NYUMA YA PAZIA

 

Kimeandikwa na Sheikh Muhamad Is-haq Sidiqi Nadwi

Kimetafsiriwa na Ibn Karim

 

Kimetangazwa na Ansaar Muslim Youth center Tanga, Tanzania

 

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehma Mwenye Kurehemu

 

Dibaji.

Shukrani zote ni za Allah (S.W.T) aliyetukuka, na rehma na amani zimshukie Mtume wa mwisho Muhammad (S.A.W) bora wa viumbe vyote, na sahaba zake (RA.) na ahli zake (RA) na wafuasi wake wa haki.

Vitabu na vijitabu vingi vimeandikwa na Mashia hivi karibuni ili kuwapoteza AhIu-Sunnah ambao si wajuzi wa dini yao au hawajui ukweli kuhusu dini ya Kishia. Ni kwa sababu hiyo mwandishi akaonelea kuwa ni kazi adhimnu na ni wajibu wake kuangazaWaislamu juu ya tofauti baina ya Mashia na Ahlu Sunnah kwa itikadi na ibada. Ninamuomba Allah (S.W.T) hali ya kunyenyekea: ‘Ewe Mola nionyeshe Rehma yako na uukubali huu utumishi wangu dhaifu kwa Uisilamu na nijaze kwa msamaha na rehma katika maisha yangu ya sasa na yale ya akhera na kijalie kitabu hiki kiwe ni chenye kufuzu na kuleta matunda mema kwa ikhwani. Ewe Mola Wewe ndiwe Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu.

Muhammad Is-haq Siddiqi Nadwi

Utangulizi

Uislamu ndiyo dini ya peke ambayo Allah (S.W.T) kwa rehma yake amewapa waja wake neema hiyo aliyoteremshiwa Mtume Adam (AS.) baba wa wanadamu

Kuna manabi na mitume -wengi waliotumilizwa baada ya Nabi Adam (AS) ambao walihubiri kulingana na maagizo waliyopewa. Allah (S.W.T) aliendelea kutuma mitume baada ya Adam (AS) mwishowe ikawa ni kuleta mtume wamwishona kitabu cha mwisho Al-Quran iwe ni muongozo kwa binadamu hadi siku ya mwisho.

Mtume Muhammad (S.A.W) aliishi miaka kumi na mitatu katika Makka akitumia nguvu zake zote kueneza dini ya Kiislamu.Wakazi wa Makka kama wakazi wengi wa bara la Arabuni, walikuwa washirikina wakawa Sahaba (R.A) zake na Wakagura (wakahama) naye hadi Madina. Hapo Madina kabla ya kuja Uislamu kulikuwa na makundi mawili ya kidini; washirikina na Mayahudi.

Washirikina walikuwa makabila mawili -Aus na Khazraj ambao baada ya kusilim waliitwa Answar. Mayahudi kwa kuwa wakijua hali ya mambo na kwa kuwa walipewa Taurat basi wao walihisabiwa kuwa ni bora kuliko washirikina ambao hawakuwa wasomi. Mayahudi walitumia hila yao ya "gawanya utawale” kuwatetesha Aus na Khazraj ili wawe ni madhaifu.Waliweza kufanya hilo kwa kusengenya jambo ambalo liliwafanya makabila hayo mawili kupigana, kumwaga damu na kuharibiana mali. Basi hapo hao washirikina waliendelea kuwa masikini na wanyonge ambapo ikawa rahisi kwa Mayahudi kuwanyonya damu zao. Ni kwa njia hiyo Mayahudi waliendeleza maisha yao.Tofauti kubwa zao za kidini hazikuwazuia washirikina kuwaheshimu Mayahudi

Na zaidi ya hayo Mayahudi ndio waliotawala uchumi na walikuwa wasimamizi wa Riba, na hao washirikina walishikilia kazi ya ukulima. Mayahudi waliweza kujiendeleza kiuchumi kwa kuwapa washirikina mikopo huku wakiwatoza riba kwa asili mia kubwa.

Idadi kubwa ya watu wa makabila ya Aus na Khazraj wakawa wafuasi halisi (Masahaba) wa Mtume (S.A.W) kabla ya kugura (kuhamia) Madina. Jambo hilo liIiwaudhi sana kwa sababu ubora wao juu ya Aus na Khazraj ulikomeshwa na uwezekano wa kuifanya Madina kuwa mji wao chini ya uongozi wa Abdullah bin Ubayya bin Salool haukupatikana.

Mayahudi walishangazwa kwa kuja Mtume katika kizazi cha Bani Ishaq kwani wao siku zote walidhania Mtume huyo wa mwisho a1iyebashiriwa katika Taurati angekuja katika ukoo waBani Ismail. Baada ya bishara hiyo ya hakika kuwafunukia, baadhi ya Mayahudi walisilimu kidhati lakini wengi wao hawakuweza kuepukana na husda, chuki na uadui wao dhidi ya Uislamu ndipo wakawa maadui wa Mtume (S.A.W). na sana sana maadui wa Qur'ani.

Kwanza kabisa walijitolea vilivyo kwa nguvu na mali zao kuumaliza Uislamu kupitia kwa mijadala na kwa hilo hawakufanikiwa. Baada ya hapo walianza kujitokeza kwenye medani wakiwa tayari kwa vita, hilo liliwatia aibu kwani walishindwa kabisa. Sasa Mayahudi walianza kutumia silaha yao 'mashuhuri' yaani unafiki. Kiongozi wa Mayahudi, Abdulla bin Ubayya bin Salool alikuwa mjanja tena hakuwa muaminifu, zaidi ya hayo alikuwa stadi katika uwanja wa udanganyifu. Kwa hivyo aliheshimiwa na wenziwe (Mayahudi) hapo Madina nakwengineko bara Arabuni. Huyo bwana (Ibn SalooI) alisilimu ili kuudhuruUislamu. Mwanzo kabisa alianza kukashifu Masahaba (R.A) ambapo alijuwa wazi- kuwa uaminifu wao ukitiliwa shaka na Waislamu basi watu wataitilia shaka hata usahihi wa Qur'ani na hadithi za Mtume (S.A.W), kwa hivyo Uislamu woteutavunjika vipande vipande.

Walijua kiyakini ikiwa Waislamu wazamazao hawatokubali zile propaganda zao dhidi ya Masahaba (R.A.), basi vizazi vijavyo wataanguka katika mtego wao. Mayahudi walianza kuwazulia Masahaba(R.A) na kutunga kila aina ya uongo ili kuharibu hadhi za Masahaba (R.A.) ikiwa moja wapo ya njama zao. Allah (S.W.T) mwenyewe akaokoa sifa njema za Masahaba (R.A) na akathibitisha kwa kauli Yake mwenyewe usahihi wa Qur'ani, hadithi za Mtume (S.A.W) na akazifichua nia mbaya za wanafiki.

Hilo halikuwazuia Mayahudi, bali waliendelea na njama zao za kisirisiri lakini Mtume Muhammad (S.A.W) kwa busara ya hali ya juu alibatilisha hila zao. Qur'ani Tukufu pia ikazidi kubaini sifa za Masahaba (R.A) na kuondoa doa kwa hulka yao njema. Si hilo tu bali iliendelea kuahidi ghadhabu za Allah (S.W.T) na uangamizaji kwa wenye kuwakashifu Masahaba (R.A).

Mayahudi walifukuzwa Arabuni kwa zile tabia zao dhidi ya Uislamu, kuleta rabsha na uharamia. Basi wakapata himaya huko Sham, Misri, Iran na nchi zingine. Waliishi miaka mingi uhamishoni, lakini nyoyo zao hazikutulia kuchomeka kwa bughudha zao dhidi ya Waislamu. Hawakuwasamehe Waislamu katu, na uadui wao kwa Waislamu ulibaki kwenye nyoyo zao. Siku baada ya siku walifikiria njia za kulipiza kisasi kwa kile walichotendewa.

Ili kutekeleza hilo,walimchagua Abdulla Ibn Saba ili kupinduwa serikali ya Kiislamu (Ukhalifa), na kupanda mbegu za kuwafarakanisha Waislamu. Abdulla bin Saba akajiunga na ummati wa Kiislamu kwa vao la Uislamu akijifanya walii kumbe nia yake fasiki bado angali anayo.

Kwa kutumia 'uwalii' wa uongo aliweza kupata wafuasi wengi kwa muda mchache, hasa wale waliosilimu karibuni ambao hawakuwa na ujuzi wamafundisho ya Kiislamu au elimu yao ilikuwa ya kiasi kidogo.

Ushia vilevile unajulikana kwa jina Ia mwanzilishi wake "USABA!" Kuna ushuhuda madhubuti wa kihistoria kuhakikisha kuwa Uyahudi ndio chanzo cha

Ushia na muasisi wa dini hiyo ni Abdalla Ibn Saba. Abdullah Ibn Saba aliushambulia Uislamu maradufu, shabaha yake ya kwanza ilikuwa ni imani thabiti ya Waislamu, na ya pili ikiwa ni hali yao imara ya kisiasa na kijamii. Ili kuweza kuwashawishi Waislamu waepukane na mafundisho ya haki ya Uislamu, ilimlazimu kutia sumu kwenye nyoyo za wafuasi wake dhidi ya Masahaba (RA) ambao waliongoza maisha yao kulingana na Qurani na Sunnah.

Vile vile ilimlazimu kutia shaka usahihi wa Qur'ani. Kuweza kuangamiza hali imara ya kisiasa ilimbidi apindue ukhalifa kwa njia yoyote. Haikuwa ngumu kwa mtu mjanja kama Ibn Saba kutekeleza jambo kama hilo.

Baadhi ya Waislamu walijiunga naye hali kutojua na wengine kwa thamani ya pesa. Mipango dhidi ya Uislamu ilianzishwa kwa utaratibu. Mwanzo kabisa aliwateka akili kwa kuwafundisha imani na itikadi zisizoshikamana na Uislamu huku akiwapa fikra kuwa yale aliyowafundisha ndiyo Uislamu sahihi na wale wasioyafuata ni maadui wa Uislamu. Kwa mahubiri yake aliweza kupata wafuasi wengi kwenye kundi la kisiri Ia siasa likishirikisha dini ili kusambaza itikadi zisizolingana na Uislamu na kuumaliza ukhalifa kwa kutumia sanaa ya ulaghai na usaliti.

Kila dini inapendekeza kanuni ya nidhamu kwa wafuasi wake na kanuni hiyo ni maamrisho na makatazo. Lakini hakuna dini yoyote iliyopendekeza na kukubali kusema uongo, udanganyifu, kusengenya na nyengine mithili ya hizo. Kwa vile dini ya Ibn Saba haikuwa chochote isipokuwa unafiki, yeye binafsi alitumia hila zote habithi akawasihi wafuasi wake watumie hayo dhidi yaWaislamu. Alitumia njia tofauti ikitegema kule walitoka na elimu yao, kwa mfano wengine aliwaambia kuwa Ali (R.A) ni 'Wasii wa Mtume (S.A.W)’ na kwamba yeye peke yake alistahiki kuwa khalifa baada ya Mtume (S.A.W) na wale Makhalifa (RA) wengine kabla yake waliupata kinguvu nguvu huku wamemnyima Ali (R.A) haki yake.

Kulingana na yeye ilikuwa ni wajibu wa kidini kupigana na yale matendo mabaya Ali (R.A) aliyoyapata. Hakukomea hapo bali aliendeleya kusema kuwa Ali (R.A) hakuwa binadamu, bali alikuwa ni kiwiliwili cha Allah (S.W.T) kwa umbo Ia binadamu! Kwa vile lengo lake lilikuwa kuchafua akili za Waislamu dhidi ya Masahaba waongofu (R.A). Huyu bwana alikuwa tayari na njama mpya ili aweze kutekeleza shabaha yake.

Inafahamika kutokana na ushahidi wa kihistoria uliotajwa hapo awali kuwa Ushia ulianzishwa na Mayahudi ukiwa ni mwendo usioambatana na Uislamu na lengo kuu lilikuwa ni kuharibu mafundisho hasa ya Uislamu, na kufuta imani tukufu ya Uislamu ili kumaliza umaarufu wake

 

SURA YA KWANZA

Misingi ya dini ya kishia

Kwa jumla, inaitakidiwa na Waislamu na pia wasiokuwa Waislamu duniani kuwa Ushia ni pote la Uislamu na kuwa hakuna tofauti katika misingi ya imani ya Kisunni na imani ya Kishia. Itikadi hii ni ya makosa mno na inaonyesha namna Waislamu

Masunni walivyo wajinga juu ya dini yao wenyewe na ile ya Kishia pia.

Utafiti wa dini ya Kishia utabainisha wazi kuwa, badala ya kuwa pote katikaUislamu, Ushia ni dini ya kipekee na iliyo tofauti na Uislamu wa Masunni. Kwa hakika Ushia ni pote Ia Uyahudi ambao uliimarishwa kierevu kwa kutumia jina la Uislamu ili uende sambamba na Uislamu. Hii ilikuwa ni katika njia ya kuwahadaa Waislamu kutoka kwenye mafundisho yao ya sawa ya Uislamu kama ilivyojadiliwa hapo juu.

Ushia unakanusha misingi yote na itikadi tukufu ya Uislamu. Mashia wanadai kuwa ni Waislamu, lakini itikadi zao hazikufarikiana na misingi ya mafundisho ya Uislamu tu bali pia ni uadui, uvunjifu na uchochezi kwa Uislamu na Waislamu. Madondoo kutoka kwenye vitabu vyao vyenyewe vya kidini, ambavyo vinakubaliwa na maulamaa wote wa kishia kuwa ndivyo vyenye uthabiti na vya kutegemewa.yatatoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Uislamu wao si Uislamu bali ni usimango wa Uislamu.

 

Je mashia wanaiamini Qurani Tukufu?

Kuna vyanzo viwili pekee vya elimu yote ya Uislamu: ya kwanza ni Quran Tukufu na nyengine ni Sunna ya Mtume (S.A.W). Qur'an Tukufu, ambayo ni neno Ia Allah (S.W.T) ndiyo muhimu zaidi na chanzo chenye neno tamma cha elimu,ambapo Sunna za Mtume (S.A.W) zinafuatia na zimeambatana na elimu na mafundisho ya Quran Tukufu. Sisi Waislamu tunaitakidi kuwa Quran Tukufu, kama tuliyonayo wakati huu, iliteremshwa na Allah (S.W.T) kwa Mtume Muhammad (S.A.W). Tunaitakid kuwa hii ni Qurani Tukufu ile ile ambayo iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na hakuna chochote kilichoongezwa wala kilichopunguzwa. Imekabidhiwa kwetu bila ya mabadiliko, maongezo au kutiwa maneno yoyote. Ni Quran Tukufu hiyo hiyo ambayo iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na akaifundisha kwa Masahaba (R.A) wake ambao waliihifadhi na wakaisoma pamoja na wafuasi wao. Tunaitakidi pia kuwa Quran Tukufu haitaongezwa chochote mpaka mwisho wa ulimwengu kwa vile Allah (S.W.T) Mwenyewe ameahidi kuulinda usafi (asili) wake.

Kuitaikidi ukamilifu, usafi na uthabiti wa Quran Tukufu, ni itikadi ya msingi na imani ya wajibu ya Uislamu. Itikadi hii ni muhimu sana hata ikawa pindi Muislamu anapoitilia shaka uthabiti wa Quran Tukufu, papo hapo anatoka kwenye Uislamu. Wajaribiwapo Mashia juu ya itikadi hii ya Uislamu, tunawapata na hatia ya ukafiri, kwa sababu wanaamini kuwa Quran Tukufu, kwa wakati huu si Quran ile ile aliyoteremshiwa bwana Muhammad (S.A.W).

Wanaitakidi kuwa mabadiliko chungu nzima na maongezo yalifanywa kwenye Quran kabla ya kukabidhiwa vizazi vilivyofuata. Wanaitakidi kuwa Quran Tukufu ilitiwa maneno yasiyokuwemo na Masahaba (R.A) wa Mtume (S.A.W).

Maulamaa na Mujtahidi wa Kishia ambao wanatambuliwa na takriban Mashia wote ulimwenguni kuwa ndio wenye kutegemewa zaidi na wenye uthabiti kwenye kazi zao, wameandika kwenye vitabu vyao kwa maneno waziwazi kabisa kuwa Quran Tukufu kama tuliyonayo wakati huu si kamili bali imeongezwa maneno yasiyokuwemo.

Hata hivyo, kabla sijatoa madondoo kutoka kwenye vitabu vyao, ningependa kuwaomba wasomaji wajiulize wenyewe: Mashia, ambao wanaitakidi kuwa Quran Tukufu imefanyiwa mabadiliko na kutiwa maneno yasiokuwemo, kweli wanaitakidi Qurani Tukufu kama tunavyoitakidi sisi? Iko haja kwao kujitakidi Quran ambapo wanaichukulia kuwa imetiwa maneno yasiyokuwemo? Jee,twaweza kumuamini Shia anaposema kuwa anaitakidi Quran Tukufu kama vile sisi? Sisi Waislamu tuna fahari ya ukweli, uaminifu, kutokuwa na ubinafsi, roho safi, uchamungu na unyenyekevu wa Masahaba (R.A) wa kwanza wa Mtume wetu (S.A.W).

Tabia zao njema na uadilifu wao ulioambatana na njema zao nyingi nyinginezo, hauonyeshi ubora wao wenyewe pekee, bali hata sifa za uongozi wa bwana Muhammad (S.A.W), ambae kutokana na mafundisho yake Masahaba (R.A) hao walipata sifa hizi. Tabia zao ni bora na mfano mwema kwa Waislamu wote ulimwenguni. Hawa ndio Masahaba (R.A) waliokabidhiwa wadhifa wa kuihifadhi na kuifundisha Quran Tukufu.

Sisi Waislamu twamshukuru Allah (S.W.T) kwa kuwakabidhi wadhifa au jukumu hilo la kuhifadhi Quran Tukufu watu hao waaminifu. Mbali na itikadi yetu Mashia wanaitakidi kuwa Masahaba (RA) hao hawakuwa Waislamu bali wanafiki na maadui wa Uislamu. Wanaitakidi kuwa Masahaba (R.A) wote walikuwa wanafiki isipokuwa bwana Ali (R.A), Fatima (RA), Hassan (R.A), Hussein (R.A),Miqdad (R.A), Abudhar (R.A) na Ammar (R.A).

Kulingana na vitabu muhakkam vyadini ya Kishia, Masahaba (RA) wote isipokuwa waliotajwa hapo juu,walibadilisha imani zao na wakawa makafiri baada ya kifo cha Mtume Muhammad (S.A.W)

Anasema mwandishi wa Rijal-eKashi', mmoja kati ya maulamaa wa kuaminika katika Ushia:

"Watu wote walikuwa makafir isipokuwa watatu ambao ni Salman, Abudhar na Miqdad.” (UK. 8) maneno hayo yametajwa Katika Haququl Yakeen, UK. 255, na tafsiri ayashi mjalada I UK. 199 chapa Tehran

Hili ni dondoo moja tu kutoka kwenye kitabu cha Shia kuonyesha fikra ya Mashia juu Ya Masahaba (R.A). Vitabu vya Maulamaa wa Kishia vimeambatana na tarifa kama hizi juu ya Masahaba(R.A) ambao waliikusanya Quran Tukufu.

Dai la Mashia kuwa wanaiamini Quran Tukufu ni unafiki mtupu uliodhamiriwa kuwahadaa Waislamu. Vipi Mashia wataiamini Quran Tukufu hali wanawachukulia wakusanyaji wake kuwa wanafiki, wasioamini, makafiri na maadui wa Uislamu? Kwa hivyo inaweza kusemwa kuwa Mashia wanaitakidi Quran Tukufu kinafikitu na wanafanya Taqiyya (ruhusa ya kuhadaa). Kwa hakika ni maadui wa Quran Tukufu lakini kwa sababu ya umbile lao la Uyahudi hawailaumu.