Suali:

 

Niigawe vipi nyama ya Udh'hiyah. Niigawe sehemu tatu au nne?


Jawabu:

Alhamdulillah

Maulamaa wamependekeza kwa mwenye kuchinja mnyama wa Udh'hiya ale katika nyama hiyo, atowe sadaka na atowe zawadi, na hii inatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema:

"Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri."

Al Hajj 28

Na akasema:

"Na walisheni walio kinai na wanao lazimika kuomba. Ndio kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru."

Al Hajj 36

Imepokelewa kutoka kwa Salamah ibn al-Akwa (Radhiya Llahu Anhum) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu Alayhi Wa Sallam) alisema:

"Kula katika nyama hiyo, nyingine wagawie wenzio na nyingine jiwekee akiba."

Bukhari

Kuwagawia wengine kunaamanisha pia kuwapa zawadi wenye uwezo na kuwapa sadaka wasiokuwa na uwezo.

 

Imepokelewa pia kuwa Bibi Aisha (Radhiya Llahu Anhum) alisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu Alayhi Wa Sallam) alisema:

"Nyingine kula na nyingine jiwekee akiba na nyingine igawe."

Muslim

 

Maulamaa (Mwenyezi Mungu awarehemu) wamekhitalifiana kuhusu kiasi cha kula na cha kutoa zawadi na cha sadaka, na hukmu zake zina wasaa mkubwa, lakini boRadhiya Llahu anhum zaidi ni kuigawa sehemu tatu.

1.     Thuluthi moja uile

2.     Thuluthi ya pili utowe sadaka

3.     Thuluthi ya tatu uwape zawadi sahibu na jiRadhiya Llahu anhumni zako

 

Ile Thuluthi ya kula inaweza kugawiwa ikaliwa na nyingine ikawekwa akiba, hata ikibidi kukaa muda mrefu, muhimu isiharibike na isiwe katika wakati wa ukame na njaa kwani katika wakati huo nyama hairuhusiwi kuwekwa zaidi ya siku tatu, na hii inatokana na hadithi ya Salamah ibn al-Akwa (Radhiya Llahu Anhum) aliposema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu Alayhi Wa Sallam) amesema:

Yeyote katika yenu atakayechinja asibakishe chochote nyumbani kwake katika mnyama huyo zaidi ya siku tatu." Mwaka uliofuata walimuuliza: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llahu Alayhi Wa Sallam), tufanya kama tulivyofanya mwaka uliopita?" Akasema: "Kuleni kidogo, gaweni kidogo na jiwekeeni akiba, kwa sababu mwaka uliopita tulikuwa katika wakati mgumu, na nilikutakeni mwasaidie wenye kuhitaji."

Bukhari na Muslim

 

Katika ruhusa ya kugawa nyama ya Udh'hiya hapana khitilafu yoyote ikiwa mnyama huyo amechinjwa kwa amri au kwa hiari, na pia hapana hitilafu ikiwa mnyama huyo amechinjwa kwa ajili ya mtu anayeishi au aliyekwishafariki, au amechinjwa kwa ajili ya kutimiza usia. Kwa sababu mwenye kuchinja hapa anachukuwa nafasi ya mwenye mnyama. Na kwa sababu mwenye mnyama angekula na angeigawa nyama hiyo na kujiwekea akiba. Na kwa vile hii ndiyo kawaida iliyopo baina ya watu.

Ikiwa mtu amewakilishwa na mwengine kuchinja mnyama wa Udh'hiya na akamtaka ale katika nyama hiyo na nyingine aigawe sadaka au zawadi, au iwe inajulikana kuwa kufanya hivyo ni jambo la kawaida baina yao, basi anaweza kufanya hivyo, ama sivyo itambidi ampe aliyemwakilisha nyama yake atakayekuwa na haki ya kuigawa.

Ni haRadhiya Llahu anhummu kuuza sehemu yoyote ya mnyama ya Udh'hiya, yote Swallah Llahu alayhi wa sallama iwe sehemu ya nyama au sehemu nyingine kama vile ngozi nk. Na mchinjaji asipewe chochote katika nyama ile kama ni malipo kwa sababu kufanya hivyo itakuwa Swallah Llahu alayhi wa sallama na kumuuzia

Lakini kama mchinjaji atapewa sehemu yoyote kama zawadi au sadaka, hapo atakuwa na haki ya kuifanya atakavyo kama vile kuiuza nk. Lakini haruhusiwi kumuuzia yule aliyempa.

 

Islam Q&A (www.islam-qa.com)