WAISLAM WOTE NI NDUGU

Ndugu zangu Waislam

Assalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Sababu kubwa ya kudhalilika kwa umma wa Kiislam na kushindwa katika wakati wetu huu ni chuki iliyochipukizwa ikakuzwa na kuenezwa baina yetu.

Mtume (SAW) alisema;

"Mtakuja kuzungukwa na mataifa, kama walaji wanavyoizunguka sinia ya chakula".

Wakamuuliza;

"Kwa ajili ya uchache wetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

Akasema;

"Laa - bali nyinyi mtakuwa wengi wakati huo, lakini mtakuwa mfano wa takataka zinazosukumwa na mkondo wa maji ya mvua. Na Mwenyezi Mungu ataiondoa haiba mliyokuwa nayo kutoka katika nyoyo za adui yenu na ataingiza katika nyoyo zenu 'Wahan'".

Wakamuuliza;

"Ni nini hicho kinachoitwa 'wahan', ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?"

Akasema;

"Kuipenda kwenu dunia, na kuyachukia kwenu mauti".

Wakati huu tulionao ndio wakati alioutaja Mtume (SAW) kuwa ni wakati tutakapokuwa mfano wa takataka zinazosukumwa na mkondo wa maji ya mvua, kila mmoja anamchukia mwenzake, kila mmoja anasema;

"Nasfi yangu nasfi yangu"..

Hapo mwanzo Waislam walikuwa umma mmoja unaopendana na kusaidiana. Muislam akiumizwa au kudhurika popote pale ulimwenguni, basi Waislam wote popote pale walipo walikuwa wakihisi na kuathirika pamoja naye.

Hivi ndivyo tunavyotakiwa tuwe.

Mtume (SAW) amesema;

"Mfano wa Muislam na Muislam katika kupendana kwao na katika kuoneana huruma kwao ni mfano wa mwili mmoja. Kinaposhitaki kiungo kimoja (kinapoumwa), basi mwili wote unashirikiana nacho kiungo hicho katika kupata homa na katika kukesha".

Makafiri (crusaders) walipoingia katika nchi za Kiislam, walianza kueneza fitna hizi za kuwatenganisha Waislam katika utaifa na kuwaita katika kuunda kila taifa umoja wa taifa lake, badala ya umoja wa Kiislam waliokuwa nao wakati huo chini ya Khalifa mmoja

Baada ya kuishinda nchi ya Uturuki katika vita vya mwanzo vya ulimwengu makafiri wakaishurutisha na kuifunga dola hiyo kwa mikataba mbali mbali ya kuwataka wavunje uhusiano wao na nchi za Kiislam, kuuondoa utawala wa ki Khalifa wa Kiislam, kuahidi kuuzima moto wa harakati zozote za Kiislam na kujichagulia nchi hiyo ya Uturuki sheria nyingine badala ya ile ya Kiislam waliyokuwa nayo.

Makafiri hawajakubali kuondoa majeshi yao ndani ya nchi hiyo mpaka pale Kamal Ataturk alipoyakubali masharti yote hayo na kuyatimiza..

Katika nchi za Kiarabu, makafiri wakapata baadhi ya viongozi waliowalea na kuwasomesha wao wenyewe na kuwatayarisha kwa ajili ya jukumu hilo. Wao nao wakaunda umoja wa nchi zao. Umoja wa nchi za Kiarabu, na Waturuki nao wakaunda utaifa wao, Wakurdi nao wakaanza kupigania utaifa wao na kila taifa likaanza kuita watu wake katika kujitenga mbali na mwili huu mkubwa wa Uislam na kuunda umoja wao na kuusahau umoja wao wa asili, umoja wao unaowaunganisha wote hao chini ya kamba ya Mwenyezi Mungu yenye nguvu.

Chuki na mfarakano zikazidi kuchochewa na kuenezwa baina ya Waislam na kutiliwa nguvu na wakoloni hao mpaka kufikia hali hii tuliyonayo hivi sasa wakati huu ambapo hapana tena Muislam anayehisi maumivu anayopata Muislam mwenzake, isipokuwa wachache alowarehemu Mola wao.

Ndugu zangu Waislam, Uislam umekuja kuondoa yaliyo batili, kuondoa chuki na mfarakano baina ya watu na kuwaunganisha chini ya bendera moja, bendera ya Laa ilaaha illa Llah, na kuleta yaliyo sahihi, undugu, kupendana na kuwa kitu kimoja kwani wanadamu wote asili yao ni moja.

Mwenyezi Mungu anasema;

"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja - Adam) na mwanamke (mmoja - Hawa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbalimbali) ili mjuane (tu basi; siyo mkejeleane) Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi".

Al Hujurat - 13

Mwenyezi Mungu anatujulisha hapa kuwa kuwaumba watu katika mataifa mbali mbali na makabila mbali mbali kwa ajili ya kujuana tu, na si kwa ajili ya kutafakhariana au kuchukiana, na kwamba mezani anyaoitumia Mwenyezi Mungu katika kuwapima waja wake ni Ucha Mungu wao na si mataifa yao.

Mwenyezi Mungu pia akasema;

"Kwa hakika Waislam wote ni ndugu".

Al Hujurat - 10

Wakati wa Mtume (SAW) hapakuwa na tofauti baina ya mwarabu na asiyekuwa Mwarabu. Wote walikuwa Waislam chini ya uongozi wa Mtume wao Muhammad (SAW)..

Hapakuwa na tofauti baina ya Abubakar mwarabu na Suleiman Al Farsiy - aliyetoka nchi ya Farsi (Iran sasa) wala baina ya Bilali Mhabeshi na Suhaib Mrumi, na watu wa mataifa mbali mbali walikuwa wakiingia katika dini hii tukufu bila kuhisi kuwa pana tofauti yoyote baina yao, bali walikuwa wakihisi kuwa wote ni ndugu na umma moja.

Siku ile Mtume (SAW) alipoingia na majeshi yake kuuteka mji wa Makka, na baada ya kusafishwa msikiti wa Makka kutokana na masanamu yaliyokuwa yamejaa humo, aliingia msikitini na kuufunga mlango akiwa yeye na Bilali na Osama (RA) peke yao ndani ya msikiti, na kuwaacha watu wa kabila lake na watu wa nyumba yake pamoja na Masahaba wakubwa wakubwa kama vile Abubakar, Omar, Othmn na Ali (RA) nje ya msikiti.

Bilal na Osama (RA) wote walikuwa watumwa kabla ya Uislam.

Na katika hadithi, Mtume (SAW) alimuuliza Bilal (RA);

"Nielezee juu ya amali njema kabisa unayoitenda, kwani nimesikia sauti ya viatu vyako vikiwa mbele yangu Peponi?"

Bilal (RA) akajibu;

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sijafanya amali yoyote niliyoiona kuwa ni bora kwangu isipokuwa kawaida yangu mimi kila nikitawadha husali kadiri ninavyojaaliwa kusali".

Bukhari

Ama Osama bin Zaid (RA) yeye alikabidhiwa na Mtume (SAW) uongozi wa jeshi kubwa ambalo ndani yake walikuwemo Masahaba wakubwa wakubwa kama vile Omar bin Khattab (RA) na wengine.

Hawa wote walikuwa watumwa kabla ya Uislam, lakini Mtume (SAW) alitenda haya ili iwe ni dalili kuwa Uislam una upofu wa rangi (colour blind). Hakuna kitu katika Uislam kinachoitwa huyu Mwarabu na huyu si Mwarabu.

Mwenyezi Mungu anasema;

"Na hatukukutuma ila kwa watu wote".

Saba - 28

Na akasema;

"Ni Mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule aliyeteremsha Qurani kwa mja wake ili awe Muonyaji kwa walimwengu (wote)".

Al Furqan - 1

Na akasema;

"Na saidianeni katika wema na taqwa, wala msisaidiane katika dhambi na uadui".

Suratul Maidah - 2

Ndugu zangu Waislam - jueni kuwa makafiri ndio walioianzisha dola ya Kiyahudi katika moyo wa nchi za kiarabu kwa ajili ya kuudhoofisha umma wa Kiislam na kuwasaidia Mayahudi hao kwa hali na mali mpaka wakaifanya kuwa ni dola kubwa yenye nguvu za silaha za nuclear.

Wakaipa nguvu dola hiyo na kusababisha vita vikali baina yao na baina ya dola za Kiislam kama vile Misri, Syria, Algeria, Libya, na Waislam kutoka nchi mbali mbakama vile Pakistan, Afghanistan na kwengineko walishiriki katika vita hivyo na roho kwa mamilioni.

Nchi za kikafiri zinajaribu kufanya kila njia ili kueneza chuki baina ya Waislam kwa kuhofia wasije kuungana tena siku moja na kurudi tena kuwa taifa kubwa lenye nguvu kama lilivyokuwa hapo mwanzo lilipokuwa likiwahami Waislam kutokana na tamaa na jeuri zao makafiri hao.

Ndugu zangu Waislam, jueni ya kuwa Myahudi ni adui mkubwa wa Waislam na haijuzu kwa Muislam kumfananisha Myahudi na Muislam mwenzake hata awe amemkosea namna gani, na haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala.

Mwenyezi Mungu anasema;

"Hakika utawakuta walio maadui zaidi kuliko watu (wengine) kwa Waislam ni Mayahudi na wale mushirikina."

AL Maidah - 82

Mtume (SAW) amesema;

"Hiwezekani Myahudi abaki peke yake na Muislam mahali isipokuwa atatamani amuue".

Ibni Mardaweya

Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hivi sasa harakati nyingi za vijana wa Kiislam zimeanza zikiwaita watu katika kurudisha umoja wao na kufuata mafundisho sahihi ya Kiislam na kurudi katika Uislam sahihi alokuja ule Mtume wetu mtukufu (SAW), na kuwatahadharisha juu ya hatari ya kuendelea kuikubali na kuieneza ile chuki iliyopandishwa na kuenezwa na makafiri ndani ya moyo wa umma huu wa Kiislam.

Tunaona katika kila nchi, kuanzia Uturuki kuelekea nchi za Kiarabu mpaka Afrika na Ulaya, sehemu zote hizo vijana wa Kiislam wamesimama imara katika kueneza shughuli za daawa zinazoamsha watu na kuhuisha nyoyo pamoja na kuwafumbua macho Waislam ili wapate kuujuwa Uislam ulio sahihi, na kwa ajili hiyo makafiri wakastushwa na kukasirishwa na harakati hizo.

Tunaweza kuona matunda ya harakati hizo katika mambo mbali mbali mfano;

Misikiti inayojaa waumini kwa ajili ya Sala na pia kwa ajili ya kujifunza mafunzo ya dini.

Wanawake wengi wamerudia kuvaa nguo zinazowasitiri pamoja na hijabu ya Kiislam na kushikamana na mafundisho ya dini.

Watu wanaingia katika dini hii makundi kwa makundi katika kila pembe ya dunia.

Katika kila nchi utasikia juu ya Waislam wanaowataka viongozi wao kuzibadilisha sheria zilizowekwa na wanadamu na badala yake kuirudisha sheria iliyowekwa na Mwenyezi Mungu.

Mikutano ya Kiislam inayofanyika kila sehemu ulimwenguni baina ya mataifa mbali mbali pamoja na nishati mbali mbali katika kutafuta kuurudisha umoja wao huo na katika kutafuta elimu ya dini na mafundisho mbali mbali yanayoongeza Imani.

Kwa ajili ya kuendeleza daawa hii, inampasa kila Muislam aache kufuata yale yaliyoingizwa na makafiri katika kuleta chuki na mfarakano, na badala yake wasaidiane na kujifunza mafundisho ya dini yao kwa ajili ya kumjenga Muislam mwema anayeweza kutambua baina ya haki na batili kupitia katika mafundisho ya Qurani tukufu.

Wassalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Ndugu yenu

Muhammad Faraj Salem