kutoka

Al Hidaaya

Yaliyomo

VILOSA. 1

Kunafa  (Vitamu vya nchi za Sham) 2

PUDINI YA NAZI 4

KEKI YA JIBINI (Cheese Cake)

KEKI YA KAROTI

KEKI YA  SEMOLINA NA JOZI  (WALNUT) 7

BASBUSA - (Shaam) 8

PURI 9

VIBIBI 10

MKATE WA KIFARANSA (french toast) 11

VIKEKI VIDOGO  VYA CHENGA ZA SHAYIRI  - (OATMEAL MUFFINS) 12

PAI YA KUKU (CHICKEN PIE) 13

KEKI YA NANASI 15

KEKI ZA VIKOMBE ZA NAZI - (COCONUT MUFFINS) 16

MKATE WA NYAMA. 17

MAANDAZI YA KUPAMBIA. 18

KEKI ZA VIKOMBE. 19

MKATE WA MAYAI 20

KEKI YA TENDE. 21

MKATE WA UFUTA. 22

KHALYAT AN-NAHL   (MZINGA WA NYUKI) 23

KEKI YA MAZIWA. 24

Maandazi 25

KEKI YA MARMAR (MARBLE CAKE) 27

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 27

KEKI YA NDIZI NA NAZI 28

BISKUTI ZA UFUTA NA JAM

BISKUTI ZA MAYAI

BISKUTI ZA KASTADI

BISKUTI ZA TENDE

BISKUTI ZA CORNFLAKES. 34

MITAI 35

VIBISKUTI VYA KUYAYUKA MDOMONI 36

DONATI 37

BISKUTI ZA JAM... 38

VISHETI: 39

VILEJA VYA KARANGA. 40

BISKUTI ZA NJUGU/MATUNDA MAKAVU - (ROCK CAKES) 41

VIBISKUTI VYA MATUNDA MAKAVU NA CORNFLAKES.. 42

VIBISKUTI VYA SIAGI 43

BISKUTI ZA TANGAWIZI 44

WALI WA KICHINA WA KAMBA NA KUKU.. 45

BIRIANI YA TUNA. 46

KABABU  ZA ROJO.. 47

Mkate wa sinia. 47

SUPU YA MAHINDI, KAROTI NA VIAZI 49

Zanzibar Grilled Fish (Samaki wa Kupaka) 50

Bar Shish Kebabs (Mishkaki) 51

Grilled Zanzibar Queen Prawns. 52

Garlic Prawns (Kamba wa Vitunguu Thomu) 53

Mango Chutney (Kachumbari ya Embe. 54

KISAMVU.. 55

MKATE WA UFUTA (SESAME BREAD) 56

VILOSA.. 57

KEKI YA NDIZI 58

VITUMBUA.. 59

KEKI YA ZABIBU.. 60

Makange ya kuku.. 61

Mishkaki kwa ndizi mzuzu.. 62

NDIZI ZA MKONO WA TEMBO.. 63

NYAMA YA KABICHI NA NJEGERE.. 64

WALI KWA NYAMA YA MAHARAGE YA MAGANDA.. 65

DESSETI YA NDIZI 66

Doughnuts. 67

CHAPATI ZA MAJI 68

FUTARI YA MAHARAGE NA VIAZI VITAMU.. 69

BIRIYANI YA NYAMA YA MBUZI 70

BIRIYANI 72

KASHATA ZA KARANGA. 74

WALI ULIOFUNGWA KWA KABEJI 75

MATOKE.. 76

KIBURU.. 77

BEANS CAKE.. 78

SAMAKI WA KUPAKA.. 79

MLENDA WA BAMIA NA KARANGA.. 80

MAJANI YA MABOGA. 81

KATLESI ZA SAMAKI 82

WALI NA NJEGERE.. 83

VIAZI VYA GARAI 85

KABABU ZA KUKU.. 86

MBATATA ZA UROJO/ZANZIBAR MIX.. 87

MAKBUS (WALI WA KIARABU) 88

FISH FINGER.. 89

GITHERI NA VITUNGUU VYA KUKAANGA.. 90

KACHORI 91

 

 Rudi juu

VILOSA

 

VIPIMO

 

Mchele                                             1/2 Kikombe

Semolin                                            1 Vikombe

Tui  la nazi                                        3/4  Kikombe

Maziwa                                             1/2 Kikombe

Mayai                                                3

Hamira                                             1 kijiko cha chai kijae

Rose essence                                  kidogo

Zaafarani                                          kidogo

Sukari                                               1 kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUTENGENEZA

 1. Roweka mchele tokea usiku
 2. Uchuje mchele maji yote
 3. Weka kwenye mashine ya kusagia (Blender)
 4. Tia mayai, maziwa, sukari, hamira, rose essence, zaafarani. Kisha usagesana mpaka chenga za mchele zote zisagike.
 5. Tia semolina na tui la nazi, kasha endelea kusaga katika blender, kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
 6. Mimina katika bakuli kubwa, funika iwache iuumuke.
 7. Ikishaumuka choma kama unavyochoma vitumbua.
 8. Shira ikipowa, tumbukiza Vilosa kwa kiasi kiasi, changanya na uvitoe uviweke upande katika sahani ya kupakulia.
 9. Endelea kufanya mpaka vyote vimalizike.

 

SHIRA  

**Tengeneza mapema ipowe. Na isiwe nzito

Sukari                        2 Vikombe

Maji                            1 kikombe

Zaafarani                    kidogo

Rose                           essence


 Rudi juu

 

Kunafa  (Vitamu vya nchi za Sham)

 

 

Muda wa kutengeneza                                                     dakika 20

Muda wa kupika                                                               dakika 25

 

VIPIMO

Kataif Pastry  (Tambi za Kataif)                            Kg   =  Pakti moja 

Cheese ya Mazorella                                            Kg 

Cheese ya Ricotta                                                Kg

(Ukipenda tumia Cheese ya Ricota pekee hivyo itakuwa Kg )

Maziwa                                                                  glass

Siagi au samli  (iliyoyayushwa)                            kikombe

 

SHIRA

Maji                                                                     1   Kikombe

Sukari                                                                 2  Vikombe

Zaafarani  (iroweke na maji kidogo)                                                          

 

NAMNA YA KUTENGENEZA

 1. Kata karatasi ya Wax paper size ya bakuli uweke katika bakuli la Pyrex (la kupikia ndani ya oven) Bakuli lisiwe lenye shimo sana (sio deep) {sio lazima kuweka karatasi ya Wax ukipenda tu}
 2. Kwaruza (Grate) cheese ya Mazorella na ya Ricotta ichanganye pamoja kisha weka katika bakuli.     
 3. Tia maziwa yamoto kidogo katika cheese na changanya vizuri.  Kisha ingandamize vizuri ikae sawa katika bakuli.
 4. Katakata Tambi za Kataif ndogo ndogo kwa mkono na kuzichambua kama urefu wa 3 cm na kuziweka zote katika bakuli.

 

 1. Pasha moto siagi au samli katika Microwave. Nyunyiza katika Kataif uliyoichambua katika bakuli itaipa rangi ya dhahabu.

 

 1. Sasa weka Tambi za Kataif juu ya cheese uliyokwishaweka katika bakuli ya Pyrex na ieneze vizuri kote huku unaigandamiza katika cheese ili igande humo.   

 

 1. Pika ndani ya oven kwa dakika  20- 25   katika moto wa 300- 350  Deg au  mpaka uanze kuona imebadilika rangu kama ya dhahabu kidogo.
 2. Itoe katika oven iweke nje ipowe.
 3. Sasa pika shira   kwa kuchemsha maji na sukari na ipike mpaka shira iwe nzito kidogo sio sana.  Weka Zaafarani uliyoiroweka na maji kidogo. Unaweza kuongeza rangi ya machungwa ukipenda kuipa rangi zaidi. 

 

 1. Mwagia shira juu ya Kunafa. Ikate kate vipande vya mraba (square) kwenye bakuli.       

 

Na sasa iko tayari kuila. 

 

KIDOKEZO  (TIPS)

Inapendeza kuila vugu vugu.


 

 Rudi juu

PUDINI YA NAZI

 

        3 vikombe vya maziwa

        1 kikombe cha unga wa mahindi

        kikombe cha sukari ya hudhurungi (brown sugar)

        1/3 kikombe cha zabibu

        kijiko cha chai cha vanila

        kijiko cha chai cha iliki iliyosagwa

        2 vijiko vya kulia vya siagi

        kikombe cha nazi iliyokunwa yenye sukari. (Sweetened shredded coconut)

 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.

 1. Pasha moto maziwa kwenye sufuria kisha mimina unga wa mahindi ndani yake na ukoroge.
 2. Ongezea sukari, vanilla, iliki, na siagi. Koroga mpaka ichemke kisha upunguze moto huku unakoroga mara kwa mara mpaka mchanganyiko uwe mzito na maziwa yote yawe yamekwisha. Epua na uwache ipoe kidogo.
 3. Chukua chombo cha kumiminia ambacho kina urembo (kama kwenye picha). Kipake siagi alafu unyunyize kikombe cha ile nazi iliyokunwa.
 4. Mimina ile pudini ndani ya hicho chombo na uweke ndani ya friji siku moja ili ipate kushikana.
 5. Ukiwa tayari kupakuwa, toa pudini kwa makini uweke kwenye sahani nzuri. Nyunyizia ile nazi iliyobaki kupambia

 Rudi juu

 

KEKI YA JIBINI (Cheese Cake) - (Na Ummu Sumayyah)

 

 VIPIMO

Malai ya Jibini (Cream Cheese)               2x 450g
Sukari                                                         1/2 Kikombe
Mayai                                                       2
Unga wa ngano                                       1 Kijiko cha chai
Mtindi (yogurt)                                         1/2 Kikombe cha chai
Ukoko wa tayari  (ready crust)                2
Mananasi ya kopo                                  1
Kastadi ya unga                                     1 Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.    Washa oveni 350F.

2.    Kwenye bakuli la mashine, changanya malai ya jibini, sukari, mtindi na unga upige hadi ichanganyike vizuri.

3.    Kisha tia mayai na upige kidogo.

4.    Ikisha changanyika vizuri mimina juu ya ule ukoko (crust) na utandaze kila kipembe.

5.    Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 15, kisha weka moto wa 300F na uchome kwa muda wa saa moja.

6.    Ikishaiva iache ipoe na huku uitayarishie sosi yake.

7.    Katika kisufuria, tia ile juisi ya mananasi utakayoitoa kwenye kopo, pamoja na kastadi na uweke moto mdogo huku unakoroga hadi iwe nzito.

8.    Mimina juu ya Keki Ya Jibini na upange mananasi. Ukipenda weka cheri au jelly katikati ya duara ya mananasi.

9.    Iweke kwenye friji ipate baridi na itakuwa tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO: Unaweza ukagawanya vipimo mara mbili ukatoa keki moja.


 Rudi juu

 

KEKI YA KAROTI - (Na Ummu Sumayyah)

 

VIPIMO
Unga                                           1 Kikombe cha chai
Baking soda                                1 Kijiko cha chai
Iliki ya unga                                1/2 Kijiko cha chai
Chumvi                                       1/4 Kijiko cha chai
Mayai                                          2
Mafuta                                            1/4  Kikombe cha chai
Sukari                                         1/2  Kikombe cha chai
Sukari ya hudhurungi

(brown sugar)                             1/3 Kikombe cha chai

 Mtindi (yogurt)                           1/3 Kikombe cha chai
Karoti iliyokaruzwa                    1 Kikombe cha chai (kama karoti 2)

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.    Washa oveni moto wa 350F.

2.    Paka mafuta chombo utakayopikia keki, kisha nyunyiza unga na gonga iliyozidi.

3.    Kwenye bakuli la kiasi, changanya pamoja unga, baking soda, iliki, na chumvi weka kando.

4.    Katika bakuli nyengine, piga mayai, sukari, mtindi, na mafuta mpaka ilainike.

5.    Polepole changanya mchanganyiko wa mayai kwenye wa unga hadi ilainike; kisha tia karoti.

6.    Mimina kwenye chombo uliyo tayarisha na uvumbike kwa dakika 40 - 45.

7.    Kisha iache ipoe kwenye sufuria dakika 15 halafu pindua na iache ipoe kabisa.

8.    Tengeneza sukari laini (icing sugar) 1/2 kikombe na vijiko 2 vya maji na unyunyizie juu; na ikisha kauka itakuwa tayari kuliwa.

 

 Rudi juu

 

 

KEKI YA  SEMOLINA NA JOZI  (WALNUT)

VIPIMO

 

Mayai                                                  5

Sukari                                                 2 Vikombe vya chai

Mafuta                                                2 Vikombe vya chai

Maziwa                                               2 Vikombe vya chai

Semolina                                            2 vikombe vya chai

Baking powder                                   3 Vijiko vya chai

Jozi zilizosagwa (Walnuts)                4 Vikombe vya chai

Ganda la ndimu iliyokaruzwa            1

Unga                                                 kuzidi kidogo kikombe cha chai  

 

SHIRA 

Sukari                                               4 Vikombe vya chai 

Mai                                                   4 Vikombe vya chai

Ndimu                                              3 Slesi

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

 1. Washa oveni moto wa 300F.
 2. Kwenye bakuli kubwa, changanya vizuri vipimo vyote pamoja isipokuwa kikombe kimoja cha jozi (walnuts), ya kunyunyizia juu kupambia.
 3. Mimina mchanganyiko kwenye chombo cha kuvumbika.
 4. Vumbika (bake) kwa muda wa dakika 45 au zaidi hadi iwive.
 5. Ipike shira kwa kuiacha ichemke dakika 1.
 6. Kisha mimina juu ya keki iliyokwishaiva, na unyunyizie ile jozi iliyobaki
 7. Iache ipoe kabisa kabla ya kuandaa.

 KIDOKEZO: Inapendeza kuliwa ikiwa baridi


 Rudi juu

 

BASBUSA - (Shaam)

 

VIPIMO                                           

 Unga wa Semolina                                 2 Vikombe

Siagi (butter) au samli                             3/4 kikombe

Sukari                                                     3/4 kikombe

Mtindi (Yoghurt au buttermilk)                1 1/4 kikombe

Vanila                                                     1-2 kijiko cha chai

Baking powder                                       1 kijiko cha chai

Baking soda                                           1 1/2 kijiko cha chai

 

Lozi zilizomenywa maganda kwa ajili ya kupambia. 

 

SHIRA

Sukari                                        1 kikombe

Maji                                            1 kikombe

Ndimu ya maji                           1 kijiko cha chai

Pika shira mapema. Chemsha kwa muda wa dakika 20-25 itakapopoa iwe nzito kidogo sio nyepesi sana.

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 1. Washa oveni moto wa 350ºF
 2. Yayusha siagi au samli na iache ipowe.
 3. Changanya sukari na mtindi katika bakuli kubwa.
 4. Changanya semolina, vanila, baking powder, baking soda katika bakuli jengine.
 5. Tia mchanganyiko wa semolina katika bakuli lenye mchanganyiko wa sukari na mtindi na changanya vizuri.
 6. Paka siagi katika sinia ya oveni (baking tray) ya saizi 11" x 7 " au 13" x 9" na tandaza mchanganyiko.
 7. Weka alama ya kukata vipande vipande vya mraba (square) na katika kila kipande weka lozi moja juu yake kupambia.
 8. Iache kwa muda wa dakika 15-20 kabla ya kuipika.
 9. Pika (bake) kwa muda wa dakika 30 au zaidi kidogo hadi iwive na igeuke rangi.
 10. Epua katika oveni na mwagia shira wakati bado imoto na shira iwe iliyopoa baridi.

 

KIDOKEZO:

Ikiwa basbusa ni imoto basi shira iwe baridi, na ikiwa basbusa ni ibaridi basi shira iwe imoto.


 Rudi juu

 

PURI

 

 

VIPIMO

Unga                                                        3 Vikombe

Mafuta ya zaituni au ya kawaida             kikombe

Chumvi                                                    kiasi

Maji ya dafu dafu                                     kikombe takriban

Mafuta ya kukaangia katika karai       

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

 1. Changanya vitu vyote katika bakuli, kisha ukande unga uwe kama wa chapati. Ikibidi uongoze maji au unga ongeza kwani inategemea na mafuta utakayotumia.
 2. Fanya madonge madogo madogo, kisha yafunike kwa kwa mfuko wa plastiki au kitamba yasipate upepo kwa muda wa dakika 15-20
 3. Pasha moto mafuta huku unasukuma madonge yawe kiasi tu.
 4. Kaanga madonge ukitia moja moja au mawili mawili inategemea na ukubwa wa karai. Kaanga hadi yafure na kubadilika rangi.
 5. Epua na yatie katika chujio yatoke mafuta yakiwa tayari kuliwa.

 

KIDOKEZO:

 

Puri nzuri kuliwa na kuku wa kuchoma na sosi zake kama sosi ya ukwaju.


 Rudi juu

 

VIBIBI

 

VIPIMO

Mchele                                                       2 Vikombe

Tui la nazi                                                  1 1/2 Kikombe

Mafuta                                                       1 kijiko cha supu

Hamira                                                       2 Vijiko vya chai

Unga wa ngano                                        1 kijiko cha supu

Hiliki                                                           kiasi upendavyo

Sukari                                                        au 1 Kikombe

  

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

 1. Osha na roweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
 2. Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari, ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
 3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike, kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure.
 4. Ukishafura, mimina sukari na changanya vizuri; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
 5. Weka chuma kipate moto.
 6. Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
 7. Utazame ikishaiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
 8. Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.

 

KIDOKEZO: 

Unaweza kutumia chuma kisichoganda (non stick); nacho hakitaraji kutiwa mafuta.


 Rudi juu

 

MKATE WA KIFARANSA (french toast)

 

VIPIMO
 
 
Mayai                                         6
 Maziwa                                      11/2 Vikombe vya chai
Vanilla/iliki                                 Kidogo
 Mdalasini ya unga                     1/4 -1/2 Kijiko cha chai
 Kungu manga(nutmeg)             Kidogo
 Ganda la ndimu iliyokaruzwa       1 kijiko cha supu
 (lemon zest)
 Maji ya machungwa                     1/4 Kikombe cha chai
 sukari                                         1 Kijiko cha supu
 Mkate wa slesi                            6

 
 
 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
   
1}
Changanya pamoja vipimo vyote isipokuwa mkate kwenye bakuli; weka kando.
 2} Panga mikate katika chombo kikubwa (trei), kisha mimina ule mchanganyiko wa mayai juu yake na iache irowanike dakika 5 hivi.
3} Weka chuma kipate moto, kisha tia siagi au/na mafuta na upange mikate kadha kama itakavyotosha kwenye chuma cha kuchomea.
4} Iwche hadi iive na kuwa rangi ya dhahabu, kisha geuza upande wa pili na endelea hivyo hivyo mpaka umalize mikate yote.
5} Panga katika sahani na itakuwa tayari kuliwa na shira ya matunda kama maple syrup.

 


 

 Rudi juu

VIKEKI VIDOGO  VYA CHENGA ZA SHAYIRI  - (OATMEAL MUFFINS)

 

 

 VIPIMO

 

Unga                                           2 Vikombe

Chenga za shayiri (oatmeal)       1Kikombe

Baking Powder                            1 Kijiko Cha Supu

Baking Soda                                1/2 Kijiko Cha Chai

Chumvi                                        1/2 Kijiko Cha Chai

Sukari Ya Buni  (Brown Sugar)   1 Kikombe

Mdalasini                                     1 Kijiko Cha Chai

Kungu manga (nutmeg)              1/2 Kijiko Cha Chai

Mayai                                           2

Mafuta                                         1/2 Kikombe

Mtindi (yogurt)                             11/2 Vikombe

Vanilla                                         1 Kijiko Cha Chai

Karoti Ziliokunwa (grated)           1 Kikombe(Karoti 3)

 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.         Chunga pamoja unga, oatmeal, baking powder, baking soda, chumvi, sukari ya buni, mdalasini na kungu manga.

2.         Changanya mayai, mafuta, mtindi na vanilla kwenye bakuli. Tia karoti kisha ule mchanganyiko wa unga.

3.         Chota mchanganyiko kwa kijiko tia ndani ya treya maalum ya kupikia muffins/cupcakes.

4.         Pika (bake) katika oveni lenye moto wa 350F kwa dakika 30.

 Rudi juu

 

 

PAI YA KUKU (CHICKEN PIE)

 

VIPIMO

Unga wa kitobosha (puff pastry)                   397-400 gm

Nyama ya kuku bila ya mifupa                      ratili (LB)

Kabichi iliyokatwa nyembamba

nyembamba                                                  2 Vikombe vya chai              

Thomu/Tangawizi iliyosagwa                        1 kijiko cha chakula

Chumvi                                                          kiasi

Pili pili manga                                                1 kijiko cha chakula

Jirah (bizari ya pilau)                                     1 kijiko cha chai

Mdalasini                                                       1 kijiko cha chai

Dania (corriander powder)                            1 kijiko cha chai

Ndimu au limau                                             2 Vijiko vya chakula

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Kama unga wa kitobosha (puff-pastry) uko katika barafu toa mapema kidogo.

2.      Washa jiko la oveni moto wa kiasi cha kiwango 375-400  Deg.

3.      Kata nyama ya kuku vipande vipande kisha itie kwenye sufuria na tia ndani yake, thomu/tangawazi, chumvi, pilipili manga, jirah, mdalasini, dania na ndimu. 

4.      Mpike kuku kwa moto mdogo mdogo hadi awive. Akihitaji maji, tia kidogo tu kiasi cha kumpika awive asibakie na maji. 

5.      Epua na chambua kuku. (Unaweze kutumia sehemu ya kuku ya mifupa, hivyo itabidi uchambue na kutoa mifupa pembeni).

6.      Sukuma unga wa kitobosha (puff-pastry). (Ukipenda kata madonge mawili zitokee pai mbili).

7.      Kuku atakuwa ameshapoa, mchanganye na kabichi vizuri ongeza vikolezo ukipenda kama chumvi, pilipili manga na ndimu.

8.      Weka mchanganyiko wa kuku na kabichi katikakati katika unga uliosukuma na kata kama miba ya samaki (kama ilivyo katika picha)

9.      Suka kufunika vizuri kuku, huku unabana msuko ili ugandane. 

10.   Ziweke pai katika trei ya oveni iliyopakwa siagi kidogo.

11.   Pika katika oven ambalo litakuwa tayari limeshashika moto unaohitajika. Pika hadi zigeuke rangi na ziwive.

12.   Epua, ziweke katika sahani ya kupakulia zikiwa tayari.


 

 Rudi juu

KEKI YA NANASI

  

VIPIMO 
 

Unga                                                        2 vikombe vya chai 

Sukari                                                      1 kikombe cha chai 

Mafuta                                                     1 kikombe cha chai 

Baking powder                                       2 vijiko vya chai 

Siagi                                                         kikombe cha chai 

Mayai                                                      6 

Sukari ya hudhurungi (brown)            1   kikombe cha chai 

Manasi ya kopo yaliyokatwa duara    1 kopo 
  

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
 

1.      Unayeyusha sukari ya hudhurungi pamoja na siagi. Ikishayeyuka vizuri unamimina kwenye sufuria au trei ya kuchomea keki.

2.      Panga vipande vya nanasi kwenye hiyo sufuria/trei. Weka pembeni. Ukipenda katikati ya duara ndogo ya nanasi weka cheri moja.

3.      Kwenye bakuli la kuchanganyia keki la mashine, piga mayai, sukari, vanilla mpaka iwe kama malai (crme) na nzito.

4.      Mimina unga pamoja na baking powder, piga kidogo, mwisho mimina mafuta.

5.      Mimina huo mchanganyiko kwenye sufuria/trei uliyopanga vipande vya nanasi, tayari kuchoma.

6.      Weka moto 180 C choma kwa muda wa dakika 30 35.

7.      Ikishaiva, acha ipowe kwa muda wa dakika 7, mimina chini juu kwenya sahani, tayari kwa kuliwa.

KIDOKEZO: Ukipenda tengeneza kastadi umimine juu yake iwe kama 'Kitindamlo' (dessert)


 

KEKI ZA VIKOMBE ZA NAZI - (COCONUT MUFFINS)

 

 

VIPIMO

 

Unga                                         kikombe

Sukari                                       kikombe

Siagi (margarine)                    1 kikombe

Mayai                                       3

Baking powder                          kijicko cha chai

Maziwa mazito                         kopo 1 (285ml)

Nazi (machicha)                      200 gms

Vanilla                                      kijiko cha chai teaspoon

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Tia kwenye bakuli siagi na sukari piga kwa mashine mpaka iwe laini kama malai (Cream)

2.      Tia mayai piga vizuri.

3.      Tia unga na baking powder.

4.      Tia nazi.

5.      Tia maziwa na vanilla, piga kidogo.

6.      Tumia treya za vishimo vya duara (muffin tray), weka karatasi zake, kisha tia mchanganyiko wa keki kiasi usijaze katika vishimo.

7.      Choma (bake) katika moto wa 325 C

8.      Choma kwa muda wa dakika 10 15 mpaka iwe rangi ya udongo kidogo (brown).

9.      Epua na tayari kwa kuliwa

 


 Rudi juu

 


MKATE WA NYAMA

  

VIPIMO

Nyama ya kusaga                                    LB

Kitunguu maji kilichokatwa kidogo          1

kidogo (chopped)

Thomu na tangawizi iliyosagawa            1 Kijiko cha chai                   

Pilipili manga ya unga                             1 kijiko cha chai

Unga wa ngano                                       2-3 vikombe

Hamira                                                    1 au 1 kijiko cha chakula 

Chumvi                                                    kijiko cha chai

Mayai                                                      5

Siagi                                                        225g

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Tia katika nyama thomu, tangawizi, chumvi, pilipili manga, (ukipenda bizari zako nyingine), vitunguu, kisha iache kama muda wa saa moja ili vikolee hivyo vitu kwenye nyama.

2.      Ikaushe nyama mpaka iwive kama nyama ya sambusa.

3.      Vunja mayai manne na la tano liache pembeni. Yatie kwenye bakuli upige kama kiasi cha dakika mbili.

4.      Tia unga kwenye mayai na changanya vizuri kisha tia hamira na chumvi halafu changanya kwa sekunde chache tu.

5.      Halafu tia siagi kwenye bakuli la unga na uchanganye vizuri mpaka uchanganyike vizuri yaani lifanyike donge halafu uzunguushie karatasi ya plastiki (plastic wrap) au mfuko wa plastiki, na uweke kwenye friji kwa usiku mzima ulale yaani ni vizuri ulale siku nzima ili ladha yake itokeze.

6.      Siku ya pili toa unga kutoka kwenye friji na uweke kwa muda wa saa moja ili ukande kwa kutumia siagi na lile yai moja lililobakia mpaka uwe laini.

7.      Sukuma kwa kifimbo kama unataka kufanya chapati, yaani utandaze kwa kifimbo halafu ukishakua bapa (flat) chukua nyama yako itandaze juu ya ule mkate yaani nyunyiza kwenye ule unga ulioutandaza.

8.      Kunja unga (roll) na nyama yake ukisha unauzunguusha duara ili kuutia kwenye treya yako ya kubake unauacha uumuke.

9.      Ukishakuumuka unapaka siagi au yai juu yake ukisha unaupika katika jiko (oven) kama unavyopika mikate mengine kwa moto wa 350 Deg. Na kwa muda wa kama dakika 20 au zaidi hadi uwive.

 

Kidokezo

Ni vizuri kuliwa kwa chai au juice


 Rudi juu

 

MAANDAZI YA KUPAMBIA.

 

VIPIMO 

Unga                 3 Magi

Sukari               1 Kikombe

Mayai                2

Hamira              2 Vijiko vya chakula

Hiliki                  1 Kijiko cha chai

Nazi                  1 Ya kopo

Samli                2 Vijiko vya chakula (jaza)

Ufuta               3 Vijiko vya chakula 
 
 
JINSI YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 
  

1.      Unatia hamira kwenye kibakuli na maji kama robo kikombe hivi ikisha unaichanganya mpaka ichanganyike na unaiweka pembeni.  

2.      Unautia unga kwenye bakuli au sinia ikisha unatia na sukari na hiliki, unapasha moto samli na unaitia ikisha unauchanganya unga na samli mpaka uchanganyike uzuri.  

3.      Unapiga mayai kwenye bakuli unayatia, unauchanganya tena halafu unatia na ile hamira ulokwisha ivuruga, huku unaendelea kuuchanganya. 

4.      Hapo sasa ndio unachukuwa ile nazi ya kopo unaitia kidogo kidogo huku unaukanda mpaka ulainike. Unga wa maandazi haya unakuwa mlaini zaidi kuliko maandazi ya mafuta.  Kama nazi haitatosha unaweza kuongeza maziwa au hata maji kidogo mpaka ulainike vizuri unga.   

5.      Ukishamaliza kuukanda utie kwenye bakuli na uwache kwa dakika 10, halafu uchanganye tena bila kuutia kitu chochote. 

6.      Halafu chukuwa treya ipakae mafuta au samli, kisha chukuwa unga usokote kama unavouona hapo juu, au kama unataka kuufanya staili nyingine pia unaweza, unausokota mpaka unamaliza unga wote.

7.      Ukimaliza nyunyiza ufuta juu ya maandazi ulokwisha yasokota, halafu tia treya ya maandazi ndani ya jiko (oven) lakini usiwashe moto, subiri mpaka maandazi yaumuke vizuri.  

8.      Maandazi yakisha kuumuka vizuri sana, washa moto (bake) kwenye jiko na uweke namba 350 kwa muda wa dakika 15, na baada ya hapo punguza moto weka 300 mpaka ukishakuyaona yamewiva. 

9.      Yakiwiva yatoe kwenye jiko na uyapake mafuta juu kidogo ili yalainike na uyawache yapoe, na yakishapoa yatakuwa tayari kuliwa. 

 


 Rudi juu

 

KEKI ZA VIKOMBE

  

 VIPIMO

Unga wa ngano              vikombe 2-3

Mayai                             6

Maziwa                          kikombe 1

Sukari                            kikombe 1

Siagi                              kikombe 1

Baking powder              vijiko vya chai 2-3 (kijiko 1 kwa kikombe cha unga1)

Vanilla                           kijiko cha chai 1

Rose essence               kijiko cha chai robo (kiasi unavyotaka harufu ijitokeze)

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Saga siagi, sukari, mayai na essence ya vanilla na rose

2.      Ikishasagika tia unga na maziwa koroga tena.

3.      Mwisho tia baking powder na koroga mpaka ichanganyike.

4.      Washa oven lako moto wa 350F kwa dakika 2-3.

5.      Chukua treya maalum ya kupikia cupcakes / muffins, tia karatasi za duara maalum za kupikia keki hizi kwenye kila duara la treya.(huna haja ya kupaka mafuta kwenye treya)

6.      Kisha tumia kijiko kikubwa chota mchanganyiko huo wa keki na tia ndani ya karatasi hizo za duara kiasi cha robo tatu (3/4) yaani usijaze mpaka juu.

7.      ukimaliza kuvijaza vyote tia kwenye oven kwa muda wa dakika 20 25.

8.      zitoe panga kwenye sahani ziache zipoe kidogo na tayari kuliwa na chai au kuwafungia watoto shuleni kama snack


 Rudi juu

 

MKATE WA MAYAI

 

 VIPIMO

 

Mayai                                        4

Sukari                                         Kikombe

Unga wa Ngano                        Vijiko 5 vya chakula

Hiliki ya kusaga                           kijiko cha chai

Baking powder                            Kijiko cha chai

Zabibu kavu                                kikombe

  

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 

 

1.      Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, hiliki na vunja juu yake mayai yote 4.

 

2.      Changanya sukari, hiliki na mayai   kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.

 

3.      Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto.

 

4.      Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge.

 

5.      Mimina unga ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.

 

6.      Tupia zabibu juu ya mchanganyiko wako.

 

7.      Ingiza sufuria  ndani ya jiko (oven) kwa dakika 20 kisha utoe.

 

8.      Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate   kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.

 

9.      Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.   


 Rudi juu

 

KEKI YA TENDE

 

VIPIMO

Unga                                                3 kikombe

Baking powder                                 3 Vijiko vya chai

Sukari                                               Kikombe

Tende iliyokatwa ndogo ndogo       2 vikombe

Maji yamoto                                     2 vikombe

Siagi                                                4 Vijiko vya supu (au vikombe 2 vya kahawa)

Mayai                                              2

Cream                                            300 gm (au vikombe2 vya Kahawa)

Tangawizi ya powder                      2 Vijiko vya chai

Kungu manga                                 1 kijiko cha chai

Mdalasini                                        1  kijiko cha chai

Hiliki                                                 kijiko cha chai

Vanilla                                             4  vijiko vya chai

 

VIPIMO VYA KARAMEL

Sukari ya buni (brown sugar)              5 Vijiko vya supu

Siagi                                                 6 Vijiko vya supu

Lozi zilizomenywa na kukatwa

Nyembamba                                      1 kikombe

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 Tia maji ya moto katika tende kuiroweka kidogo.

1.      Changanya unga na baking powder vizuri katika bakuli.

2.      Tia vitu vyote vingine na uchanganye vizuri.

3.      Mimina katika bati la duara la kupikia keki ulilolipaka siagi kidogo la kiasi ya 10 in dia x 2 in    

4.      Ipikie (bake) katika moto wa 300 kwa muda wa kama saa au zaidi hadi iwive.

5.      Iweke katika sahani au bakuli la keki na mwagia karamel juu yake, kisha haraka upambie lozi.

 

Namna ya kutayarisha Karamel

Yayusha siagi katika sufuria ndogo au frying pan kisha tia sukari ya brown.

Inapoyayuka, mwagia katika keki.


 Rudi juu

 

MKATE WA UFUTA

 

 

VIPIMO:   (vya kutokea mikate 6)

Unga                                                 3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Tui la nazi au maziwa                       2  Vikombe vikubwa (Mugs)

Hamira                                              1 Kijiko cha supu

Chumvi                                             Kiasi

Sukari                                               1 kijiko cha chai

Yai                                                    1

Ufuta                                                Kiasi

Mafuta au samli Ya kupakia mkate   Kiasi

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Changanya pamoja unga, nazi, chumvi, hamira, sukari na yai.  Hakikisha unga wote umetoka madonge na umevurugika vizuri uwe laini. (uwe maji maji kama wa kaimati lakini unakuwa mzito kidogo kuliko wa kaimati).

2.      Usubiri uumuke (Ufure)

 

JINSI YA KUCHOMA MIKATE:

1.      Hakikisha chuma cha kuchomea kiwe kinagandisha vizuri (Kisiwe non- stick) na pia kisiwe kilichopikiwa mafuta.

2.      Weka chuma kwenye moto, kikipata moto rushia maji ya chumvi kidogo halafu tia unga kiasi kama kiganja kimoja cha mkono, utawanye vizuri kwa vidole halafu nyunyizia ufuta juu yake.

3.      Ukianza kuwa mkavu nyanyua chuma   kifudikize kwenye moto mpaka mkate wako uwe rangi ya dhahabu.

4.      Toa kwenye chuma kwa kutumia kisu.

5.      Paka samli au mafuta juu ya mkate kwa tumia brush.

6.      Endelea hivyo hivyo mpaka umalizie unga wote.

 


 Rudi juu

 

KHALYAT AN-NAHL   (MZINGA WA NYUKI)

 

 

VIPIMO

Unga                                                Vikombe 3 1/2 visivyojaa

Maziwa ya maji                                Vikombe 1

Maji                                                  Kikombe 1/2

Yai                                                   1

Sukari                                               Vijiko 2 1/2 vya supu

Mafuta                                              Kikombe 1/2

Hamira                                             Kijiko 1/2 cha chai

Chumvi                                            robo kijiko cha chai

Cheese ya Cream                           Kiasi utakavyotumia kujaza

 

Shira

Sukari                                                Vikombe 2

Maji                                                    Kikombe 1

Zaafarani                                            nusu kijiko cha chai (iroweke)

Ipikie shira lakini isiwe nzito.

 

Namna ya kutayarisha na kupika

1.      Changanya vitu vyote hivyo isipokuwa cream cheese.

2.      Kanda kidogo tu kulainisha unga uwe mlaini kama mfano unga wa maandazi. 

3.      Pakaza siagi katika sinia ya round utakayopikia 

4.      Fanya viduara vidogo vidogo na tia ndani yake cheese ya cream kwa kutumia   kijiko cha chai, na vifunge viduwara vizuri na kuvipanga katika sinia bila ya kuwacha nafasi.

5.      Iwache ifure

6.      Ipikie katika oven moto wa chini kwanza katika 350 Deg, kwa muda wa baina dakika  20  na 25 Kisha washa moto wa juu kidogo tu uwive kwa juu.

7.      Toa katika over na mwagia shira kama ifuatavyo.

 

v  Kama ni shira iliyopowa basi mwagia juu ya mkate uliomoto

v  Kama ni shira imoto basi subiri mkate upowe.  Yaani mojawapo iwe moto au baridi.

 


 

 Rudi juu

KEKI YA MAZIWA

 

VIPIMO

Siagi                                                     Kikombe 1

Sukari                                                   Kikombe 1 (usijaze sana)

Unga                                                    Vikombe 2 (usijaze sana)

Maziwa                                                Kikombe 1

Mayai                                                  6

Baking Powder                                   1 Tablespoon

Arki rose                                             kidogo

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.

2.      Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.

3.      Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.

4.      Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri                   (unaweza kufanya bila ya mashine)

5.      Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako.

6.      Ipike (Bake) 300 Deg C 

 


 Rudi juu

 

Maandazi

 

 VIPIMO

Unga                                                                5 Vikombe

Tui la Nazi zito vugu vugu                               1 kikombe

Sukari                                                                 3/4 kikombe cha chai

Samli iliyoyayushwa au mafuta                      3 vijiko vya Supu

Hamirah                                                           2 Vijiko vya Supu

Hiliki                                                                1/2 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia                                 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:

 

1.      Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.

2.      Pasha samli moto

3.      Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na   samli ikiwa bado moto moto.

4.      Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. Kanda unga mpaka uwe laini.

5.      Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke.

6.      *Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12.  Ukipenda mepesi fanya madonge 15  

7.      Madonge yakifura, sukuma kama chapati kisha ukate mara nne kama kwenye picha. Endelea kufanya hivyo na madonge yote. Yawache maandazi yafure tena baada ya kukata kama dakika 15 hivi.  

8.      Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.

 

9.      Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari.

 

VIDOKEZO: KUHIFADHI MAANDAZI

 

v  Unaweza kuweka unga wa maandazi uliyokwisha kuyakata ndani ya freezer yakisha umukua ikiwa unataka kutumia siku nyengine. Tumia waxed paper na unga wa kutosha kuweka katikati ya maandazi ili yasishikane unapoya freeze kwanza katika freezer. Yakishika barafu, toa na yafunike kwa wax paper kiasi kama matano pamoja na uyatie katika freezer bags. Ukitaka kukaanga maandazi siku nyengine, toa maandazi mapema kidogo yatoke barafu kidogo tu. Pasha mafuta moto kwenye karai na kanga maandazi.

  

v  Vile vile unaweza kuyapika kabisa na kuweka katika freezer bags, ukitaka kutumia ni kuyatoa tu na kupasha moto katika Microwave.

 


 Rudi juu

 

VITUMBUA

 

VIPIMO 

 

1 Kikombe cha mchele.

1 Kijiko cha kulia cha unga wa ngano.

3/4-1 Kikombe cha tui la nazi zito.

2 Mayai.

Kijiko cha chai cha hamira.

1/2- 3/4 kikombe cha sukari.  

Iliki kiasi upendacho.

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:

 

1.      Osha na kuroweka mchele ndani ya maji ya baridi masaa manane au siku moja.

2.      Mimina vifaa vyote ispokuwa sukari, ndani ya blender na usage mpaka mchele uwe umesagika kabisa.

3.      Mimina sukari ndani ya mchanganyiko na usage tena kidogo tu.

4.      Mimina mchanganyiko ndani ya bakuli na ufinike. Weka bakuli mahali penye joto ili mchanganyiko uuumuke.

5.      Mchanganyiko ukisha umuka, weka karai kwenye moto.

6.      Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.

7.      Mimina mchanganyiko kiasi kwenye karai kulingana na kikarai unachotumia.

8.      Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.

9.      Panga kwenye sahani. Unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.

 


 Rudi juu

 

KEKI YA MARMAR (MARBLE CAKE)

 

            2/3  kikombe cha siagi iliyolainika

        2 2/3 vikombe vya sukari

        4 mayai

        2 vijiko vya chai vya vanilla

        3 vikombe vya unga wa ngano

        1 kijiko cha chai cha baking soda

        1/2 kijiko cha chai cha chumvi

        1 1/2 vikombe vya sour cream

        1/2 kikombe cha cocoa isio na sukari (unsweetened)

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Washa oven moto wa  350F. Paka siagi kwenye chombo cha kuvumbika(bake), kisha unyunyize unga kidogo tu. Weka kando.

 

2.      Kwenye bakuli kubwa, changanya sukari na siagi ukitumia mchapo kwa muda wa dakika kama mbili hivi. Mimina yai moja moja na vanila huku unachanganya vizuri.

 

3.      Ongezea unga, baking soda na chumvi ukipokezana na sour cream. Toa kama 2 vikombe vya mchanganyiko uweke kando.

 

4.      Kwenye mchanganyiko uliyobaki, mimina ile cocoa na ukoroge vizuri. Mimina nusu ya ule mchanganyiko mweupe ulioweka kando, kwenye chombo cha kuvumbika. Kisha mimina juu yake nusu ya ule mchanganyiko wenye cocoa. Pitisha kisu kwenye mchanganyiko ili utengeneze alama ya marmar (marble). Mimina tena mchanganyiko mweupe uliyobaki, juu yake na umimine ule mchanganyiko wa cocoa uliobaki pia, kisha upitishe tena kisu.

 

5.      Vumbika kwenye oven kwa muda wa dakika 50 au 60 mpaka keki iwe tayari.

 

6.      Iwache ipoe kabisa kabla ya kuandaa

 

 


 Rudi juu

 

KEKI YA NDIZI NA NAZI

 

        Kikombe Cha Siagi Laini

        Kikombe Cha Creame Cheese Laini

        1 Kikombe Cha Sukari

        5 Mayai Yaliyogawanywa Kiini Mbali Na Ute Mbali

        1 Vikombe Vya Ndizi Zilizosagwa

        2 Vijiko Vya Chai Vya Harufu Ya Lozi (Almond Extract)

        Kikombe Cha Tui La Nazi

        Kikombe Cha Nazi Iliyokunwa (Unsweetened Shredded Coconut)

        2 Vikombe Vya Unga Wa Ngano

        1/3 Kikombe Cha Cornstarch

        1 Kijiko Cha Chai Cha Baking Poda

        1 Vijiko Vya Chai Vya Baking Soda

        Kijiko Cha Chai Cha Chumvi

        Sukari Ya Unga (Sio Lazima)

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.

 

1.      Kwenye bakuli kubwa ukitumia michapo, piga siagi, cream cheese, na sukari pamoja mpaka iwe laini na nyepesi.

2.      Ongezea viini vya mayai, kimoja kimoja huku unachanganya vizuri.

3.      Mimina ndizi, harufu ya lozi, tui la nazi na nazi iliyokunwa, na ukoroge pamoja.

4.      Chunga (sift) unga, cornstarch, baking poda, baking soda na chumvi kwenye ule mchanganyiko wa ndizi. Changanya vizuri ukihakikisha kuwa unakoroga mpaka chini.

5.      Osha michapo kisha upige ute wa mayai katika bakuli jengine mpaka ufure na kuwa mgumu. (Stiff)

6.      Changanya pole pole na ule mchanganyiko wa ndizi.

7.      Mimina kwenye chombo cha kuvumbika (bake) kilichopakwa siagi. Vumbika kwenye oven lililowashwa kabisa, lenye moto wa 350 kwa muda wa dakika 45. Zima na uwache keki humo ndani kwa muda wa dakika 15 zaidi.

8.         Epua keki na uiwache ipoe. Ukitaka mimina ile sukari ya unga juua yake. 


 Rudi juu

 Rudi juu

 

BISKUTI ZA UFUTA NA JAM - (Na Ummu Ibraahiym)

 

 

VIPIMO                                             

 

Unga                                                          2 Viwili

Sukari ya kusaga                                       1/4 Kikombe

Siagi                                                           250 gms

Jam                                                             kisia

Ufuta                                                          Kisia

Vanilla                                                        1 kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai, sukari na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.

 

2.      Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.

 

3.      Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.

 

4.      Tengeneza viduara vidogo vidogo.

 

5.      Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unynyuzie ufuta.

 

6.      Pika katika moto wa chini 350ºF kwa muda wa dakika 20-25.

 

7.      Tayari kwa kuliwa.

 

 


 Rudi juu

 

BISKUTI ZA MAYAI - (Na Ummu Ibraahiym)

 

VIPIMO

 

Unga                                                   3 Vikombe

Sukari ya unga (icing sugar)               1 Kikombe

Siagi                                                    250 gm

Mayai                                                  3

Vanilla                                                 2 Vijiko vya chai

Baking powder                                    1 Kijiko cha chai

  

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).

 

2.      Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini .

 

3.      Tia unga na baking powder changanya na mwiko.

 

4.      Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.

 

5.      Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.

 

6.      Pika (bake) katika oven moto wa 350F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama

 

 


 Rudi juu

 

BISKUTI ZA KASTADI (Na Ummu Ibraahiym)

  

VIPIMO

 

Unga                                                             6 Vikombe

Sukari ya kusaga                                         2 vikombe

Siagi                                                             500 gm

Baking powder                                             1 Kijiko cha chai

Kastadi                                                         kikombe

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1)      Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).

 

2)      Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli.

 

3)      Tia unga na baking powder na Kastadi.

 

4)      Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray)

 

5)      Pika (bake) katika oven moto wa 350 F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

 


 Rudi juu

 

BISKUTI ZA TENDE  (Na Ummu Waliyd)

 

 VIPIMO

Unga                                                    4 Vikombe vya chai
Sukari ya laini  (icing sugar)                1 Kikombe cha chai
Baking powder                                     2 Vijiko vya chai
Mayai                                                   2
Siagi au margarine                             1 Kikombe cha chai
Vanilla                                                 1 Kijiko cha chai
Maziwa ya kuchanganyia                    kiasi
Tende iliyotolewa koko                       1 Kikombe
ufuta (sasame) kiasi                           1/4  kikombe

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
 

1.    Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine.
 

2.    Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane.

 

3.    Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana.

 

4.    Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika.

 

5.    Vumbika (bake) moto wa 350F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive.

 

6.    Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.


 

 Rudi juu

BISKUTI ZA CHUMVI

 

VIPIMO                          

Unga                                           3 Vikombe vya chai

Siagi                                            250 gms

Baking powder                            3 Vijiko vya chai

Mayai                                          2

Chumvi                                       1 kijiko cha chai

Maziwa                                       1/2 Kikombe

Pilipili manga ya unga                1 Kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream).

2.      Tia Unga, baking powder, pilipili manga.

3.      Tia maziwa.

4.      Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda.

5.      Pika (bake) katika moto wa 350º C usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.


 Rudi juu

 

BISKUTI ZA CORNFLAKES

 

VIPIMO                                           

 

Unga                                                      1 Kikombe

Sukari ya kusaga                                    3/4 Kikombe

Siagi                                                      125 gms

Yai                                                         1

Baking powder                                      1/2 kijiko cha chai

Zabibu kavu                                          1/2 kikombe

Cornflakes iliyovunjwa (crushed)          2 Vikombe

Vanilla                                                   1 kijiko cha chai

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.

2.      Tia baking powder, zabibu na unga na changanya   vizuri.

3.      Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.

4.      Tengeneza viduara vidogo vidogo.

5.      Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni.

6.      Pika katika moto wa 350ºF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.

 

 Rudi juu


 

MITAI

 

 VIPIMO

Unga wa ngano                                 11/2 Kikombe

Baking powder                                  1 Kijiko cha chai

Baking soda                                        Kijiko cha chai

Kungumanga(nutmeg)                      3/4-1 kijiko cha chai

Chumvi                                                kijiko cha chai

Sukari                                                1 kijiko cha supu

Hamira                                               1/2 Kijiko cha supu

Yai                                                      1

Maziwa                                                Kikombe

Mafuta ya kukaangia

 

SHIRA

Sukari                                               1 Kikombe

Maji                                                    Kikombe

Iliki au Mdalasini                                  kijiko cha chai (ya unga)

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari, kungumanga na hamira.

2.      Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.

3.      Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga; na ukande kama unga wa maandazi.

4.      Kisha weka katika bakuli la ufiniko na iwache ifure.

5.      Ikisha fura, sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai.

6.      Pasha moto mafuta na uchome hadi iwe rangi ya dhahabu, upande zote mbili.

7.      Ipikie shira lakini isiwe nzito.

8.      Tia mitai na upepete hadi sukari ienee kote; Na zitakuwa tayari


 Rudi juu

 

VIBISKUTI VYA KUYAYUKA MDOMONI

 

VIPIMO

 

Unga wa cornstarch               1 Kikombe

Unga wa Ngano                      3/4 Kikombe+1 Kijiko Cha Chakula

Chumvi                                   1/4 Kijiko Cha Chai

Siagi  iliolainika                       250gm.

Sukari Ya Icing                       1/2 Kikombe

Vanilla                                     1 kijiko Cha Chai

 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
 

1.      Katika bakuli la kiasi, chunga corn starch, unga na chumvi, weka kando.

2.      Koroga siagi na sukari kutumia mashine mpaka iwe laini.

3.      Weka vanilla, kisha mchanganyiko wa unga na huku unakoroga hadi uwe umeshikamana.

4.      Kanda unga kidogo kisha sukuma kama chapati, lakini sio nyembamba sana.

5.      Kisha tumia kidude cha kutolea design unayotaka na zipange katika treya.

6.      Ziweke kwa firigi kwa muda wa nusu saa,ili zisienee wakati wa kupika.

7.      Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375F kwa muda wa dakika 10-12.

8.      Toa kwenye oven na uwache bisikuti zipowe. Ukipenda chunga sukari ya icing juu kwa umaridadi.

  

KIDOKEZO

 

Unaweza kusaga sukari ya kawaida kwenye blenda ikawa sukari ya icing.

 


 Rudi juu

 

DONATI

 

VIPIMO

Unga                                                2 Magi

Sukari                                               1/3 Kikombe                           

Mayai                                               5

Siagi                                                4 Vijiko vya chakula

Hamira                                            1 Kijiko cha chakula

Baking Powder                               1 Kijiko cha chai

Vanilla                                             1 Kijiko cha chai

Hiliki zilizosagwa                             1 Kijiko cha chai

Sukari ya laini ya unga

(icing sugar)                                  1 Magi

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.       Unavunja mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.
 

2.       Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.
 

3.       Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.
 

4.       Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
 

5.       Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge. 
 

6.       Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe halafu teleka mafuta na uyachome.
 

7.       Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto yarovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu.

 

8.       Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.


 Rudi juu

 

BISKUTI ZA JAM

 

VIPIMO 
Unga                                     2 gilasi

Sukari                                         gilasi

Samli                                         1 gilasi

Mayai                                         2

Baking powder                           2 kijiko vya chai

Vanilla                                       1 kijiko cha chai

Maganda ya chungwa               1 
 
 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA  

1.      Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri.

2.      Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.

3.      Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.

4.      Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.

5.      Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam

6.      Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.

7.      Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.

 


 Rudi juu

 

VISHETI:

 

VIPIMO:

Unga wa Visheti

Unga                                        4 Vikombe vya chai

Siagi                                        1 Kikombe cha chai

Hiliki                                        Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1.      Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.

2.      Changanya vizuri isiwe na madonge.

3.      Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.

4.      Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.

5.      Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .

6.      Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili

7.      Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.

8.      Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

 

Shira: 

Sukari                                    2 Vikombe vya chai

Maji                                       1 Kikombe cha chai

Vanilla                                     Kijiko cha chai

 

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai


 

 Rudi juu

VILEJA VYA KARANGA

  

  VIPIMO

 

Mayai                                            5

Sukari                                           450gm (1 lb)

Unga wa Ngano                           1 kg

Siagi                                             450gm (1 lb)

Baking powder                               Kijiko cha chai

Unga wa Custard                         Vijiko 2 vya chakula

Karanga za kusaga                      250gm

Jam                                               kikombe

 

 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 

 

1.      Chukua bakuli la kiasi, weka sukari na siagi.

 

2.      Changanya sukari na siagi kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ichanganyike na siagi.

 

3.      Vunja yai moja moja na weka kiini chake kwenye mchanganyiko wa sukari na siagi, endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri. Hifadhi ute wa mayai ndani ya kibakuli.

 

4.      Mimina unga wa ngano ndani ya mchanganyiko wako huku ukichanganya. Changanya unga wa custard na baking powder.

 

5.      Tengeneza viduara vidogo vidogo.

 

6.      Vichovye viduara   ndani ya ute wa yai kisha zimwagie unga wa karanga na kuzipanga kwenye tray ya kuchomea.

 

7.      Weka dole gumba kati kati ya kila kiduara na uweke jam.

 

8.      Washa jiko   (oven) 350F na uchome vileja vyako kwa dakika 20.

 

9.      Toa vileja vyako vipoe na uviweke ndani ya sahani tayari kwa kuliwa.

 

 Rudi juu


 

BISKUTI ZA NJUGU/MATUNDA MAKAVU - (ROCK CAKES)

 

 

VIPIMO:

 

Unga                                                         4 Vikombe

Sukari                                                       10 Ounce

Siagi                                                         10 Ounce

Kungu manga ya unga                             2 vijiko vya chai

Maziwa ya maji                                        4 Vijiko vya supu

Matunda makavu/njugu 4 ounce

(kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa,

Cherries na kadhalika                              

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1)       Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.

 

2)       Tia vanilla kungu manga, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)

 

3)       Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.

 

4)       Chota mchanganyiko  na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.

 

5)       Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

  

KIDOKEZO

 

Unaweza kufanya nusu ya vipimo kwani biskuti zinatokea nyingi.

 Rudi juu


 

VIBISKUTI VYA MATUNDA MAKAVU NA CORNFLAKES

 

 

 

VIPIMO

 

Unga                                                             4 Vikombe

Sukari                                                           1 Kikombe

Siagi                                                             454 gms

Mayai                                                            2

Matunda makavu (tende, zabibu, lozi)         1 Kikombe

Vanilla                                                          2 Vijiko vya chai

Cornflakes                                                    kikombe

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy)

 

2.      Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy)

 

3.      Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko.

 

4.      Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed)

 

5.      Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika  moto wa 375 F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.

  

KIDOKEZO

 

Unaweza kufanya nusu yake kwani zinatoka nyingi kipimo hicho.


 Rudi juu

 

VIBISKUTI VYA SIAGI

 

 

VIPIMO

 

Unga                                                         2 Vikombe

Sukari ya icing                                          1 Kikombe

Siagi                                                         250 gm

Yai                                                            1

Vanilla                                                      2 Vijiko vya chai

Baking powder                                          1 Kijiko cha chai

Jam                                                          kikombe

Lozi                                                           kikombe

 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.      Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).

 

2.      Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi (fluffy).

 

3.      Tia unga na baking powder changanya na mwiko.

 

4.      Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia.

 

5.      Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa.

 

6.      Pika (bake) katika oven moto wa 375 F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

 


 Rudi juu

 

BISKUTI ZA TANGAWIZI

                 BISKUTI ZA TANGAWIZI

       2 vikombe vya unga wa ngano

       1 kijiko cha chai cha tangawizi ya unga    

       2 vijiko vya chai baking soda

       1 1/2 vijiko vya chai mdalasini wa unga

       1/2 kijiko cha chai karafuu ya unga

       1/2 kijiko cha chai chumvi

       3/4 kikombe cha vegetable shortening

       1 kikombe cha sukari

       1 yai

       1/4 kikombe molasses

       sukari ya kusukumia

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:

 

1.      Washa oven moto wa 350.

2.      Katika bakuli la kiasi, chunga (sift) unga, tangawizi, baking soda, mdalisini, karafuu na chumvi Katika bakuli kubwa, ukitumia mchapo, piga ile vegetable shortening mpaka iwe laini. Mimina sukari kidogo kidogo huku unapiga mchanganyiko mpaka uwe laini kabisa.

3.      Mimina yai na molasses na upige mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri.  

4.      Mimina ile sukari ya kusukumia kwenye bakuli dogo. Teka kijiko cha chai cha mchanganyiko na ufanye mviringo alafu weka ule mviringo ndani ya bakuli la sukari ili mviringo wote uwe umepata sukari. Endelea kufanya hivyo mpaka mchanganyiko umalizike.

5.      Weka miviringo kwenye sinia ya kuvumbika (baking tray) ukiwacha nchi mbili katikati ya kila mviringo.

6.      Vumbika mpaka biscuti ziwe rangi ya hudhurungi (brown) juu.

7.      Toa kwenye oven na uwache biscuti zipoe kabisa.

8.      Ukitaka kuhifadhi biscuti hizi kwa muda, weka ndani ya chombo ambacho hakipati upepo (airtight).