndani ya vitabu visivyo na ushahidi wowote wa kielimu ndani yake, vitabu vilivyojaa hadithi za uongo, visivyokuwa na wapokezi wanaojulikana (narrators).

Ukweli siku zote uko wazi na hauhitajii kupambwa kwa falsafa, lakini uongo, ndio wenye kujificha na unahitajia kupambwa sana ili uweze kubabaisha.

Elimu ya kweli ni ile yenye kauli za; Mwenyezi Mungu Amesema,au Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema.

( )

Muislamu ni mtu mwenye hekima, na hawezi kukubali kila anachotupiwa masikoni mwake bila kupima na kutumia akili, kwani anajua vizuri kuwa dini hii ni dini ya haki, na kwamba Siku ya Kiama atakuja kuulizwa juu ya kila alichotenda.

Mwenye akili timamu ataona kuwa ndani ya vitabu vya Shia mna maelfu kwa maelfu ya hadithi Maudhui walizosingiziwa watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa wamesema, lakini ukweli ni kuwa hadithi hizo zimepachikwa tu na watu wasiopenda kuuona Umoja wa Kiislamu ukisonga mbele.

Anayetaka kujadiliana kwa nia ya kuupata ukweli, basi lazima aondoe inadi na siku zote sikio lake liwe wazi, na mara anapouna ukweli basi aufuate, na asiwe kama wale waliosema:

Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.

Al Zukhruff 22

 

Bali awe katika wale wanaosema:

Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.

Yusuf 108

 

Na asiutie kufuli moyo wake hata ikamsibu kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?

Muhammad 24

 

Kwa hivyo anayetaka kujadili kikweli kwa nia ya kuutafuta ukweli na si kufanya inadi tu, basi huyo anaingia katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo;

 

Na ikiwa haki ni yao, wanamjia kwa kut'ii.

An Nur 49

Ukweli unapatikana katika kufuata hadithi zilizosihi isnadi zake, ama hadithi zisizosihi isnadi hata ziwe zimeandikwa na mtu mtukufu wa aina gani, hizo haziwezi kuwa na nuru ya kuongoza kuelekea Peponi, kwani hapana kiumbe mwenye kauli tukufu kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Kwa hivyo hadithi iliyosihi isnadi lazima ifuatwe, ama kauli zisizo na isnadi wala msingi, na zile zisizo na uhakika, lazima ziachwe mara ukweli unapodhihirika.

 

Tutaandika makala haya kwa njia ya majadiliano matulivu baina ya Khalid na Haydar.

 

Kadhia ya Uimamu

 

Khalid: Assalaam alykum wa Rahmatullahi wa barakatuh. karibu ewe

 

Haydar: Wa alaykumu ssalaam ewe ndugu Khalid

 

Khalid: Unaonekana kama kwamba una tatizo?

 

Haydar: Ndiyo, na yareti jambo lenyewe lingekuwa jepesi, lakini inaelekea ni gumu sana na sitoweza kulitatua.

 

Khalid: Ni jambo gani tena hilo ewe Haydar?

 

Haydar: Hii khitilafu iliyopo baina ya Mashia na Masunni kwa kweli inautia dhiki moyo wangu.

 

Khalid: Kweli ndugu yangu, unaonaje tukajadiliana juu ya jambo hili muhimu kwa utulivu ili tuweze kuzifahamu vizuri fikra na itikadi za Mashia na Masunni huenda tukaweza kuzikaribisha fikra zetu.

 

Haydar: Maneno yako ni ya kweli. Jambo hili ni muhimu sana, bora tujadiliane juu ya maudhui haya lakini kwa utulivu kama ulivyosema, huenda tukafanikiwa kuzifanya pande mbili hizi ziwe karibu zaidi.

 

Khalid: Vizuri, unaonaje basi tukajadiliana juu ya zile kadhia muhimu za Madhehebu mawili haya ili huenda tukaweza kupanua fikra zetu juu ya itikadi za Masunni na Mashia kwa nia ya kutaka kuzifanya ziwe karibu zaidi.

 

Haydar: Sawa, jambo hili ni muhimu sana, kwa hivyo tuanze kujadiliana.

 

Khalid: Nakuomba usikasirike tu, kwani itabidi kuzungumza juu ya kadhia zote kwa uwazi bila kuficha. Kwa hivyo ikiwa umekubali basi nakuomba uanze wewe kuzungumza.

 

Haydar: Kwa vile kusudi letu ni kuitafuta haki, mimi sitokasirika. Kwa hivyo tuanze tokea pale Ushia ulipoanza, na ni jambo linalojulikana na kila Muislamu kuwa Umeanza tokea siku ile Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipoanza kuwalingania watu katika Uislamu, isipokuwa baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kufariki dunia Masahaba hawakuupa umuhimu Uimamu wala ule Usia alouacha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Khalid: Umuhimu wa Uimamu umeanza kabla ya hapo unaposema wewe, na zamani kuliko unavyodhania, kwani Maulamaa wa Kishia wameandika ndani ya vitabu vyao kuwa Uimamu ulikuwa ukijulikana na Mitume yote, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Usul al Kafi (437/1) kutoka kwa Abu Hassan kuwa amesema;

Uimamu umeandikwa ndani ya vitabu vya Mitume yote. Hakuletwa Mtume yeyote isipokuwa ameeleza juu ya Utume wa Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na juu ya Usia wa (Uimamu wa)Aliy alayhi ssalaam.

Na baadhi ya maulamaa wamesema kama unavyosema wewe, na kauli yako hii inajulikana sana miongoni mwa watu wa kawaida.

Anasema Al Noubakhty katika kitabu chake kiitwacho Firaq al Shia ukurasa wa 17 kuwa Ushia umeanza pale Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipoanza kuwalingania watu katika Uislamu, na kwamba walikuwa wakiitwa Shiat Ali (wafuasi wa Ali), wakiwemo Miqdad bin Al Aswad na Salman al Farsy na Abu Dhar na Ammar bin Yasir na walikuwa wakijulikana sana kwa kumpenda kwao Ali, na walikuwa daima wakizungumza juu ya Uimamu wake,.

Na Ibni Nadim katika kitabu chake kiitwacho Al Faharasat ukurasa wa 249 ameeleza kuwa Mashia walianza kuonekana baada ya vita vya ngamia Maarakat al Jamal, na kwambaAliy alikuwa akiwaita kuwa ni Mawalii waliotakasika.

 

Haydar: Kutokana na haya tunaelewa kuwa Ushia hauna uhusiano wowote na yule mtu anayejulikana kwa jina la Ibni Sawdaa Abdullahi bin Saba-a na kwamba yote yanayosemwa juu yake mtu huyo ni khurafaat uongo uliozushwa tu na kwamba mtu huyo hakuishi duniani aslan.

 

Khalid: Mwanadamu ni adui wa asichokijua, na haki inajulikana kwa kuifuatilia na kwa kuitafuta kwa nia halisi, kwani mtu huyu ametajwa ndani ya vitabu maarufu vinavyoaminika vya Madhehebu ya Kishia vikiwemo vitabu vya Firaq al Shia kilichoandikwa na Al Noubakhty, na kitabu cha Rijaal al Koshy, na pia katika sharhi ya Nahjul Balagha na vinginevyo.

 

Hader: Unataka nifahamu kutokana na maneno yako kuwa Ushia haukuanza pale Abubakar (Radhiya Llahu anhu) alipouchukuwa kwa nguvu Ukhalifa kutoka kwa Amiri wa Waislam Aliy (Radhiya Llahu anhu).

 

Khalid: Kadhia hii si kama inavyoelezwa na watu wanaofuata matamanio ya nafsi zao, kwani Ukhalifa wa Abubakar Al Siddique (Radhiya Llahu anhu) umepatikana baada ya watu wenye maarifa na hikma kumchagua, na baada ya Masahaba wote kukubaliana kwanza mahali panapoitwa Saqifa, kisha watu wote waliobaki wakafungamana naye msikitini, na hivi ndivyo ilivyokuwa katika Ukhalifa wa Umar na Uthmaan (Radhiya Llahu anhu), na alipouliwa Uthmaan (Radhiya Llahu anhu) watu wote wakazielekeza nyuso zao kwaAliy (Radhiya Llahu anhu) na kumtaka awe Khalifa wao, naAliy (Radhiya Llahu anhu) akawaambia;

Msinichaguwe mimi (bora) mchaguweni mwingine, kwani tumekabiliwa na jambo lenye sura nyingi na rangi nyingi na nyoyo hazisimami wala akili haithibiti. Msiponichaguwa mimi, nitakuwa sawa na yeyote kati yenu, na huenda nikamtii zaidi yule mtakayemchagua kuongoza amri yenu kuliko mtakavyonitii mimi. Bora mimi niwe waziri kuliko kuwa Amiri (Khalifa). Na melezo haya yameandikwa ndani ya kitabu chenu kitukufu Nahjul Balaghah 136

Na haya yanakubaliana pia na alivyoelezea Al Mufiyd katika kitabu kiitwacho Al Irshad, ikiwa ni dalili kuwa hapana ushahidi unaoonesha kuwaAliy (Radhiya Llahu anhu) ndiye aliyechaguliwa kuongoza baada ya kufariki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

 

Haydar: Unataka kuniambia kuwa juu ya umuhimu wa kadhia ya Uimamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hakuacha usia wowote juu ya nani atakayetawala baada ya kufariki kwake?

 

Khalid: Kuwa na Imam atakayewaongoza Waislamu ni jambo muhimu sana kwa umma, lakini tusilifanye jambo hili likawa ndiyo nguzo muhimu sana katika dini na kwamba katika kuiamini nguzo hii tu kutamuingiza mtu Peponi na kwamba daraja yake ni sawa na daraja ya Utume kama alivyoandika Hadi al Taharani katika kitabu kiitwacho Wadai al Nubuwah ukurasa wa 114 aliposema;

Uimamu ni bora kuliko utume kwani daraja yake ni ya tatu aliyomtakasa nayo Ibrahim baada ya utume na Ukhalil.

 

Haydar: Huenda hii ikawa ni rai ya aalim huyu peke yake na maulamaa wengine wa Kishia hawakubaliani na rai yake.

 

Khalid: Riwaya zifuatazo zitalijibu suali lako;

Amesema Al Khashif al Ghitwa-a katika kitabu chake kiitwacho Aslu Shia ukurasa wa 58;

Cheo cha Imam ni cha Mwenyezi Mungu kilicho sawa na Utume.

Ama Khomeni katika kitabu chake kiitwacho Al Hukumat al Islamiah ukurasa wa 52 ameandika;

Hakika Uimamu ni daraja kubwa na tukufu, na Ufalme wenye kutiiwa na kila kitu kilichomo ulimwenguni vikiwemo atoms. Na ni jambo la lazima katika madhehebu yetu kuamini kuwa daraja la Maimamu wetu haifikiwi hata na Malaika walio karibu (na Mwenyezi Mungu) wala Mtume aliyetumwa.

 

Haydar: Maulamaa wetu wameupa umuhimu Uimamu kutokana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alivyoupa umuhimu.

 

Khalid: Kama kweli jambo hilo lina umuhimu huo, kwanini basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akalipuuza na asimchague atakayeushika baada yake? Bali jambo hili halikutajwa kabisa ndani ya Qurani ambayo Mwenyezi Mungu ameihifadhi kutokana na kubadilishwa na kugeuzwa. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hakuwahi kulitaja kwa ufasaha hata pale alipokuwa akiisalimisha roho yake kwa Mola wake, wala hata wakati ule alipowakusanya Waislamu wote katika Hija yake ya kuaga alipowahutubia akasema;

Huenda sitokuoneni tena baada ya mwaka wenu huu.

Ile ilikuwa ni fursa isiyoweza kulipika wala kurudi tena iliyoweza kuwakusanya Waislamu kutoka pembe zote za Bara ya Arabuni ya kuwaeleza juu ya Usia wa Imamu atakayetawala baada yake.

Kwa hivyo jambo hili halikuwa na umuhimu ule mnaoupa nyinyi hata muifanye kuwa ni nguzo mojawapo muhimu sana ya dini.na kwamba asiyeiamini anakuwa kafiri.

Ama Khomeini yeye anayo tafsiri nyingine kinyume na wanavyosema maulaaa hao juu ya sababu iliyomfanya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) asizungumie jambo hili la uimamu.

 

Haydar: Tafsiri gani nyingine tena?

 

Khalid: Anasema Khomeni katika kitabu chake kiitwacho Kashf al Asraar (kuzifichua siri) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliificha siri hii ya Uimamu katika siku za mwanzo za daawa yake alipokuwa Makka, akihofia kuwaambia watu jambo kubwa kama hili mpaka Mwenyezi Mungu alipomlazimisha kufanya hivyo pale alipomwambia;

Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hukufanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu wanaokufuru.

Al Maidah 67

Kisha akamuamrisha tena katika kauli yake Subhanahu wa Taala;

Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni kuzirudisha amana kwa wenywe (wanozistahiki)

An Nisaa - 58

Anasema Imam Khomeni katika kitabu chake kiitwcho Al Hukumah al Islamiyah ukurasa wa 81 kuwa;

Mwenyezi Mungu hapa anamuamrisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) airudishe amana, yaani aurudishe (Uimamu) Uongozi kwa wenyewe (wanaostahiki), yaani amrudushie Amiri l Muuminin alayhi ssalaam (Ali bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu)) na yeye amrudishie atakayemfuata nk..

Na maneno haya maana yake ni kuwaAliy (Radhiya Llahu anhu) ndiye mwenye haki na kwamba Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) anatakiwa amrudishieAliy amana yake hiyo, na kama mnavyoona kuwa tafsiri hii ni ya kupotosha na haina dalili yoyote ndani yake. Hii ukijumuisha pia kulifasiri kwake neno Amana kuwa maana yake Uimamu Imam Khomeni hapa anabadilisha na kuyapotosha maneno ya Mwenyezi Mungu, na anaonesha ujinga wake wa kutojuwa sababu za kuteremshwa kwa aya hizi.

 

Haydar: Lakini Khalifa wa mwanzo alikwenda kinyume na kawaida ya ushauriano (Shura), kwani hakushauriana na Waislamu wenzake pale alipomchagua Khalifa atakayetawala baada yake na hili ni jambo la fardhi.

 

Khalid: Hakuna mtu aliyefaridhisha jambo hili, na kwa yeyote atakayefuatilia mwenendo wa Al Siddique (Radhiya Llahu anhu) atajua kwa uhakika kuwa alikuwa mtu mwenye kuchunga maslahi ya Umma huu na akiutakia kila la kheri. Kwa hivyo jambo hili halikuwa sudfa wala kosa, kwa sababu Waislamu walimtaka Abubakar (Radhiya Llahu anhu) atoe ushauri wake juu ya nani anayemdhania kuwa atafaa kutawala baada yake, ndipo alipomtaja Umar (Radhiya Llahu anhu) na kwa mwenye kufuata mwenendo wa Umar (Radhiya Llahu anhu) pamoja na Masahaba wakati wa ukhalifa wake ataiona hekima kubwa aliyokuwa nayo Abubakar pale alipomtaja Umar awe Khalifa baada yake, lakini mtu afanye nini ikiwa chuki na bughudha dhidi ya Makhalifa hawa wawili zishajazwa ndani ya nyoyo za baadhi ya watu?

 

Haydar: Zile kauli zinazosema kuwa Imamu ni mtu aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu na kwamba uimamu umekamatana na utume, unataka kuniambia kuwa kauli hizo hazina dalili zilizo thabiti?

 

Khalid: Suali hili ingefaa uwaulize wale walioifanya kadhia hii ya Uimamu kuwa ni nguzo ya dini, kisha wakaibunia milango yake na mambo mengi, kisha wakauleta uzushi wa mrithi wa Faqih na mabalozi wake, kisha vikatungwa vitabu visivyo na idadi kuhusu jambo hili, yote haya kwa ajili ya kuilazimisha itikadi hii. Kutokana na yote haya ni vizuri kama ungewataka hao waliouleta uzushi huu wakupe dalili kutoka katika Qurani au kutoka katika mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)( juu ya itikadi hii.

 

Haydar: Utanisamehe kidogo, maana sijauelewa vizuri bado msimamo wako kuhusu Uimamu. Yaani unataka kuniambia kuwa hapana nassi yoyote katika Qurani wala katika mafundisho ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) juu ya Uimamu waAliy na maimamu waliokuja baada yake?

 

Khalid: Tukichukulia kimjadala tu kwamba Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimtaja Aliy (Radhiya Llahu anhu) kwa jina kuwa ndiye atakayekuwa Khalifa baada yake, na kwamba Al Siddique aliuchukuwa kwa nguvu ukhalifa huo, huoni wewe mwenyewe kuwa wakati wa ukhalifa wa Abubakar na Umar dola ya Kiislamu ilipata mafanikio mengi sana, utulivu ulipatikana ndani yake, na hitilafu iliondoka baina ya Waislamu wakaweza kuziteka nchi nyingi sana za kikafiri? Haya yote yalipatikana wakati wa ukhalifa wa Abubakar na Umar na sehemu kubwa ya Ukhalifa wa Uthmaan (Radhiyallahu anhum ajmaiyn).

Hebu niambie ewe ndugu Haydar wangelikuwa kweli watu hawa wamekwenda kinyume na nguzo muhimu sana ya dini kupita nguzo zote kama mnavyosema, vipi basi Mwenyezi Mungu angewapa mafanikio kama haya katika kuzifungua nchi mbali mbali wao pamoja na watoto wao. Isitoshe, wakati wote huo hapakuwa hata mtu mmoja aliyekuwa akizungumza juu ya Uimamu au juu ya kunyanganywaAliy (Radhiya Llahu anhu) ukhalifa wake.

 

Haydar: Huenda ikawa Amiril Muuminin alayhi ssalaam hakulalamika kwa sababu ya kuona kwake mbali, alikuwa hataki kuleta mfarakano baina ya Waislamu.

 

Khalid: Tuchukulie kuwa mambo yalikuwa kama unavyosema, lakini baada ya kuuliwa Aliy (Radhiya Llahu anhu) na ukhalifa ulpoangukia kwa Al Hassan (Radhiya Llahu anhu) tulimuona akimkabidhi ukhalifa huo Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu), tena kwa hiari yake. Sasa je, inajuzu kwa mtu asiyetenda makosa (Maasum) kuiangusha nguzo hii muhimu sana ya Uimamu ambayo ni tukufu kupita zote kama mnavyosema, na kumpa mtu duni yake kwa daraja. Tena ampe kwa hiari yake bila kulazimishwa baada ya kupita miezi sita tu tokea alipouliwa baba yake? Isitoshe, tunasoma katika vitabu vya historia kuwa Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu) alitawala kwa muda wa kiasi cha miaka ishirini huku Waislamu wakipata ushindi baada ya ushindi dhidi ya majeshi ya makafiri kupitia miaka yote iliyopita, na kwa ajili hiyo dini ya Mwenyezi Mungu ikazidi kusambaa na kuenea kila pembe ya ulimwengu, na hili si jambo la kushangaza kwa sababu Mu'awiyah na Masahaba wenzake (Radhiya llahu anhum) walioifanya kazi hiyo wanatoka katika madrasa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

 

Kuwakufurisha Waislamu

Haydar: Tujadiliane ewe ndugu mpenzi kikweli na bila kuficha chochote juu ya kadhiya muhimu na isiyostahamilika katika jamii yoyote ya Kiislamu. Naomba kifua chako kiwe laini kusikiliza.

 

Khalid: Hatukuamua kuzungumza isipokuwa kwa sababu ya kunasihiana na kuijuwa haki ilipo, na pia kwa ajili ya kujiepusha na ukireketwa.

 

Haydar: Hivi ndivyo ninavyokujuwa. Kwa hivyo nataka unielezee juu ya sababu ya kupenda kuwakufurisha wenzenu na kuwavurumishia tuhuma za ukafiri ndugu zenu wanaoswali kama nyinyi, juu ya kuwa msingi wa mafundisho ya dini yetu ni kumdhania Muislamu mwenzio mema, na kumtafutia udhuru kwa yale aliyojitahidi katika kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu.

 

Khaled: Unajuwa ewe ndugu Haydar kuwa hapana dhulma kuliko kumshrikisha Mwenyezi Mungu? Na hapana jema kuliko 'Tawhiyd' (kumpwekesha Mwenyezi Mungu)? Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipokuwa Makka alikuwa akiwalingania watu katika kadhia moja tu, nayo ni:

} ( : 65)

Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?

Al Aaraf 65

Wakati wote huo hakuwa akiwafundisha namna ya kutawadha wala kutoa Zaka wa Kuhiji nk. Kwa hivyo wito wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hapo mwanzo ulikuwa kuithibitisha itikadi ya Tawhiyd vifuani mwa Masahaba, na kila kitu kikaja baada yake.

 

Haydar: Haya yanajulikana na hayana shaka yoyote ndani yake, lakini kwa nini mnawachukiza watu kwa kuwakufurisha mbele ya Waislamu wenzao?

 

Khalid: Kutokana na niliyosoma ndani ya vitabu, nimeona kuwa maulamaa wengi wa Kishia ndiyo watumiaji wakubwa wa neno Kafir wakiwakufurisha Waislamu wenzao pamoja na maulamaa wao, mfano Hussayn Annajafiy katika kitabu chake Jawhar al Kalaam 6/62 aliposema: "Na kila mwenye kuwapinga wenye haki (Shia) basi huyo ni kafir na hapana hitilafu yoyote juu ya haya."

 

Haydar: Tuziache kauli kama hizi na tuiangalie sira ya Al Mustafaa (Swallah Llahu alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya jambo hili.

 

Khalid: Mwenye kufuatilia sira ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na namna alivyowalea Masahaba wake (Radhiya Llahu anhum), ataona kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) alikuwa akiwatanabahisha na kuwatahadharisha kwa haraka sana kila anapoona jambo lolote linalofanana na shirki kwa ajili ya kuilinda Tawhiyd na kujiepusha na ushirikina.

Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala Anasema:

} ( : 48)

"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa."

Annisaa 48

 

Kwa hivyo dhambi yoyote ni nyepesi, kinyume na shirki.

 

Haydar: Tukubaliane kwanza juu ya kusudi la neno Shirk kabla ya kulizungumzia.

 

Khalid: Neno Shirk kama inavyojulikana katika lugha ya kiarabu linatokana na kushiriki, yaani kwa maana ya kumjaalia mwanadamu kama ni mwenzi wa Allah akafanywa mwanadamu huyo kuwa anao uwezo ama wote au baadhi ya uwezo Alionao Mwenyezi Mungu. Sheria imetaja mifano mingi mfano wa watu wa Makka walivyokuwa wakiyajaalia masanamu kuwa yanao uwezo wa aina hiyo. Walikuwa wakiyaomba kama wanavyomuomba Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo shirki ni kumjaalia mwingine kwa kitendo au kutamka maneno au kuwa na itikadi kuwa anao uwezo alionao Allah, au kumfananisha mwingine na Allah. Kwa hivyo mtu akiapa kwa mwingine asiyekuwa Allah anakuwa keshafanya kitendo cha shirki kwa kauli yake hiyo, na akichinja kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allah anakuwa kesha fanya kitendo cha shirki. Na ikiwa ataamini kuwa aliyeapa kwa jina lake au aliyechinja kwa ajili yake kuwa anao uwezo wa kunufanisha au kudhuru kinyume na Allah, basi mtu huyo anakuwa kesha toka katika mila ya Kiislamu na kuingia katika mila ya Kufru.

Akiwa mtu huyo ni jaahil asiyejuwa anachofanya, basi inapasa kumtahadharisha na kumfundisha kuwa jambo hilo halijuzu kutendwa na kwamba ni haramu, hata kama alikusudia kutabaruk tu, kwa sababu Dua na Tawafu na Kiapo na Kuchinja na Swala na Hija na mengine ya mfano huo katika mambo ya ibada hayajuzu kuelekezewa mwengine isipokuwa Allah peke Yake, na haya ndiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliyokuwa akiwafundisha na kuwakataza watu wa Makka kwa muda wote ule.

 

Haydar: Unayosema ni katika mambo yanayojulikana na maulamaa wote wa Kishia. Kipi kipya katika haya uliyoyasema?

 

Khaled: Niliyoyasema ni mepya katika masikio ya maulamaa wa Kishia, bali wapo miongoni mwao waliohusisha ushirikina na dini wakaupa ushirikina huo jina jipya, kama alivyosema Yusuf Al Baharani katika kitabu chake Al Hadaaiq An Naadhirah (18/153): "Pana tofauti gani baina ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuwakufuru maimamu alayhimussalaam baada ya kuthibiti kuwa Uimamu ni msingi wa dini?"

 

Haydar: Hizi ni miongoni mwa kauli chache zisizokubalika kutoka kwa maulamaa wa dini na haikubaliki kuwa ni hoja dhidi yetu, kwa sababu hatujapata kumuona yeyote kati ya maulaa wetu asiyeamrisha juu ya Tawhiyd na kukataza kumshirikisha Mwenyezi Mungu, bali jambo hili hawalifanyii mchezo.

 

Khaled: Al Khomeini kwa mfano; aliuliza suali katika kitabu chake Kashf al asraar ukurasa wa 65, kisha akalijibu mwenyewe kwa ajili ya kutubainishia itikadi yake katika jambo hili aliposema: "Hakika jawabu ya suali hili linafahamika zaidi kutokana na maana ya shirki, na mlikwisha juwa kuwa shirki ni kumshirikisha Allah na mwengine au kumuabudu mwingine kama anavyoabudiwa Allah, au kumuomba mwingine kama kwamba yeye ndiye Allah au mshirka wake, au anao uwezo wa kuathiri. Bali yote hayo hayahesabiwi kuwa ni shirki au kufru ikiwa mwenye kuomba anaamini kuwa Allah anao uwezo wa kujibu ombi kupitia kwa waliopoteza maisha yao kwa ajili ya dini Yake, na walipoteza roho zao kwa ajili Yake Allahu Taala." Unajuwa ndugu yangu Haydar maneno haya yamefungua mlango upi?

 

Haydar: Maneno ya Imam Mwenyezi Mungu amtukuze, yanafahamika vizuri kwangu. Kwani wewe unataka kusema nini?

 

Khaled: Nataka kukufahamisha kuwa Khomeini ametamka jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) hajapata kulisema, wala wale waliokuja baada yake hawajapata kulisema katika kutujulisha maana ya Shirki, na maneno haya ya Khomeini yamefungua milango ifuatayo:

1.      Kwamba Muislamu anaweza kuomba shifaa kwa kutumia uchawi au kuvaa hirizi kwa kujikinga na maradhi. (Soma kitabu cha Bihaar al Anwaar (94/193)

2.      Kuomba istikhara kwa njia ya lozi au jiwe litakaloweza kumsaidia mwanadamu. Soma kitabu cha Attahdhiyb (1/306) na Furu'a al Kafi (1/131)

3.      Itikadi kuwa Maimamu wana haki ya kufanya watakavyo juu ya ardhi na kwamba wao ndio miungu juu ya ardhi. Soma Bihaar al Anwaar Uk. 95

4.      Itikadi kuwa Maimamu wanao uwezo wa kuamua katika mambo ya kidunia na mambo ya hali ya hewa. Soma kitabu cha Al Ikhtiswaas cha Al Mufiyd Uk. 327 na Bihaar al Anwaar (27/33).

5.      Itikadi kuwa Imam anao uwezo wa kufufua maiti makaburini mwao. Soma kitabu cha Usuwl al Kaafi (1/457) na Baswaair Adarajaat (76).

Kwa hivyo itikadi kama hizi unadhani zinamuongoza mtu katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu au katika kumshirikisha? Hii ni shirki ambayo hata makafiri wa Makka hawakuwa wakiikubali.

 

Haydar: Nia ndiyo muhimu katika matendo yoyote katika kukubaliwa na kukataliwa kwa matendo, na haya ndiyo aliyosema Imam Khomeini.

 

Khaled: Nitazidi kuwadhihisha; katika kitabu chake Al Khomeini kiitawacho Kashf al Asraar Uk. 42 amesema: "Baada ya kubainika kuwa shirki ni kumuomba asiyekuwa Mola wa ulimwengu kwa kuitakidi kuwa yeye ndiye Allah! Kwa hivyo yaliyo duni ya haya hayahesabiwi kuwa ni shirki. Na hapana tofauti baina ya aliye hai na aliyekufa. Kwa mfano kuliomba jiwe siyo katika shirki juu ya kuwa kitendo hicho ni baatil." Na Mwenyezi Mungu Ametujulisha kuwa watu wa Makka hawakuwa wakiyaomba masanamu wakiitakidi kuwa hiyo ni miungu, kama alivyosema Khomeini, bali wao waliyafanya masanamu hayo kuwa ni walinzi tu wenye kuwakaribisha karibu na Allah. Mwenyezi Mungu Anasema:

} ( : 3)

Na wale wanao wafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu kumkaribia Mwenyezi Mungu.

Az Zumar 3

 

Unadhani walipofanya vile, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwaacha waendelee tu kwa sababu hawakuwa wakiitakidi kuwa ni miungu? Angelifanya hivyo, basi ingewezekana, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) aliwakataza na akapambana nao na akawabainishia kuwa hii ndiyo shirki kubwa.

 

Haydar: Unataka kuniambia kuwa Imamu, Mwenyezi Mungu amtukuze hakuwa akielewa maana ya shiriki, au alikuwa akiwaruhusu watu wa kawaida kufanya hivyo?

 

Khaled: Mimi siye nitakayetoa hukmu katika hilo, bali Mwenyezi Mungu ametupa akili na vifua vinavyoweza kupambanua baina ya haki na upotovu.

Kwa hivyo inatubidi tufahamu kuwa Maimamu Mwenyezi Mungu awarehemu walikuwa ni watu wema, tunawapenda kwa sababu ya mapenzi yetu kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kwa ajili wao wanafuata mafundisho yake. Na hatuwapi isipokuwa daraja wanayoistahiki. Na tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu katika kuwanyanyua na kuwageuza miungu kama alivyosema Al Koshy Uk. 224

Amesema Jaafar bin Muhammad: "Wallahi sisi si chochote isipokuwa ni watumwa wa Mwenyezi Mungu aliyetuumbana akatuchaguwa, na wala hatuna uwezo wa kudhuru wala kunufaisha. Tukipata rehma, basi kwa Rehman Zake na tukiadhibiwa, basi kwa dhambi zetu. Wallahi hatuna hoja yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu, wala hatuna dhima, na sisi tutakufa na tutazikwa na tutafufuliwa na kusimamishwa na kuulizwa. Ole wao, wanana nini Mwenyezi Mungu awalani hawa, walimuudhi Mwenyezi Mungu wakamuudhi Mtume wake katika kaburi lake, na Amiri wa Waislamu na Fatima na Al Hassan na Al Hussayn na Aliy bin Al Hussayn na Muhammad bin Aliy Swalawaatu Llahu alayhim. Nashuhudia mbele yenu kuwa mimi ni mja ninayetokana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na sina dhima mbele ya Mwenyezi Mungu, nikimtii atanirehemu na nikimuasi ataniadhibu adhabu kali."

 

Kukingwa

 

Khaled: Bado ningali nastaajabu kwa wale wenye kuzifasiri aya za Qurani kinyume na maana yake iliyo sahihi, na wanatoa ushahidi wa hadithi dhaifu katika kuthibitisha jambo lisilokuwemo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu.

 

Haydar: Unaweza kunipigia mfano katika haya unayoyasema?

 

Khaled: Kauli Yake Mwenyezi Mungu aliposema:

} ( : 33)

Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba (ya Mtume), na kukusafisheni baarabara."

Al Ahzaab 33

Iwapi hapa dalili ya kuthibitisha kuwa Maimamu wamekingwa?

 

 

Haydar: Dalili hapa ni kwa kuifahamu maana ya aya hii na siyo kwa yaliyoandikwa. Kwa sababu atakayemwakilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) lazima awe aliyekingwa asije akaharibu katika kuifikisha risala. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyomkinga Mtume wake (Swalla Llahu alayhi wa sallam), katika kuifikisha risala, kwa hivyo pia Maimamu wakakingwa kwa sababu wao ndio waliousiwa baada yake Alayhi Swalaat wa ssalaam.

 

Khaled: Kukingwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni wajibu kwa ajili ya kuifikisha risala, kutokana na kauli Yake Subhanahu wa Taala Aliposema:

} ( : 3-4)

Wala hasemi kwa maneno ya nafsi yake. Hayakuwa haya (anayoyasema) ila ni Wahyi (ufunuo) uliofjnuliwa (kwake).

An Najm 3-3

 

Sasa ni nani aliyewajibisha kwa watu wengine maalum baada ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)? Kama ipo habari yoyote juu ya jambo hilo, basi lazima iwe sahihi na mutawaatir iliyopokewa kwa njia nyingi sahihi na yenye kueleweka na kufahamika na iliyoenea baina ya watu. Kwa kukosekana hayo, hiyo itikadi ya kukingwa haina dalili yoyote.

 

Haydar: Lakini lazima ieleweke kuwa aya hii imeteremshwa hasa kwa ajili ya watu wa nyumba ya Aliy (Alayhissalaam) ambao ndio waliousiwa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) baada yake.

 

 

Khaled: Kwanza lazima ieleweke kuwa aya hii haikuteremshwa kwa ajili ya watu wa nyumba ya Aliy, na dalili ni kwamba Allah alipoiteremsha aya hii aliiteremsha pamoja na aya nyingine zikiwasifia wake wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), kisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akainuka na kumwita Fatima na Aliy na Al Hassan na Al Hussayn (Radhiya Llahu anhum) akawafunika na shuka yake, kisha akaisoma tena aya hii ili iwaingize nao pia ndani yake na ili nao wapate baraka za aya hii pamoja na wake wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Ikiwa kweli aya hii inamaanisha kutwahirika kwao, kwanini basi Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) airudie. Kwa nini airudie tena ile dua wakati kitendo kishakamilika kwa kutakaswa kwa amri ya Allah

 

Haydar: Lakini aya ina dalili mbili za kukingwa kwa Maimamu. Ya kwanza ni kutumiwa mfumo wa maneno ya wingi wa wanaume Aliposema: badala ya kutumia wingi wa wanawake. Na ya pili ni maana ya neno 'Al Rij's' uchafu, na maana yake ni kuwakinga na uchafu na maovu. Ikafahamika kuwa aya hii ni kwa ajili ya watu wa nyumba ya Aliy peke yao.

 

 

Khaled: Sababu ya kutumika kwa mfumo wa maneno ya wingi wa wanaume badala ya kutumiwa ya wanawake katika neno ni kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) mwenyewe pia yumo katika waliotakaswa katika aya hii, kwa sababu yeye ndiye mkubwa wa ukoo, na siku zote anayehutubiwa ni mkuu wa ukoo ambaye daraja yake katika nyumba ni kubwa kupita wake zake, ili iweze kuwaingiza wote kwa pamoja.

 

Haidar: Mwenyezi Mungu Anasema:

{ } ( : 59)

59. Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.

Annisaa 59

Na kwa vile inajulikana kuwa Uimamu baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ni wa Aliy (Radhiya Llahu anhu) ikaamrishwa kuwa atiiwe kama anavyotiiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam)

 

Khaled: Muislamu haifasiri Qurani kwa rai yake, bali anaziangalia kauli za maulamaa mbali mbali, kwa sababu maana ya aya hiyo iko wazi kabisa. Na kumtii Mwenyezi Mungu kunatofautiana na kumtii Mtume wake (Swallah Llahu alayhi wa sallam). Na wenye madaraka kuwatii kwao ni kutokana na kutimiza kwao yale waliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam), na hawana twaa ya aina nyingine. Ama kuhusu kuchaguliwa Aliy (Radhiya Llahu anhu) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) kuwa Amiri wa Waislamu, haya ni maudhui mengine ambayo tutayazungumzia baadaye. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ameusia juu ya watu wa nyumba yake aliposema: "Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu." Na maana yake ni kuwa 'Muzijuwe haki zao.' Na Masahaba waliwahesimu kwa heshima wanayoisahiki kwa kuwapenda na kuwaheshimu.

Haidar: lakini kwa nini mnakuwa wakali hivi mnapozungumza juu ya kadhia ya yule anayehesabiwa kuwa ni mwakilishi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu alayhi wa sallam) ambaye tumeusiwa juu yake.

Khaled: Utanisameh kama unahisi katika mazungumzo yangu pana ukali ndani yake, kwani sisi ni watu wenye kuitafuta haki Inshaallah, na ujuwe ewe ndugu Haidar, yareti mambo haya yangelimalizikia katika kuchaguliwa na kuusiwa, bali mambo yamekuwa hata akawa anapewa daraja ya Mitume, ikiwa si daraja kubwa kupita hizo.

Kumlilia Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)

 

Khalid: Nakuona rangi yako imebadilika tokea uliporudi kutoka katika Al Husayn iat (kupiga jauseni)?

Haydar: Yeyote atakayekaa na kutafakari akaukumbuka msiba wa Imam Al Husayn alayhi ssalaam lazima moyo wake utajaa huzuni.

Khalid: Lakini karne nyingi sana zishapita tokea msiba huu ulipotokea, kwanini basi nyinyi mumo tu bado mnaendelea kuufanyia kumbukumbu msiba huu kila mwaka?

Haydar: Si haramu mtu kuhuzunika wala kulia, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alitokwa na machozi alipofiwa na mwanawe, na alilia pia siku ile Hamza (Radhiya Llahu anhu) alipouliwa na alitokwa na machozi pale baadhi ya Masahaba walipofariki dunia. Ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alihuzunika kwa misiba hiyo unadhani upo msiba mkubwa duniani ambao watu wanapaswa zaidi kulia kwa ajili yake kuliko msiba wa Abu Abdullah alayhissalaam (Imam Al Husayn )?

Khalid: Katika Uislamu, huzuni na kilio kwa ajili ya misiba si jambo linalohukumiwa na hisia peke yake, kwani jambo hili limewekewa sheria maalum na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Haydar: Namna gani?

Khalid: Huzuni na kutoa pole kwa mtu aliye karibu ni siku tatu, na mke anayo eda maalum inayojulikana, ama kuhusu kulia, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amekwishatujulisha namna yake kutokana na kauli yake (Swalla Llahu alayhi wa sallam) siku ile aliyofariki mwanawe Ibrahim aliposema;

Kwa hakika moyo unahuzunika, na jicho linatokwa na machozi lakini hatusemi ila yale tu anayoridhika nayo Mwenyezi Mungu, na sisi kutokana na kufarikiana nawe ewe Ibrahim tunahuzunika.

Hatukupata kusikia hata siku moja au kusoma kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alirudia tena kulia au kuhuzunika kutokana na kifo cha mwanawe huyo au kutokana na kifo cha ammi yake aliyekuwa akimsaidia au kutokana na mke wake Bi Khadija (Radhiya Llahu anhu) au juu ya Hamza wala hata juu ya yeyote miongoni mwa Masahaba.

Haydar: Kwa nini unakasirika mimi ninapomlilia Al Husayn alayhi ssalaam?

Khalid: Kwanza siku ya Ashura inajulikana kuwa ni siku ambayo ndani yake Mwenyezi Mungu alimuokoa Nabii Musa (AS) kutokana na Firauni, na kwa ajili hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akaamrisha watu wafunge siku hiyo kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, na akaongeza kuwataka watu wafunge siku ya tisa pia kwa ajili ya kwenda kinyume na namna Mayahudi walivyokuwa wakifunga.

Pili - Mwenyezi Mungu amekadiria siku kama hiyo auliwe Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu), lakini hapana hukmu yoyote ya kisheria inayozungumza juu ya kuitukuza au kuifanyia kumbukumbu siku hiyo kila mwaka kutokana na kifo hicho, na mwanadamu anakipokea kwa moyo wa imani kile alichokadiriwa na Mwenyezi Mungu. Sasa nani aliyetufundisha sisi tuirudie huzuni ya kuuliwa kwa Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kila mwaka inapofika siku kama hii?

Wakati huo huo kufunga siku hii ya Ashura kumethibiti kwa dalilim tena ndani ya vitabu vyote vya Ahlu Sunnah takriban na pia imethibiti katika vitabu vya madhehebu ya Kishia.

Katika kitabu cha madhehebu ya Kishia kiitwacho Al Istibsaar kilichoandikwa na Al Tuusi, na huyu Al Tuusi anaitwa Baba wa taifa la kishia.

Imethibiti katika kitabu chake cha Al Istibsaar juzuu ya 2 ukurasa wa 134 na katika kitabu kiitwacho Wasail al Shia, kutoka kwa Abi Abdullah alayhi ssalaam kutoka kwa baba yake kuwaAliy alayhi ssalaam amesema;

Fungeni siku ya Ashura siku ya tisa na siku ya kumi kwani funga hiyo inafuta madhambi ya mwaka mzima.

Rudi juu

HADITHI NYINGINE

Kutoka kwa Abal Hassan (AS) kuwa amesema;

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alifunga siku ya Ashura.

 

HADITHI NYINGINE

Kutoka kwa Jaafar kutoka kwa babake alayhima ssalaam kuwa amesema;

Funga ya Ashura inafuta dhambi za mwaka mzima.

 

Huoni basi namna gani Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alivyokuwa akiitilia mkazo funga hii na pia ImamAliy (Radhiya Llahu anhu) na Jaafar (Radhiya Llahu anhu). Wote hao wanatilia mkazo funga hiyo? Na hii ni dalili kutoka katika vitabu vyenu wenyewe kuwa funga hii ya Ashura ni katika mafundisho aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Haydar: Kweni nani aliyekuambia kuwa Mashia hawaifungi siku hii na kwamba hawafanyi ibada mbali mbali za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu?

Khalid: Kufunga kuna wakati wake maalum, nao ni kutoka pale alfajiri inapoingia hadi jua linapozama pamoja na nia. Hahesabiwi mtu kuwa amefunga ikiwa atakaa na njaa mpaka wakati wa adhuhuri kisha ale vyakula vizuri vizuri huku akisema;

Siku ya leo mimi nina huzuni.

Haydar: Kwa nini unashadidia katika kulikataza jambo hili wakati nina hakika kuwa halimpeleki mtu kufanya maasi?

Khalid: Mambo mnayoyatenda siku kama hii ambayo ni kinyume na mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hawezi kuyakubali mtu yeyote mwenye akili timamu, yakiwemo yafuatayo;

1.      Kulia na kuomboleza.

2.      Kuchana nguo na kujipiga makofi ya uso.

3.      Kujipiga vifua kwa minyororo na visu mpaka damu kumwagika.

4.      Kauli za kumsifia Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) zinazopindukia mipaka.

5.      Kuwalaani na kuwatukana Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

6.      Kuibatilisha amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ya kufunga siku hii ya Ashura na kuwakataza watu wasifunge.

7.      Kuchinja na kupika vyakula na kugawa kwa jina la Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu).

8.      Kuzika mbegu ya chuki ndani ya nyoyo za watu wa kawaida, jambo linalosababisha mfarakano baina ya umma.

9.      Kuharimisha kufunga ndoa katika siku hii na kuharimisha kuingiliana baina ya mtu na mkewe, na mengi mengineyo yenye mfano huu mnayofanya katika siku kama hii.

Haydar: Lakini dhulma alofanyiwa Al Husayn alayhi ssalaam inaumiza sana moyo na kuujaza huzuni kubwa sana, na Waislamu hawajapata kupambana na msiba mkubwa kuliko huu.

Khalid: Msiba mkubwa kuliko yote uliowasibu Waislamu ni kuondokewa na Mtume wao (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kama ilivyoelezwa na Addarimiy na Imam Malik kuwa Ibni Abbas (Radhiya Llahu anhu) amesema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alimwambia;

Atakayekutwa na msiba, basi aukumbuke msiba wangu (wa kufa kwangu), kwani huo ni msiba mkubwa kupita (misiba) yote.

Haydar: Naogopa nisije nikakufahamu vibaya kama kwamba kusudi lako ni kuwa Msiba wa Al Husayn alayhi ssalaam hauna athari yoyote ile ndani ya nafsi zetu.

Khalid: Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni kipenzi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na bwana wa vijana wa Peponi, aliuliwa kwa dhulma akiwa shahid na Inshaallah mahali pake ni katika Firdaws al Aala. Subhanallah! kwa hili sisi hatukhitilafiani, na si msingi wa hitilafu baina yetu, isipokuwa hitilafu yetu ni kuwa; Nani aliyetoa amri hii au fatwa hii, au nani aliyejuzisha kufanya yale maovu yanayotendeka katika siku kama hii ya Ashura, mambo yaliyokatazwa hata katika vitabu vya maulamaa wenu wa Kishia.

Katika kitabu kiitwacho Al Bihar, 103/82 anasema Al Majlisi;

Kuomboleza ni katika matendo ya Ujahilia.

Na Ibni Babaweh al Qummy naye pia katika kitabu chake kiitwacho Man la yahadhuruhul Faqiyh (271/2) anasema;

Katika maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) yenye miujiza ndani yake ambayo hakupata kutamka mwingine kabla yake ni kuwa; Kuomboleza ni katika matendo ya Ujahilia.

Na akaongeza kusema kuwa; Anapata dhambi hata yule aliyehudhuria na asifanye matendo hayo.

Haydar: Nitapata dhambi ikiwa nitahudhuria hata bila kupiga vifua wala kulia kwa sauti kubwa?

Khalid: Ndiyo, ukihudhuria katika vikao kama hivi kisha usiwanasihi watu wala kuwaongoza katika mema, bila shaka unapata dhambi. Hata Al Hur al Aamily katika kitabu chake kiitwacho Wasail al Shia (915/2) amesema;

Kutoka kwa Imam Al Sadiq kutoka kwa baba yake alayhimu ssalaam kuwa amesema;

Amekataza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kupiga kelele katika misiba na amekataza kuomboleza na kusikiliza (maombolezo).

Vipi Muislamu anakubali kujifananisha na watu wa zama za Ujahilia na kuwaiga matendo yao na akaacha mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam)?

Hamuoni kuwa katika mwahali mwa maombolezo ya namna hii hakuzidishi imani yoyote katika nyoyo za watu? Bali kinyume chake vikao hivi vinazidisha chuki na mfarakano baina ya Waisalmu kila mwaka. Na tatizo kubwa zaidi ni kuwa kila jeraha hilo linapoanza kutaka kupona, unaingia mwaka mwingine na watu huanza tena kukusanyika na kulichoma kisu kovu lake na kusababisha kufunguka tena kwa jeraha hilo.

Kwa nini basi hamuyaachi hayo mkafuata uongofu aliokuja nao Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) badala ya kufuata wale wanaotaka kulizamisha jahazi hili na kuwazamisha umma huu?

Rudi juu

Ziara ya kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)

 

Khalid: Huoni basi ewe ndugu yangu Haydar kuwa kuiadhimisha siku ya kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kunazalisha fikra za hatari ambazo hawezi kuzikubali Muislam yeyote mwenye akilia timamu?

Haydar: Bora ungenifafanulia zaidi maneno yako haya.

Khalid: Kuwa na nia nzuri tu peke yake na kupenda mambo ya kheri bila kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu kunaweza kumpeleka mtu katika njia mbaya akajikuta anakwenda kwa kupepesuka bila ya nuru ya kumuongoza. Na hivi ndivyo walivyofanya baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi, wakamnyanyua Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) pamoja na kaburi lake katika daraja kubwa kuliko aliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Haydar: Maneno yako haya ni makali, na mimi sitokubali mpaka unibainishie kwanza, ama sivyo nitakutuhumu kuwa umewatukana maulamaa wetu.

Khalid: Nilikuwa nikiwasikia sana watu wa madhehebu ya Sunni wakisema kuwa; Mashia wanapolizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) wanalitukuza sana na wanalipa daraja kubwa sana kupita hata daraja na mapenzi wanayoipa nyumba ya Mwenyezi Mungu Al Kaaba, na wanaitakidi kuwa penye kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) pana baraka nyingi sana zisizopatikana mahali pengine popote duniani. Na mimi nilikuwa nikidhani Masunni walikuwa wanazidisha chumvi katika maneno yao hayo ya kuwatuhumu Mashia, na kwa ajili hiyo nikaamua kuutafuta ukweli kwa kufanya utafiti wangu mwenyewe. Ndipo nilipogundua kuwa yale maneno yaliyokuwa yakisemwa na Masunni juu ya Mashia juu ya kulitukuza kaburi la Al Husayn ni machache sana ukilinganisha na mengi niliyoweza kuyajua.

Haydar: Huu wallahi ni uongo unaowasingizia watu wanaoikubali shahada ya Laa ilaaha illa Llah Muhammadan Rasulu Llah.

Khalid: Imeandikwa katika kitabu kiitwacho Furu-ul Kafi, (1/324) na katika kitabu Thawabul aamal cha Ibni Babaweyh ukursa wa 56 na katika Kamil al Ziarat cha Ibni Kooloweyh (161) na Wasail al Shia (348/10) kuwa;

Ziara ya kaburi la Al Husayn ni sawa na Hija ishirini pamoja na Umrah (ishirini).

Na imeandikwa pia katika Tahdhiyb al Ahkam kilichoandikwa na Al Tusiy (16/2) na Wasail al Shia (348/10) kuwa mmoja katika Mashia alimwambia Imam wake;

Mimi nimehijii mara kumi na tisa na nimefanya Umrah mara kumi na tisa.

Imam akamwambia;

Ongeza bado Hija moja na ufanye Umra niyingine ili uweze kuandikiwa thawabu ya ziara moja tu ya kaburi la Al Husayn .

Na hii maana yake ni kuwa bora mtu alizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) mara moja kuliko kuhangaika kwenda Makka akahiji Hija ishirini, ikimaanisha pia kuwa maulamaa wenu wanapendekeza watu kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kuliko kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Haydar: Huenda wanakusudia kuwakumbusha tu watu wasije wakasahau kwenda kulizuru kaburi la Al Husayn .

Khalid: Ningependa kukuuliza suali; Unadhani wanalijuwa kweli mahali lilipo kaburi la Al Husayn ?

Haydar: Unasema nini ewe Khalid, unataka kuifuta historia na ukweli wake?

Khalid: Unajuwa vizuri kuwa mimi sipendi kuongea maneno matupu bila ya dalili. Ama kuhusu mahali lilipo kaburi laAliy (Radhiya Llahu anhu) imeandikwa katika kitabu Tahadhiyb al Kamal (305/13) kutoka kwa Abu Jaafar al Sadeq amesema;

Kaburi laAliy halijulikani lilipo.

Na imeandikwa katika Tarikh al Baghdadi (138/1) kutoka kwa Mutin kuwa amesema;

Lau kama Mashia wangelimjua aliyezikwa ndani ya kaburi hili wanalolizuru nje ya mji wa Al Kufa (wakidhani kuwa ni kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)) basi wangelilipiga kwa mawe. Hili ni kaburi la Al Mughira bin Shuuba.

Na hii ni kwa sababu hapana hata mtu mmoja mwenye kujua uhakika wa mahali alipozikwa Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) baada ya kuuliwa.

Haydar: Juu ya uhakika uliotaja, hata hivyo mimi sidhani kama watu wanalitukuza kaburi hilo kiasi cha hivyo unavyosema wewe, isipokuwa watu wanahimizwa tu ili wasipuuze ziara ya kwenda huko.

Khalid: Turudie mazungumzo yetu juu ya thawabu anazopata mtu aliyezuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu), kwani yareti mambo yangesimama hapo kuwa thawabu zake ni sawa na thawabu za Hija ishirini, bali katika vitabu vingine thawabu zake zimefikia kuwa sawa na Hija themanini, na haya yameandikwa katika kitabu kiitwacho Thawabul aalmaal ukurasa wa 52 na katika Wasail al Shia, imeandikwa kuwa thawabu za kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni sawa na Hija mia moja tena hija yenyewe iwe pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) 350/10).

Na katika hiyo hiyo Wasail al Shia, zimekuja riwaya nyingine zinazosema kuwa thawabu zake ni sawa na Hija elfu zilizokubaliwa, Umra elfu zilizokubaliwa, Ujira wa mashahidi elfu moja waliokufa katika vita vya Badar, thawabu za watu elfu waliofunga, thawabu za sadaka waliopewa watu elfu zikakubaliwa pamoja a thawabu za watu elfu waliotenda mema kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.

Haya yote yameandikwa katika Wasail al Shia (353/1), Kamil al Ziarat uk. 143 na Bihar al Anwar (18/110).

Haydar: Maneno haya maana yake ni kupunguza shani ya kuikusudia nyuma ya Mwenyezi Mungu.

Khalid: Kama nilivyokwambia ewe ndugu Haydar kuwa sisi tumekwishajulishwa kiasi cha thawabu tunazopata tukenda kuhiji Makka, na pia tukisali ndani ya msikiti mtukufu wa Makka. Lakini kama itakavyokuwa, hatuwezi kuzifikia thawabu mnazozipata nyinyi mnapokwenda kulitembelea kaburi la Al Al Husayn mara moja tu. Kwa sababu maulamaa wenu wanaifadhilisha ziara ya kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kuliko Hija, kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Furu-ul Kafi (324/1) na kama alivyoeleza Attusi katika kitabu cha Tahadhiyb (16/2) na kama walivyoeleza wengi miongoni mwa maulamaa wenu waliosema; Atakayelizuru kaburi la Al Husayn akiwa anaijuwa vizuri haki yake katika siku isiyokuwa sikukuu Mwenyezi Mungu atamuandikia Hija ishirini zilizokubaliwa, na atakayelizuru siku ya Sikukuu Mwenyezi Mungu atamuandikia Hija ishirini na Umra ishirini, na atakayelizuru siku ya Arafat akiwa anaijuwa vizuri haki yake Mwenyezi Mungu atamuandikia Hija elfu moja na Umra elfu moja pamoja na thawabu za kupigana vita elfu vya jihadi pamoja na Mtume aliyetumwa au Imam muadilifu.

Haydar: Juu ya yote hayo katika nyoyo zetu tunaipenda nyumba ya Mwenyezi Mungu mapenzi yasiyo na mfano.

Khalid: Lakini katika vitabu vyenu yako baadhi ya maandishi yanayoufadhilisha mji wa Karbala kuliko Al Kaaba na kuliko mji wa Makka, kwa mfano maneno aliyoandika Al Majlisi katika kitabu cha Bihar al Anwar (101-107) kutoka kwa Abu Abdullah kuwa alisema;

Mwenyezi Mungu aliifunulia wahyi Al Kaaba akaiambia; Lau kama si udongo wa Karbala nisingekufadhilisha, na lau kama si kwa heshima ya yule aliyezikwa Karbala nisingekuumba, na wala isingejengwa nyumba unayojifakharisha nayo, basi powa tena tulia na uwe mkia usiotakabari juu ya ardhi ya Karbala, ama sivyo nitakughadhibikia kisha nitakutumbukiza katika moto wa Jahannam.

Haydar: Haya tena wallahi ni maneno ya ajabu ndiyo kwanza leo nayasikie.

Khalid: Kauli hizi ni sahihi inayotiliwa nguvu na kuungwa mkono na maulamaa wengi wanaojulikana miongoni mwa Mashia.

Haydar: Ikiwa zinapatikana thawabu zote hizi kwa nini basi ziara hii isitajwe ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu?

Khalid: Jawabu yako utaipata ndani ya kitabu cha Bihar al Anwar (101-290) imeandikwa;

Mtu mmoja alimuuliza Imam; Mwenyezi Mungu amewafaridhishia watu kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu lakini haikuitaja ziara ya Al Husayn alayhi ssalaam.

Imam akampa jibu linaloonyesha kama kwamba kuna utata kidogo ndani yake. Alisema;

Juu ya kuwa haikutajwa, lakini Mwenyezi Mungu ametaka kuijaalia iwe hivyo.

Kuna kukiri wazi wazi kuliko huko juu ya uongo wa riwaya hizi zisizokuwa na isnadi wala ukweli?

Haydar: Juu ya yote uliyoyataja, lakini mimi naitakidi kuwa watu wa kawaida miongoni mwa Mashia na wale wanaopenda ukweli wanaienzi na kuitukuza nyumba ya Mwenyezi Mungu na kwamba ndani yake mna thawabu nyingi sana na nyoyo zao siku zote zina shauku ya kuiendea nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Khalid: Fadhila hizi zinazotajwa juu ya kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) zimewafanya watu wengi wawe na shauku kubwa ya kulizuru kaburi la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kuliko waliyokuwa nayo ya kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Wasail al Shia kuwa;

Wallahi nilitamani nisingehiji na badala yake ningekwenda kumzuru.

Wanazusha hadithi nyingi za uongo juu ya fadhila za Karbala hata wakazua hadithi inayosema kuwa eti ndani yake udongo huo mna ponyo, kama alivyosema Khomeni katika kitabu chake kiitwacho Kashf al Asrar uk. 62

Haydar: Tufanye nini mbele ya hadithi hizi nyingi zinazopokewa na watu wa kawaida katika Mashia wanaopenda kufanya mambo ya kheri hata wakatamani kuwazuru watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Khalid: Muislamu mwenye kumpenda Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) hafuati matamanio ya nafsi yake, bali hutumia akili pamoja na dalili zilizo wazi zinazotokana na hadithi sahihi zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na hata kama atawapenda watu wa nyumba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) lakini anatakiwa asiende kinyume na yale yaliyothibiti. Ni vizuri pia kama atafuata yale aliyofanyaAliy (Radhiya Llahu anhu) kwa sababu yeye aliishi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kwa sababu yeye anayajua vizuri zaidi matendo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Yareti kama Shia wa kawaida atafanya hayo basi atapata kheri nyingi sana ndani yake.

Ujuwe pia ewe ndugu Haydar kuwa riwaya hizi hazikuja ila baada ya kubaidika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na zama za waloziandika hadithi hizo na hii niyo sababu ya kujaa kwa habari za uongo ndani yake, na kuenea kwake uongo huo, na wakati huo hapakuwa na wanaoitetea dini ya Mwenyezi Mungu.

Rudi juu

Kupiga vifua

 

Khalid: Hebu tuzungumze juu ya kulia kwenu kwa ajili ya kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya Llahu anhu), kuomboleza, kupiga vifua, kujipiga vichwani mpaka damu kuwatoka na mambo mengi mnayofanya kila mwaka katika mwezi huu wa Muharrahm katika Al Husayniyat.

Haydar: Mambo haya si mageni na wala si uzushi, ingawaje jina lake ni jipya, lakini mambo yote hayo yalikuwa yakijulikana tokea wakati wa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na ilikuwa ikijulikana kuwa Al Husayn alayhi ssalaam atauliwa tokea Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipomhadithia binti yake Al Zahraa juu ya kuuliwa kwa mwanawe na alimuonesha hata udongo wa ardhi atakayouliwa juu yake, na hali kadhalikaAliy bin Al Husayn alipowasili Madina alipiga kambi na wanawake wakakaa hapo, akamwita mshairi akawa anasoma mashairi ya kuomboleza kifo cha Al Husayn na akaweka msiba mahali hapo karibu miaka thelathini na nne.

Khalid: Hebu tuyaangalie mambo kwa utulivu. Tokea pale Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipowajulisha juu ya yale yatakayomsibu mjukuu wake alitamka hayo kwa ajili ya kutoa habari tu au alikusudia kuweka sheria maalum?

Haydar: Kuna tofauti gani?

Khalid: Kama ilikuwa kwa ajili ya kutoa habari tu, basi haiwezi kuchukuliwa kuwa ni amri iliyowekewa sheria. Kwa mfano; tumejulishwa kuwa Siku ya Kiama ni sawa na miaka elfu hamsini. Habari hizi haziwezi kuwekewa sheria yoyote ile juu yake katika hukmu za halali na haramu.

Kwa hivyo Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipotupa habari ya kifo cha Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) alikuwa akitujulisha tu, na ilikuwa wajibu wetu sisi kusadiki yale aliyotujulisha, lakini hatukuambiwa tena na sisi tuanzishe au tuzushe hukmu nyingine za kisheria juu ya yale yaliyotendeka siku hiyo, ama sivyo Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) angetuamrisha kufanya hivyo pale alipotujulisha juu ya kuuliwa kwa mjukuu wake.

Ama kuhusu ile riwaya yaAliy bin Al Husayn kuwa alimwita mshairi aliyekuwa akisoma mashairi ya kuomboleza na kwamba aliendelea kufanya hivyo kwa muda wa miaka thelathini na nne takriban, riwaya hii haina isnadi sahihi yaani hadithi hii ni dhaifu na kufanya matendo kama hayo si katika yale aliyotufundisha babu yake ambaye ni Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), bali kinyume chake ametukataza kufanya hivyo.

Haydar ; Lakini ukichunguza vizuri juu ya yaliyomsibu Al Husayn alayhi ssalaam kwa jicho la kutafakari, ungejuwa kuwa alifanya jambo asilopata kulifanya kiumbe chochote kingine. Kwani yeye alitoka akiwa amekasirishwa na dhulma iliyokuwa ikitendeka wakati wake, hata akawa mfano bora wa kuigwa na kwa ajili hiyo hata mwahali mwengi kumeitwa kwa jina lake (Al Husayniyat).

Khalid ; Ewe ndugu Haydar,

kwanza - Hili jina la Al Husayniyat (sehemu zinazopigwa jauseni) halikuja isipokuwa katika miaka ya mwisho ya utawala wa Kiislamu katika dola ya Kibuweihiyah kwa mfano. Na jambo hili halikuwepo zama za Al Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) wala wakati wa watoto wa Al Husayn (Mwenyezi Mungu awarehemu).

Pili Huoni kuwa kutokana na jina hili, ni dalili ya kupindukia mipaka katika kumtukuza kwenu Al Husayn (Radhiya Llahu anhu). Kwanini hamujaita kwa mfano Aliyat au Alawiyat au Muhammadiyat, kwa vile wao ni bora kuliko Al Husayn (Radhiya Llahu anhu), jambo ambalo sidhani kama yeyote mwenye akili timamu anaweza kulipinga.. Kwa nini mkalipa jina la Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)?

Tatu - Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipata adhabu nyingi sana kutoka kwa makafiri hata ikambidi auhame mji wa Makka. Na katika mji wa Taif Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipigwa mawe, na mara nyingi alikosewa kuuliwa, lakini hatukupata kumsikia hata siku moja akiwachochea watu kufanya zogo, isipokuwa aliwataka kupigana Jihadi chini ya bendera yake (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Nne Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) aliuliwa tokea mwaka wa 61 Hijri (miaka 61 baada ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kuhama kutoka Makka kwenda Madina), kwa nini basi tusijishughulishe kufanya zile ibada zilizokuwa zikifanywa wakati ule au kabla yake?

Tano - Kwa nini Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) asitoke kwenda kupigana na Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu) juu ya kuwa Mu'awiyah alikuwa Khalifa wa Waislamu kwa muda upatao miaka ishirini?

Sita Kwa nini Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) asitoke kwenda kupigana na Yazid mpaka zilipoanza kumfikia zile barua kutoka Iraq?

Saba Kwa nini Al Hassan (Radhiya Llahu anhu) asiende kupigana na Mu'awiyah baada ya kumpa ukhalifa yeye mwenyewe?

Nane Yupo Imam yeyote mwingine aliyetoka kwenda kupigana na Khalifa yeyote wa Kiislamu baada ya Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)?

Haydar ; Kuna ubaya gani ikiwa watu fulani watajikusanya kwa ajili ya kuwakumbuka watu wa nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam)?

Khalid ; Hapana kilicho bora kuliko kufuata mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) katika kuwalingania kwake watu na katika kupigana Jihadi, na tunatakiwa daima tuwe tunachukua ibra katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo;

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema (mfano mwema wa kuufuata) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.

Al Ahzab 21

Je, haya yote yanapatikana katika vikao vyenu hivi?

Na pia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo ;

Wanaoamirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kusimamisha Sala na kutoa Zaka na hawamuogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu.

At Tawba - 18

Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala anawasifia hapa wale wanaoamirisha misikiti Yake kwa kumdhukuru na kwa kufanya matendo ya kumtii, lakini hatuwaoni wale wanaohudhuria vikao kama hivi vya Al Husayniyat (vikao vya kupiga jauseni) kuwa ni watu wenye kuijaza misikiti, wala hatuwaoni kuijaza misikiti hata katika mwezi wa Ramadhani, jambo lililohimizwa katika dini na pia maulamaa wengi wamesema juu yake na hata aalim maarufu wa Kishia Al Amiliy amesema katika Wasail (185/50) kuwa; Bin Mahran alimuuliza Imam wake juu ya umuhimu wa kusali ndani ya mwezi wa Ramadhani, akamjibu;

Usali kama unavyosali katika miezi mingine, isipokuwa ndani ya mwezi wa Ramadhani mja anatakiwa azidishe katika Sunnah zake kama akipenda. na kama ataweza basi azidishe katika mwanzo wa mwezi huo rakaa ishirini kuliko alivyokuwa akisali katika miezi mingine.

Haydar: Lakini ndani ya Al Husayniat (vikao vya jauseni) mna mafunzo makubwa sana katika kuwaelimisha watoto hukmu za dini yao na kuwalea malezi bora yenye baraka ndani yake.

Khalid: Yareti hayo unayosema yangekuwa yanatendeka kweli basi yangekubaliana na mafunzo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam), lakini ndani ya vikao hivyo juu ya kuwa yanakuwepo baadhi ya mawaidha na nasaha lakini mengi yanayotendeka humo ni matusi, laana na kuzika mbegu za chuki ndani ya nyoyo za Mashia dhidi ya ndugu zao Masunni. Na yareti maneno hayo yangekuwa yanasemwa na watu wa kawaida, lakini la kusikitisha ni kuwa laana na matusi hayo yanafundishwa na maulamaa wakubwa wanaojulikana

Rudi juu

Wali na nyama

 

Khalid: Usisahau kuniletea na mimi chakula mnachogawiwa katika Ashura.

Haydar: Bila shaka, vipi nitakusahau na wewe ni rafiki yangu?

Khalid: Hukubaliani namimi kuwa kuihusisha siku kama hii kwa matendo kama haya pamoja na kufunga nusu siku, kuwa haya yote yanahitajia dalili za kisheria ili yakubalike kuwa ni ibada anayopata mtu thawabu ndani yake?

Haydar: Unataka kuwakosowa Mashia kwa sababu wanatoa sadaka na vyakula katika siku kama hii kwa ajili ya Al Husayn alayhi ssalaam huku wakitegemea ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu?

Khalid: Chakula hakina makosa yoyote, mtu akitaka anakula na asipotaka hali, lakini kadhia yetu sisi ni ile nia ya kutoa sadaka hizo na ile nia ya kuwachinja wanayama katika siku hiyo, pamoja na matendo mbali mbali wanayohangaika kuyatenda ndani ya siku hiyo. Kwa sababu mtu anapochinja kwa ajili ya mtu fulani na si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huyo anapata dhambi hata kama atapiga bismillahi pale anapochinja.

Haydar: Unataka kuniambia kuwa wewe unaweza kuzisoma nia za watu?

Khalid: Mtu anatakiwa matendo yake yalingane na nia yake, kwa sababu Muislamu anapokuja akachinja siku ya Karbala na mtu huyo hana kawaida ya kuchinja isipokuwa katika siku hii tu, tunaelewa wazi kuwa hakuchinja isipokuwa kwa mnasaba wa siku hii. Na chochote ambacho msingi wake ni batili basi siku zote kitabaki kuwa batil, kwa sababu haikuja katika sheria ya Kiislamu hukmu ya mtu kuchinja mnyama kwa ajili ya kumbukumbu ya kuuliwa kwa mtu.

Haydar: Kama kwamba umesahau yale niliyokwambia kuwa wanyama wanaochinjwa na vyakula vinavyopikwa ni kwa ajili ya kuwalisha waliohudhuria shughuli hizi za jauseni waliokuja kwa ajili ya kupata ibra na kujifunza juu ya kuuliwa kwa shahid Abu Abdullah Al Al Husayn alayhi ssalaam?

Khalid: Kwa hivyo kusudi lote hilo ni kuwakusanya Waislamu katika siku hii ya Kerbala siku aliyouliwa Al Husayn (Radhiya Llahu anhu)?. Je, ninaweza kukuuliza suali moja?

Haydar: Tafadhali uliza.

Khalid: Ipo dalili yoyote kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ya kuihusisha siku hii ya Ashura kwa ibada maalum?

Haydar: Ninavyojuwa mimi ni kuwa hapana dalili yoyote isipokuwa juu ya kufunga siku hii kama ulivyonambia wewe mwenyewe hapo mwanzo.

Khalid: Sasa ikiwa hapana dalili yoyote ile, nani huyu basi aliyethubutu kutoa fatwa kama hii ya kuwataka Waislamu wawe wanakula baada ya adhuhuri katika siku hii ya Ashura, au nani aliyetoa fatwa ya kuwataka Waislamu wawe wanajipiga vifua kwa mikono na kwa visu na vijembe na damu nyingi kumwagika? Na nani aliyetoa fatwa ya kuirudia huzuni hii kila mwaka kuwa watu wawe wakijikusanya na kulia na kuomboleza huku wakijipiga makofi ya uso na kuchana nguo zao? Na nani huyu mwenye akili nyingi aliyetoa fatwa hii ya kuwataka watu waache ibada zao zilizowekewa sheria na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na badala yake kujishughulisha na mambo kama haya yenye kupoteza wakati wa watu bila manufaa yoyote?

Haydar ; Huenda ikawa mmoja katika Masahaba (Radhiya Llahu anhu) au katika watu wa nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliwahi kufanya haya?

Khalid: Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) aliuliwa mwaka wa 61 baada ya Hijra na baadhi ya Masahaba (Radhiya Llahu anhu) walikuwepo wakati huu, kwanini basi tusisikie kuwa hata mmoja wao aliwahi kufanya matendo kama hayo kutokana na mnasaba huo? Na je, Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) kwa mfano angeliuliwa siku ya Sikukuu, tungeacha kuisherehekea siku hiyo pia na kuvaa nguo nyeusi katika siku ya furaha ?

Haydar: Kama kwamba unauona msiba huu kuwa ni mdogo sana?

Khalid Nani aliyekwambia kuwa kuuliwa kwa Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) ni msiba mdogo? Bali msiba huu ni mkubwa sana na dhulma kubwa sana imepita, na kila aliyeshiriki katika mauaji haya atapata kwa Mwenyezi Mungu kile anachostahiki. Lakini msiba upi unadhani ulio mkubwa zaidi; kufariki kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) au msiba wa Al Husayn  (Radhiya Llahu anhu) au hata kuuliwa kwaAliy bin Abu Talib (Radhiya Llahu anhu)? Juu ya ukubwa wa msiba wao lakini hatufanyi lolote isipokuwa kufaidika na ibra inayopatikana katika kuwakosa kwa njia isiyokwenda kinyume na sheria.

Haydar ; Lakini Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) ametupa funzo kubwa la namna ya kupambana na wapotofu.

Khalid ; Ndugu yangu mpenzi, unataka tujifunze kutokana na haya juu ya namna ya kupambana na serikali zinazotutawala au namna ya kuupigania ukubwa, na je Masahaba waliokuwa wakiishi wakati wake walikubaliana naye kuhusu jambo hilo, Sahaba kama vile Ibni Abbas na wengine (Radhiya Llahu anhu)? Lazima utambuwe ewe Haydar kuwa utawala wa Bani Umayya umewekwa na Imam Al Husayn (Radhiya Llahu anhu) baada ya kujishusha ukhalifa wake na kumkabidhi Mu'awiyah (Radhiya Llahu anhu).

Sasa je, unataka tuwafunze watoto wetu namna ya kuzipindua serikali? Na kwa nini tuiadhimishe siku aliyouliwa Al Husayn tu (Radhiya Llahu anhu) wakati wapo wengi walio watukufu kupita yeye waliouliwa pia kwa dhulma?

Haydar: Sisi hatumhusishi Al Husayn peke yake (Mwenyezi Mungu awe radhi naye), bali tunajitahidi kufanya maombolezo ya kila mtu mwema.

Khalid: Ikiwa haya unayoyasema ni kweli ewe ndugu Haydar, basi itatukuta kazi kubwa ya kufanya maombolezo na hafla za misiba kwa ajili ya watu wema wengi wakiwemo watu wa nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na wengineo. Na kama tutahesabu misiba iliyowakuta watu wema tokea siku aliyoumbwa Adam (AS) mpaka siku ya leo, basi idadi yao itazidi idadi ya siku za mwaka mzima, bali huenda idadi hiyo ikazidi idadi ya saa za mwaka mzima. Hivyo sisi tumeumbwa kwa ajili hiyo ?

Rudi juu

Kwa nini Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu)?

 

Haydar: Katika mazungumzo yaliyopita ulitaka tuzungumze juu ya uadilifu wa Masahaba, ukasema kuwa watu hawa hawasemi uongo. Utasemaji nikikuuliza juu ya Sahaba ambaye zimepokelewa kutoka kwake hadithi nyingi kupita kiasi. Kupita hata uwezo wake?

Khalid: Kama kwamba unataka tuzungumze juu ya hadithi za Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) zilizopokelewa kutoka kwa baadhi ya Masahaba (Radhiya Llahu anhu)?

Haydar: Ndiyo, tuzungumze juu ya Masahaba wanaohusika na elimu ya hadithi.

Khalid: Si bora tuzungumze juu ya aalim wa hadithi mashuhuri kupita wote katika Masahaba?

Haydar: Nani unayemkusudia ?

Khalid: Namkusudia Abdul Rahman bin Sakhar al Dousiy, yule Sahaba aliyejitolea kuifanya kazi ya elimu hii ya hadithi.

Haydar: Mara ya mwanzo leo nalisikia jina hili.

Khalid: Hulaumiki, kwa sababu Sahaba huyu anajulikana zaidi kwa umaarufu wake kuliko kwa jina lake. Nakusudia Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu).

Haydar: Nishamkumbuka! mwanachuoni wetu maarufu aitwae Al Husayn Sharafuddin Al Mousawiy alizungumza juu yake katika kitabu kizuri sana kiitwacho Abu Hurairah, na akabainisha ndani yake udhaifu wa riwaya zake mtu huyu.

Khalid: Kabla sijasema lolote kuhusu kauli yako hii, ningependa kukuuliza suali moja. Umewahi kusoma chochote juu ya Sahaba huyu mtukufu (Radhiya Llahu anhu) katika vitabu vya Masunni?

Haydar: Kusema kweli sijapata kusoma chochote, isipokuwa nimekwishasikia mengi sana juu yake mtu huyu kutoka kwa wanavyuoni wetu, na wote wanasema kuwa hadithi zilizopokelewa kutoka kwake zote si sahihi. Hata hivyo na tuzungumze juu yake, lakini kwa utulivu, na suali langu la mwanzo nataka kujua ; mtu huyu amesilimu mwaka gani?

Khalid: Inajulikana kuwa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) amesilimu mwaka wa saba baada ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kuhajiri kwenda Madina na umri wake wakati ule ulikuwa miaka thelathini, na alikuwa akiishi al Suffah (mtaa ulioshikamana na nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) mahali walipokuwa wakiishi masikini na wacha Mungu), na alikuwa daima pamoja na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), hambanduki, kila anapokwenda alikuwa naye mpaka siku ile Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) alipofariki dunia.

Haydar: Lakini kinachostaabisha ni ule uwezo wake wa kuhifadhi hadithi hata akaweza kuhifadhi hadithi nyingi kuwapita Masahaba wote.

Khalid: Hii inatokana na dua aliyoombewa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) pale Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) alipomuendea Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kumshitakia udhaifu wake wa kuhifadhi, na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia; Itandaze nguo yako, na alipoitandaza (Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamuombea dua) kisha akamwambia; Sasa jifunike nayo kifuani pako, akajifunika na tokea siku hiyo hakusahau tena hadithi.

Haydar: Hadithi hii ngeni kwangu, je umewahi kuifanyia tahakiki ewe ndugu Khalid ?

Khalid: Hadithi hii imesimuliwa na Bukhari na wengineo kwa hivyo ni sahihi Alhamdulillah, na hadithi hii haimo ndani ya vitabu vya maulamaa wa Kisunni peke yao, bali imo hata ndani ya vitabu vya hadithi vya Kishia.

Imeandikwa katika kitabu cha Al Kharaij (1/75) na katika Bihar al Anwar (18/913) mlango wa Miujiza ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na kukubaliwa kwa dua zake kuwa; Abu Hurairah alimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam); Mimi nasikia kutoka kwako hadithi nyingi kisha nazisahau Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akamwambia; Tandaza guo lako lote, akatandaza kisha Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akauweka mkono wake ndani yake kisha akamwambia; Jifunike nalo, nikajifunika anasema Abu Hurairah; na tokea siku hiyo sijasahau tena hadithi.

Haydar: Lakini kinachoshangaza ni kuwa Abu Hurairah huyu amesimuliwa hadithi nyingi zisizoweza kulingana na muda wake mfupi tokea aliposilimu.

Khalid: Kwa kuanzia ndugu Haydar, ningependa kukuuliza iwapo unazijuwa idadi ya hadithi alizozisimuliwa Abu Hurairah?

Haydar: Maelfu kwa maelfu ya hadithi.

Khalid: Jaribu kunipa idadi sahihi, kwani katika vitabu sita maarufu vya Masunni na katika Muwata-a cha Imam Malik hadithi za Abu Hurairah zilizopokelewa ndani yake idadi yake ni 2218 zilizokubaliwa na katika vitabu vya Sahih Bukhari na Sahih Muslim mna hadithi 609 tu za Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) na walizokubaliana juu yake Bukhari na Muslim ni 326, ziko wapi sasa hizo hadithi maelfu kwa maelfu?

Haydar: Si mimi ninayesema hivyo, haya ni maneno ninayowasikia maulamaa wetu wengi wanapozungumza juu ya mtu huyu.

Khalid: Masahaba wengi na maulamaa wengi pia wamemsifia sana Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) na wameisifia elimu yake pia, mfano wa Abu Saeed al Khudary (Radhiya Llahu anhu) aliposema;

Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema kuwa Abu Hurairah ni chombo cha elimu.

Imam Shafi naye alisema; Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) hodari wa kuhifadhi kupita wote wenye kuhifadhi hadithi katika wakati wake.

Ama Imam Bukhari yeye amesema yafuatayo juu ya Abu Hurairah; Maulamaa wapatao mia nane wamepokea hadithi kutoka kwake, na alikuwa hodari wa kuhifadhi kupita watu wote wa elimu ya hadithi wa zama zake.

Haydar: Lakini anacholaumiwa Abu Hurairah ni kuwa hapana mtu yeyote duniani aliyewahi kusimulia hadithi nyingi kuliko yeye. Hapana mwanadamu yeyote anayeweza kuhifadhi hadithi nyingi kama hizo.

Khalid: Kwanza kabisa uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi unatokana na baraka za ile dua aliyoombewa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Pili Mtu aliyekiwishajitolea kutafuta elimu na kusikiliza hadithi za Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ataweza kweli kushindwa kukusanya idadi hiyo ya hadithi?

Tatu Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) alikuwa na wanafunzi wengi waliopokea kutoka kwake hadithi hizo.

Nne Hadithi alizozisimuliwa Abu Hurairah zimo ndani yake maneno ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na zingine ni juu ya matendo ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) na nyingine ni juu ya matendo ya baadhi ya Masahaba yaliyokubaliwa na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Tano Zipo hadithi ambazo Abu Hurairah amesimulia juu ya aliyoyasikia kutoka kwa Masahaba (Radhiya Llahu anhu) yale ambayo Masahaba hao waliyasikia kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Sita zipo hadithi nyingi pia zisizosihi isnadi, yaani hadithi alosingiziwa tu Abu Hurairah kuwa amesimulia wakati yeye hakuzisimulia hadithi hizo.

Saba kupania kwake Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kwa ajili ya kuifanya kazi hii tu. Yaani kuzikusanya hadithi za Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam).

Nane Ulizungumza juu ya uwezo wake wa kuhifadhi hadithi ukasema kuwa hapana mwanadamu anayeweza kuhifadhi namna hiyo. Sasa mimi nitakuuliza suali; Uwezo upi unaoshangaza zaidi, ule wa Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kuhifadhi hadithi elfu chache alizozisikia kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kwa muda wa miaka mitano au ule wa yule aliyehadithia maelfu kwa maelfu ya hadithi?

Haydar: Pengine unawakusudia Maimamu wetu!

Khalid: Wala si katika Maimamu, bali hawa ni watu wa kawaida tu na hawaifikii hata chembe daraja ya Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu), na mmoja wao ni Aban Bin Taghalab ambaye Al Sadeq amesema juu yake; Hakika Aban Bin Taghalab amesimulia hadithi zangu 30,000, kwa hivyo na nyinyi zisimulieni.

Na mwengine Muhammad bin Muslim bin Rabah, huyu amesema juu yake An Najashi katika kitabu chake kiitwacho Al Rijal ukurasa wa 163 kuwa; Muhammad amepokea kutoka kwa Al Baqer hadithi 30,000 na amepokea kutoka kwa Al Sadiq hadithi 16,000.

Na mwengine Jaber bin Yazid al Juafiy aliyesimulia hadithi nyingi sana za watu wa Nyumba ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) ambaye Al Koshy katika tarjima yake uk.194 akimnukuu mtu huyu ameandika yafuatayo; Nimehadithiwa hadithi 50,000 hajapata kuzisikia mwengine isipokuwa mimi.

Na Al Hurr al Amiliy ameandika katika hitimisho la kitabu chake kiitwacho Wasael (20/151) kutoka kwa Jabir yafuatayo; Kuwa yeye amehadithiwa hadithi 70,000 kutoka kwa Al Baqer na amehadithia hadithi zipatazo140,000.

Sasa tukirudia suali lako; Je hadithi alizozisimulia Abu Hurairah zinaweza hata kukaribia idadi ya hadithi alosimulia mtu huyu? Kwa kukupa habari tu, Abu l Al Husayn huyu ameandika kitabu kiitwacho Al Muraja-at ambacho ndani yake amewasifia sana na kuwatetea watu hawa walohadithia maelfu kwa maelfu ya hadithi, kwa nini basi asingefanya uadilifu angalau kidogo akamtetea na Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) pia?

Haydar: Lakini wapokeaji wa hadithi wa madhehebu ya Kishia Mwenyezi Mungu awarehemu wanajulikana kuwa ni watu wema na waadilifu na wanajulikana pia kwa uwezo wao mkubwa wa kuhifadhi. Tafadhali usizikanushe fadhila hizi ewe Khalid.

Khalid: Ama kuhusu uwezo wa kuhifadhi, jambo hili halina haja hata kuzungumza juu yake, kwani hadithi zilizoandikwa ndani ya vitabu vyenu vya asili zinagongana na kupingana. Ama kuhusu wema wao lau kama ungesoma kidogo tu katika vitabu vya kishia mfano kitabu kiitwacho Rijal al Koshy, nk. ungeujuwa vizuri wema wao watu hawa waliohadithia hadithi kwa maelfu. Na hapa nakunukulia riwaya iliyoandikwa katika kitabu hiki cha Rijal al Koshy uk. 95 inayomzungumzia juu ya mmoja wa watu hao aitwae al Uqaili. Anasema Al Koshy: Al Uqaili alikuwa miongoni mwa masahaba wa Amiri l Muuminin, na alikuwa mlevi wa kutupwa lakini alikuwa akihadithia hadithi kama alivyokuwa akizipokea.

Na Abu Hamza al Thamali Thabit bin Dinar naye pia alikuwa mlevi kama ilivyoandikwa katika kitabu hicho cha Al Koshy uk. wa 76.

Ali bin Hamza al Batainiy alikuwa akiiba pesa za Al Maasum na khums wanazolipa maimamu wa kishia, na hata amefikia kulaaniwa na kuambiwa kuwa ni muongo. Yote haya yanapatikana katika kitabu kiitwacho Al Waqifiyah dirasah tahaliyliyah (1/418). Na wengi wengineo. Kwa hivyo katika vitabu vya Mashia si muhimu kwao uadilifu wa msimuliaji wa hadithi, inatosha tu msimuliaji huo awe ni mtu anayewapenda Ahli l Bayt basi hadithi zake zitakubalika na si muhimu hata kama atakuwa muongo au mlevi au mwizi au awe fasiqi namna gani.

Haydar: Juu ya yote uliyosema ewe ndugu Khalid, lakini hizi riwaya za Abu Hurairah hazikubaliwi na maulamaa wetu na hii ndiyo sababu huwezi kuziona ndani ya vitabu vyetu.riwaya za mtu huyu.

Khalid: Ndugu Haydar naona bora nimalize mazungumzo haya mazuri baina yetu kwa kukujulisha kuwa Mashia waliotangulia walikuwa wakiziandika na kuzifanyia kazi hadithi za Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu), na pia maneno yake na fatwa zake zote hizo zilikuwa zikiandikwa na maulamaa wengi wa mwanzo wa Kishia na walikuwa wakizifanyia kazi pia na utazikuta kwa mfano katika kitabu cha Mirza Al Husayn Nuri al Tubrusi katika kitabu chake kiitwacho Mustadrak al Wasael. Ndani ya kitabu hicho ameandika hadithi nyingi za Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) katika mlango wa Al Ijarah (14/28), bali Sheikh al Mufiyd pia ameandika hadithi nyingi za Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) katika kitabu chake kiitwacho Al Amaliy na utazikuta katika ukurasa 111-112-113.

Na Sheikh Al Saduq naye pia katika kitabu cha Maaniy al akhbar ukurasa wa 80-90 ameandika hadithi zake, na pia katika kitabu Ikmal al din, ukurasa wa 136, na katika kitabu cha Al Khiswal wa thawab al aamal pia na katika vitabu vingi vinginevyo. Kwa nini basi unakanusha tu kabla ya hata kuangalia kwanza ndani ya vitabu? Daima mimi husema kuwa tatizo la vijana wa Kishia wenye kupenda kheri huwa hawapendi kusoma vile vitabu vya asili vya Kishia na pia hawaulizi dalili kutoka kwa mashekhe wao, bali wao wanasema tu kila wanachoambiwa na wale mashekhe wanaopenda kuzungumza bila dalili.

Haydar: Unataka kuniambia kuwa yote wanayosema wanavyuoni wetu juu ya mtu huyu si ya kweli?

Khalid: Ndiyo ewe ndugu Haydar, kwani maulamaa wote wa Ahlu Sunnah wamekubaliana juu ya ukweli wa riwaya zake Sahaba huyu mtukufu (Radhiya Llahu anhu), na pia maulamaa wa Kishia waliotangulia nao pia wamezikubali riwaya zake, na kama utasoma vitabu vyenu vilivyoandikwa na maulamaa wa zamani basi hutamuona yeyote kati ya maulamaa wenu mwenye kumchukia au mwenye kuzikataa riwaya zake isipokuwa mtu mjinga ambaye Mwenyezi Mungu hakumfungua kifua chake apate kunufaika na elimu iliyo sahihi. Na lau kama utamuuliza yeyote anayemtukana au anayejaribu kumuondolea hadhi yake Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) Kwa nini unamchukia Sahaba huyu namna hii? Umesoma nini juu sira ya Sahaba huyu? Ameukosea nini Uislamu? Hutoweza kupata jawabu yoyote itakayokukinaisha, kwani tuhuma zote hizo zinatokana na ujinga wa watu wachache wasiosoma chochote katika vitabu vya Kisunni wala vya Kishia.

Haydar: Lakini anayezitoa makosa hadithi za Abu Hurairah hufanya hivyo kwa ajili ya kuitakia kheri elimu hii ya hadithi isije ikaingia ndani yake hadithi zisizo sahihi.

Khalid: Wanaojaribu kumtia ila Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) kusudi lao hasa ni moja tu; nalo ni kuitia ila Sunnah iliyotahirika ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Na kwa vile hawakupata njia nyingine ya kuitia ila, wakaona bora wawatie ila waliotunukulia Sunnah hiyo, na kwa vile Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) ndiye mashuhuri kupita wote na ndiye aliyesimulia riwaya nyingi zaidi kupita wote ndiyo sababu wakawa wanajaribu kumtia ila.

Ijulikane kuwa watu kama Abu Hurairah (Radhiya Llahu anhu) na walio mfano wake katika Masahaba watukufu (Radhiya Llahu anhu), Mwenyezi Mungu ndiye aliyewajaalia kuifanya kazi hii ya kutufikishia Sunnah hii tukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llahu alayhi wa sallam). Sunnah ambayo ndani yake yamo mafundisho na sheria anayoipenda Mwenyezi Mungu na kuridhika nayo. Na sisi tunawapenda kwa ajili hiyo na kwa ajili ya mengi mema waliyo nayo.

Rudi juu

Hitimisho

 

Ndugu msomaji,

Baada ya mazungumzo matulivu haya pamoja na maneno yenye hekima yaliyoegemzewa dalili zilizo wazi kutoka katika vitabu vikubwa vinavyotambulikana pamoja na masdari zinazotegemewa, hatuna budi kuikubali haki na kufikiri vizuri kabla hatujatoa uamuzi wowote juu ya upande mwengine.

Inajulikana pia na kila mtu kuwa mazungumzo baina ya Shia na Sunni siku zote yanakuwa makali yaliyojaa shutuma na mwisho wake huwa hayaleti manufaa yoyote.

Kabla ya mazungumzo yoyote baina ya pande mbili hizi, zinawajibika pande zote zijaalie na kuzihusisha nia zao ziwe halisi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, na kusudi la mazungumzo yao liwe kwa ajili ya kuifikia njia ya haki, na njia ya kuifikia haki ni moja tu, nayo ni ile tuliyoitumia katika mazungumzo yetu haya.katika kuleta hoja na dalili zenye nguvu pamoja na ufasaha wa maneno.

Msomaji ataona kuwa katika mazungumzo haya hamna ndani yake ujeuri wala matusi dhidi ya mtu yeyote, isipokuwa tu tumezitaja fatwa mbali mbali na kuzungumza juu yake.

Huenda mazungumzo haya yakawa hayakujadili mambo yote yanayopaswa kuyajadiliwa baina ya Shia na Sunni, lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutoa mwangaza katika mambo mengi, pamojua na kutuwezesha kuwajilsha watu juu ya yale yasiyokuwa yakijulikana.

Namuomba Mwenyezi Mungu azijaalie kurasa hizi ziwe zenye manufaa kwa watu na hatuna haja ya chochote isipokuwa tu watu wote wawe wafuasi wa Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) kwa kufuata dalili zilizo sahihi, huku tukimuomba Mwenyezi Mungu atufufuwe sote chini ya kivuli cha Uislamu tukiwa kama ndugu tunaopendana.

Mwenyezi Mungu ni muweza wa yote hayo, na mwisho kabisa wa maneno yetu tunasema Alhamdulillahi rabbil aalamiyn, na sala na salaam zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Llahu alayhi wa sallam) pamoja na aali zake na Sahaba zake wema.

Rudi juu